Mafanikio ya mkato katika maisha kwa wadada zinaumiza ndoa za watu

rubwe

Senior Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
109
Reaction score
25
Wapendwa habari?

Jamani wadada acheni tabia ya kuharibu ndoa za watu kwenye ushirikina acheni tamaa za kijinga mnatesa familia za watu mkishaona mwanaume ana uwezo akikutongoza tu tayari mke wake na watoto waandike maumivu hii tabia ni mbaya isitoshe kila mtu ana mume wake aliyeandikiwa na Mungu.

Unapoharibu ndoa ya mwenzako kichawi kumbukeni hiyo itakuwa ni Neema ya muda ambayo kinyume matakwa ya Mungu Mwisho wa siku mnaweza kuishia kwenye matatizo zaidi wewe kama umetongozwa ishi nae tu kawaida usisalitishe kwake na kuangamiza familia yake kishirikina ni dhambi na Mungu hapendi.

Ni ushauri tu nimeguswa siku hizi wanandoa wengi wanalia shauri ya hii tabia hasa kipindi hiki waharibifu wakuu ni wasichana.
 
Aah mabinti waache ushirikina na wale walio kwenye ndoa waheshimu wenzi wao na viapo vya ndoa zao

Mnajua kabisa kuna watu wapo tu kuharibu ndoa zenu, inakuwaje tena mnaenda kuwatongoza? Tulieni njia kuu, michepuko sio dili
 
Usipoteze muda wako kuamini kitu ambacho hakipo. Hakuna kitu kama 'uchawi' ni mentality tu unaiweka kichwani kwako.

Pia, somo la uaminifu liende kwa wanandoa. Waachane na mambo ya usaliti.

Hio michepuko haiwezi kuwepo kama hakuna wa kuwachepukia.
 
wnandoa heshimuni ndoa zenu .... hilo swala la kulogwa kama hujatongoza huwezi logwa.. dawa hapa kama umeoa achana na michepuko la sivyo UTALOGWA TU HAKUNA NAMNA NYINGINE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…