travelme2014
Member
- Aug 7, 2022
- 5
- 3
MAKALA: SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Miaka 200 iliopita yaani mwaka 1822 hakukuwa na kiwango kikubwa cha maendeleo ya sayansi na teknolojia. Nchi nyingi duniani hazikujua kuna jambo gani linaloendelea upande mwingine wa dunia. Kulikuwa na changamoto kubwa ya kupata tiba, usafiri, mawasiliano, nishati na kilimo chenye tija.
Licha ya changamoto hizo kubwa duniani, bado watu hawakukaa tu bure bila kutafuta maarifa na kufanya uvumbuzi na ugunduzi kwenye sayansi na teknolojia.
Hapa ndipo tunakuja kuona kwanini sayansi na teknolojia inapokuja kuwa ni muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwanini Sayansi na Teknolojia ni muhimu?
Ni muhimu sana kwasababu imekuja kuleta maisha ya kisasa, imeunganisha watu wa tabaka zote duniani bila kujali mipaka ya nchi iliyopo duniani kote. Imekuja kuleta ustarabu mpya wa maisha yetu ya kila siku. Imesaidia kuleta maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na makundi ya watu. Imekuwa si rahisi tena kutamani kurudi nyuma kwenye miaka ya 1822.
Mwaka 1957 dunia iliingia katika mabadiliko chanya baada ya kurushwa kwa Satelaiti ya kwanza kwenda anga za juu. Ilikuwa ni mwendelezeo wa uvumbuzi na ubunifu vya vifaa vya mawasiliano duniani.
Sasa jamii mbalimbali duniani zilianza kuwasiliana kwa njia ya simu kutoka eneo moja hadi lingine, na kutumia huduma za intaneti kuanzia mwaka 1989, Jambo ilo likaifikia Taifa letu miaka 1990 na kufikia mwaka 1994 kampuni ya kwanza ya simu ya mawasiliano ya simu za mkononi ikaingia nchini, inayojulikana sasa kwa jina la Tigo Tanzania.
Kwa hakika mawasiliano yamefanya dunia yetu kuwa kijiji. Pia, zimerahisisha kwenye huduma za kitiba, sasa madaktari wanaweza kuwasiliana kupitia simu au intaneti kutuma taarifa za kitiba za mgonjwa na hivyo kusaidia kutoa huduma bora na za kisasa kwa wagonjwa.
Sayansi na teknolojia kwenye usafiri:
Gari ya kwanza iliundwa nchini Ujerumani kati ya mwaka 1885 – 1886. Na mwaka 1903 kuliundwa ndege ya kwanza duniani. Uvumbuzi huo ulikuja kuleteta mabadiliko makubwa katika ulimwengu usafirishaji. Dunia ilipata gari ya kwanza na ndege miaka kadhaa baade, hiyo haikuwa mwisho badala yake uundaji wa magari na ndege za aina mbalimbali uliendelea. Na mnamo 1933 gari ya kwanza ilisajiliwa Tanganyika wakati huo, ambayo sasa ni Tanzania, tukawa tumeingia katika ulimwengu mwingine kuonja faida za sayansi na teknolojia kwenye usafirishaji.
Sayansi na Teknolojia kwenye nishati:
Mwaka 600BC mtu wa kwanza aligundua nishati ya umeme duniani, na 1700 ikavumbuliwa mashine ya kwanza ya kuzalisha umeme. Sayansi na teknolojia imeleta mabadiliko makubwa kwenye nishati hata hapa Tanzania, Mnamo mwaka 1964 kulianzishwa shirika la umeme (Tanesco) ili kuzalisha nishati ya umeme. Tanesco imesaidia kuleta maendeleo kwa jamii yetu, ikiwepo kuja wawekezaji nchini ili kuwekeza kwakuwa kumekuwa na nishati ya uhakika, imesaidia vijana kwa wazee kujiari au kutoa ajira kwa wengine kupitia uanzishwaji wa viwanda vidogo na vikubwa. Hayo yote ni matokeo ya sayansi na teknolojia.
Changamoto
Taifa letu linakabiri changamoto kubwa katika sekta ya Sayansi ya teknolojia licha ya kuwa na vyuo vingi vilivyojikita katika elimu ya juu ya sayansi na teknolojia. Kumekuwa na matokeo hasi baada ya wanachuo wengi wanaohitimu kutoka katika vyuo hivi, wengi wao wameshindwa kujiari ama kuajiriwa. Hii imetokana na elimu waliopata imekuwa haihakisi hitaji la soko na kufanyaja vijana wengi kukaa nyumbani. Aidha vyuo vingi vimekosa vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujikuta ikifundisha wanafunzi kwa kutumia vifaa vilivyopitwa na wakati/chakavu. Matokeo ni kutoa vijana wasioweza kuleta ushindani.
Changamoto si kwa vyuo vya elimu ya juu tu bali hadi kwenye elimu ya msingi. Tunajua elimu ya msingi ndiko kwenye mizizi, watoto wakianza kufundishwa huku chini kuhusu sayansi na teknolojia basi huku juu itakuwa rahisi kuwaandaa wataalamu wenye matokeo chanya na kutengeza soko la ajira kwa vijana.
Nini kifanyike kufanikisha?
Serikali na wadau wengine waungane pamoja kuhakikisha kuna miundo mbinu ya kutosha kutoa elimu bora, viwepo vyumba vya madarasa vya kutosha, madawati, vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia, walimu wa kutosha kwenye masomo ya sayansi na teknoloji, hii ikitia ndani walimu ya masomo ya hesabati. Umeme wa uhakika katika shule zote nchini (Kufungwe mifumo ya nishati ya Jua kama hakuna miundo mbinu ya umeme wa Tanesco), maana bila umeme ili halitafanikiwa kwa urahisi. Shule zote zipate maabara na vifaa vyote vya majaribio ya kisayansi.
Iundwe mitaala itakayosaidia watoto kujifunza tangu wakiwa shule ya awali na hii itapelekea kuwa na vijana wenye uwezo mkubwa wa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii kupitia sayansi na teknolojia na kuzifanya kuwa zenye tija na kuzalisha ajira nyingi zaidi kwa vijana wenzao.
Mfano: Kampuni za simu hapa Tanzania, zimetumia sayansi na teknolojia kubuni njia ya kutuma na kupokea pesa kupitia njia ya simu kutoka mtu moja kwenda kwa mtu mwingine, ubunifu huo uliweza kuzalisha maelfu ya ajira kwa vijana Tanzania na hivyo kuweza kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.
Pia, serikali itenge bajeti maalumu ya kusaidia vijana wote wanaobuni au kufanya uvumbuzi fulani kwenye nyanja ya sayansi na teknolojia, iwe kijana amebuni gari, mashine, ndege au kifaa chochote ili kiwe endelevu kwa ajili ya kuitangaza nchi na kuongeza ajira kwa vijana.
Kuwe na mbinu bora ya kuibua vipaji vya vijana kwenye maswala ya sayansi na teknolojia na kuendelezwa kwenye elimu katika nchi ambazo zimepiga hatua kubwa katika sayansi na teknolojia na kisha vijana hao kurudi nchini ili kuwajengea vijana wengine uwezo wa vipawa vyao.
Leo, tunanunua bidhaa nyingi kutoka nchi za mbali, zilizobuniwa na watu wengine, lakini sasa tununue bidhaa zilizobuniwa na Tanzania. Lakini ilo litafanikiwa tu ikiwa serikali pamoja na wadau wengine watawekeza kwa nguvu zote katika sayansi na teknolojia. Mwanzo mwa makala yangu nimetoa mifano ya uvumbuzi na ubunifu kutoka nje ya Bara la Afrika ambao leo wametufanya tuone umuhimu wa sayansi na teknolojia katika kutatua changamoto za kijamii.
Tukumbe tayari Taifa letu limekuwa na wabunifu kadhaa kwenye sayansi na teknolojia, tukiwaona kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Watu hawa wakishikwa mkono na kusogezwa mbele zaidi ya hapo walipo watazalisha ajira zaidi kwa vijana wenzao.
Mwisho sayansi na teknolojia ndio njia ya maisha ya mafanikio kwenye ulimwengu wa kisasa, kumekuwa na ushindani mkubwa hata katika nchi za kiafrika, nasi tuingie katika ushindani huo ili kuongeza ajira kwa vijana wetu.
Makala hii imendikwa na:
TRAVELME2014
Nawakilisha kwa wadau

Attachments
Upvote
1