Mafanikio ya CHADEMA kwa kivuli cha maandamano

Mafanikio ya CHADEMA kwa kivuli cha maandamano

sangaone98

Member
Joined
Apr 16, 2024
Posts
77
Reaction score
107
Rais Samia Januari 2023 wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya kisiasa, katika kikao kilichofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa tamko la kuruhusu shughuli za nje za kisiasa, ikiwemo mikutano ya hadhara.

Wengi waliamini ndio mwanzo mpya wa uhuru wa kisiasa nchini Tanzania, baada ya kipindi kirefu cha shughuli za kisiasa za upinzani kuwa kifungoni. Swali la ikiwa maandamano ya jana yamefanikiwa au la, bila shaka litakuwa na jawabu tofauti, kulingana na nani unaye muuliza.

Kwa ambaye anataka maandamano yawe chanzo cha serikali kurudi nyuma na kubadili msimamo, na matakwa ya wanaoandamana yatekelezwe, jawabu itakuwa, ‘bado maandamano haya hayajafanikiwa.’

Pia soma: Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024

Lakini kwa upande wa utawala, kuzuia maandamano inaweza kuingia katika hesabu ya ushindi, ingawa kwa nchi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikituhumiwa kwa kukandamiza shughuli za upinzani, kuuhesabu huo kuwa ni ushindi, kwa hakika ni namna mbovu ya kuhesabu ushindi.

Wakati Chadema inashindwa kweli kufanikisha kile wanacho kitaka – yaani kuandamana hadi viwanja vya Mnazi Mmoja, lakini inafanikiwa kuuonesha ulimwengu kile kinachosemwa kuhusu ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa nchini Tanzania

Source BBC swahili
 
Back
Top Bottom