Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 11,786
- 18,562
Diamond Platinum amezidi kuonyesha ubora wake si kwa Tanzania tu bali Africa na ulimwengu mzima... Ubora huo unaonekana kwenye tunzo mbali mbali anazozidi kunyakua kadri siku zinavyosonga, kinachonisikitisha zaidi ni kwamba nyimbo zinazomfanya achukue tunzo hizo za kimataifa ndo zile zile ambazo zilitumiwa na KTMA ambapo aliambulia baadhi ya tunzo chache tu na zingine kwenda kwa mtu asiyestahili wakati ni wazi kabisa zilikuwa zake,... Hii ni aibu kubwa kwa KTMA natumai siku nyingine watakuwa na weledi zaidi kuliko kuendeshwa na hisia za mashabıki.