MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,727
- 6,615
Muunge mkono wewe na mkeo, usitupangie mtu wa kumuunga mkono kwani akili na utashi ni wa kwetu peke yetu na sii vinginevyo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kupitia Press alizofanya, Nape mpaka sasa anaonekana kusapoti kutimuliwa kwake kwa madai kua hakuiomba nafasi hiyo, hana kinyongo blah blah blah nk.
However, waandishi wanaguswa na kuumizwa, wakati Muhusika mkuu ambaye ndiye mwathirika ametaka tumuunge Mkono Magu na yeye hana kinyongo.
Kwangu Mimi kumuunga mkono Rais ni pamoja na kuunga mkono 100% kutumbuliwa kwa Nape na ku sapoti Uteuzi wa Magu kwa 100%.
It's a way easy. Kwasababu Nape amevuna alichopanda.
Sio siri, Nape ananuka ukijani. Nape hana hisia na matatizo wapatayo wapinzani 100%. kwa yeye kutishiwa bastola, ni sawa kabisa hata kama jamaa ange pull the trigger.
Kwasababu Dubwana hili walilisuka wao wenyewe. Hawajawahi kuonja machungu, angalau kwa kiasi sasa, Nape Ame- experience kile RAIA na vyama vya upinzani tunakipigia kelele.
Zipo nadharia za ku-justify sababu mbalimbali za kwanini Nape ametumbuliwa.
Ila ukweli utabaki kua serikali haikua na Muda wa kutafakari nadharia zote hizo ndipo imtumbue. Na hii serikali mara zote haina hulka hiyo ya kuumiza kichwa.
Ukweli Utabaki kua ;-Nape ametumbuliwa kwa kuenda kinyume na Katazo la Magu. Magu ambaye alipuuza malalamiko kuhusu kumwanyibisha Mteule wake RC Makonda. Na kwa hilo Nape alipoteza Utiifu kwa Mkuu wake. Kwa kuonekana anashadadia sana kuhusu tuhuma za Makonda. Hata Yesu alisema.. "Ufalme hausimami ukifitinika ndani yake." Ufitini wake kwa Mkuu ndio Umetumbua. Period.
Magu amewataka waandishi watumie kalamu zao vizuri, natumai hata yeye sasa hivi atakua amemtaka na Makonda achague video nzuri za kupeleka Clouds Media ili zichezwe na shilawadu.
My take; kama wakina Mwigulu wanaonekana kumkosoa askari aliemtishia Nape bastola bila kuangalia aliemtuma, Natumai watakua wana ufitini ufalme wa Magu, Mungu saidia natamani kesho asubuhi Magu awatumbue na wao pia.aweke mawaziri Wengine.
Unatuchosha na stori za mfalme juha.Na Donati Salla
Nimeona Zahama ya upofu wa fikra na ushabiki usiokuwa na tija ambao unachagizwa na kutiwa chumvi na wafuasi wa vyama vya upinzani na baadhi ya wanaCCM bila ya kutafakari na kuielewa shabaha ya chumvi hiyo nao pia wamekuwa wakifuata mkumbo na kushabikia mambo ambayo ama kwa hakika lengo lake ni kufifisha uhai wa CCM.
Nichukue fursa hii kuwambukusha wanaCCM wenzangu kuwa tunapaswa kurejea kwenye Misingi ya Umoja wa Chama chetu na kutimiza wajibu wetu wa kutoa uongozi kwa nchi yetu bila ya kuyumba au kuyumbishwa!!!
Ninayasema hayo kwa sababu zifuatazo;
1. Kwa wale wakristo mtakumbuka kuwa Yesu alipoingia Yerusalemu walimtandikia kanga na kumshangilia kwa shangwe kubwa huku wakisema Hosana!! Hosana!! Hosana!! Hosana Mwana wa Daudi!!!
Baada ya yesu kufika pale hekaluni alisema kwamba "Nyumba ya Baba yangu siyo Pango la Wanyang'anyi!!! na kisha aliwafukuza wale wafanya biashara kule hekaluni na alihojiwa kuhusu Mamlaka yake (Mathayo 21: 1 -27).
Sasa turudi kwenye uhalisia; Mhe. Magufuli alipoanza kazi ya Urais mnamo mwishoni mwa mwaka 2015 na mwanzoni mwa mwaka 2016 , Mzee Lowassa alisahaulika ghafla!!! Kila mtu alikuwa akimsifu kwa shangwe na kusema kuwa "Tumempata Rais" hakuna hata mmoja aliyekuwa akimponda!!! Tutakumbuka kuwa Mhe. Magufuli alianza kwa kutumbua 'majipu'!! Watu tukasema kuwa tumbua!! tumbua!! akaja kwenye watumishi hewa tukasema safi!! akaja kwenye vyeti tukasema safi!! akaja kwenye sukari tukasema safi!! akaja kwenye mageuzi ya CCM tukasema kuwa ni safi!! Alipokuja kwenye Madawa baadhi ya watu wameanza kutuimbisha nyimbo na kutaka kutuaminisha kuwa Mhe. Rais anakosea kitu ambacho sicho!!!
Ni busara tukakumbuka kuwa, Magufuli yule aliyeshangiliwa 2015 mwishoni na 2016 mwanzoni ndiye Magufuli huyuhuyu ambaye leo tunamlaumu!!! Kwa hiyo wakati tulipokuwa tukimshangilia Mhe. Magufuli tulikuwa kama wale wayahudi waliomlaki yesu wakati akienda yerusalemu!! Na sasa baadhi yetu tumegeuka na kuwa ni walewale wayahudi ambao sasa tunasema kuwa yesu asulubiwe na Baraba awe huru ilhali tunasahau kuwa tulimshangilia pale mwanzoni!!! Hivyo bhasi yafaa tuache ukigeugeu!!!
KUHUSU UHALALI WA VYETI NA ELIMU YA PAUL MAKONDA
2. Kwa sasa hasa vijana tumekumbwa na upofu wa "fikra" tumepumzisha uwezo wetu wa kufikiri na tumesahau wajibu wetu kwa taifa letu!! Ni jambo la kushangaza sana kuona Kijana Mzima mwenye elimu ya Digrii Moja au Masters unaamini kabisa kwamba Gwajima ndiye Baraza la Taifa la Mitihani!!! Unaamini kwamba Gwajima ndiye Mwenye Kadi ya Kliniki ya Paul Makonda!!! Inashangaza sana kuona Msomi wa aina hii ya kuamini hearsay!!
Embu turudi kwenye Misingi ya kawaida!!!
Ni utaratibu wa kawaida kabisa kwamba, unapokwenda kuomba kazi ni lazima uambatanishe nakala za vyeti ambazo zimegongwa muhuri wa Wakili ili kuthibitisha kwamba, nakala zile za vyeti ni nakala za vyeti halisi!!!! "Certified True Copy of the Original" sasa niwaulize watu !! Yale Matokeo ya Daudi Albert Bashite yanayobandikwa kule milangoni kwa Kanisa la Gwajima yamethibitishwa na nani??? Inawezekana na pengine ndivyo ilivyo kwamba matokeo yale ni feki!!! Swali jengine ni kwamba, kama Gwajima ana vyeti halisi vya matokeo ya Daudi Albert Bashite (Kwa sababu Miaka ya 2000 Matokeo yalikuwa hayajaanza kuwekwa kwenye Mtandao) Je, Gwajima anamiliki vipi vyeti ambavyo si vya kwake??? Kwa sababu kumiliki cheti ambacho si chako ni kosa kisheria!!! OK! with all that fallacy!! Unamwambia Mtu kwamba, atoke hadharani aonyeshe vyeti vyake!! Jamani tuko serious kweli??? Yaani hivi; nina cheti feki!! Halafu unaniambia kuwa nitoke hadharani nionyeshe vyeti!! Sasa nitaonyesha cheti gani wakati umeshanituhumu kuwa vyeti vyangu ni feki???
Siifahamu elimu ya Gwajima lakini embu turudi kwenye utaratibu! Nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa STK (Sheria, Taratibu na Kanuni). Mamlaka yenye uwezo wa kuthibitisha uhalali wa cheti cha mtu ni Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), na Seneti za Vyuo!!
Kwa kuwa kufoji cheti ni kosa la jinai!! na kwa kuwa kosa la jinai huripotiwa kwenye vyombo vya kisheria kama vile Polisi na Mahakama! Je, Gwajima aliwahi kwenda kwenye Kituo gani cha Polisi au kwenye Mahakama ipi na kuripoti kuhusu utata wa vyeti vya Makonda?? Na kama aliripoti mrejesho ulikuwa ni upi??? Je, ni lini Gwajima aliwahi kuiandikia Mamlaka ya Uteuzi wa Bw. Makonda kuhusiana na utata wa vyeti vya Makonda??? Na kama aliiandikia Mamlaka hiyo, Je, Mrejesho wake ulikuwa ni upi??? Gwajima anasimama Kanisani kwake na kusema kuwa Rais Magufuli ni Mtu Mzuri na ana hekima sana ila Makonda hafai na anamshauri kuwa Rais Magufuli amfute kazi Makonda tena hadharani!! Je, huo ndio utamaduni wetu wa kumshauri Rais katika hali ya chuki kwa sababu ulitajwa kwenye madawa ya kulevya??
Kumbuka kuwa Gwajima alikuwa mpinzani mkubwa wa Magufuli kuingia Ikulu!!! Leo anamsifu Magufuli!!! Embu shangaa hicho kioja!!!
Je, ni sahihi kwa Rais Magufuli kuamua mambo kutokana na chuki binafsi kati ya Makonda na Gwajima???
Makonda amewahi kuwa Mwenyekiti wa TAHLISO, amewahi kuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, amewahi kuwa Katibu wa Idara ya Chipukizi na Hamasa ya UVCCM, amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na leo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam!! Huko koooooooote Makonda hajawahi kuripotiwa kughushi vyeti!! leo hii baada ya kuwagusa vigogo wa Madawa ya Kulevya ndio tuhuma zinamwangukia???!!!
OK!! What is so special kwa Makonda kutoka Madarakani??? Na Makonda akitoka madarakani ndio furaha ya wauza madawa!! wewe utafaidi nini???
Kama Mtu hajafuata taratibu za kuripoti jambo, Je, ni sahihi kwa Rais kufanyia kazi maneno ya vijiweni na kwenye mitandao???
Ikumbukwe kwamba, uongozi si vyeti, ni kipaji!!! Yesu alikuwa na vyeti vingapi??? Mohammad alikuwa na vyeti vingapi?? Musa alikuwa na vyeti vingapi??? Sisemi kuwa elimu haina umuhimu lakini wakati mwingine ni kwamba tunahitaji utayari zaidi kuliko kustahili!!!
Ukitaka kufahamu kuwa nchi hii tunahitaji utayari zaidi kuliko kustahili, Mhe. Freeman Mbowe ni Form Six (Hata elimu yake haieleweki vizuri) na ni DJ (Disk Jockey) lakini yeye ndiye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini, ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ni Waziri Mkuu Kivuli!! Pale CHADEMA kuna Prof. Baregu, Makamu Mweyekiti wa huyu DJ ni Prof. Abdallah Safari!! Je, ni kwanii watu wa UKAWA hawalizungumzii hilo la elimu ya bosi wao na kutushinikiza sisi tuone kuwa Makonda hafai???
Ndio maana Rais wetu anasema kuwa hafanyiii kazi maneno ya Mitandaoni na yupo sahihi!!!
KUHUSU SAKATA LA NAPE NNAUYE
Mimi ninamuunga Mkono kwa dhati kabisa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Maamuzi aliyoyachukua ya kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri!!!
Ukiisoma vizuri taarifa ya Gerson Msigwa aliyoitoa tarehe 23 Machi 2017 hakuna mahali popote inapomzunguzia Mhe. Nape Moses Nnauye!!! Kwa lugha nyingine ni kwamba, Nape Nnauye ni Waziri wa Nchi ambaye hana Wizara Maalum kwa sababu Rais HAJATAMKA kwamba ametengua Uteuzi wa Nape Nnauye kama Waziri!!!! Someniiiii!!!! Uteuzi wa Waziri na Utenguzi lazima uchapishwe kwenye gazeti la serikali!! Je, ni wapi ambapo utenguzi wa Nape Nnauye umetenguliwa????
Baadhi ya watu tunasahau sana Historia lakini katika Nchi yetu tumeshawahi kuwa na Mawaziri wengi ambao hawakuwa na Wizara Mfano wa Waziri wa Mwisho Kabisa ni Mhe. Mzee wetu Prof. Mark Mwandosya!!! Alikuwa Waziri wa Kazi Maalum huyu kama mnakumbuka!!!
Tatizo la Nape Nnauye ni kukurupuka na kupaniki pamoja na kuropoka!!!!
Laiti kama ningelikuwa ni mimi nisingeongea na waandishi wa habari na ningenyamaza kimya mpaka ithibitishwe vinginevyo. Mhe. Magufuli hajakurupuka kwa sababu uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Mawaziri unafanyika chini ya Ibara ya 55 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na ni utaratibu wa kisheria kuwa uteuzi/Utenguzi wa nafasi ya Waziri/Naibu Waziri ni lazima utangazwe hadharani kwa umma!! Sasa utenguzi wa Nape haujatangwazwa kwa hiyo Nape ni Waziri na kutokana na matamshi yake ya tarehe 23/03/2017, hata kama Mzee Magufuli alitaka kumbakiza kwenye Baraza sidhani kama atafanya hivyo kwa sababu 'Nape amekosa adabu'!!!
Ukitaka kuona mahali ambapo Nape Nnauye amekurupuka, ni namna alivyounda tume ya kuchunguza sakata la 'kuvamiwa kwa clouds' Kwa mujibu wa tuhuma za Clouds ni kwamba 'walivamiwa'!!! Sasa twende taratibu!!
Kuvamiwa ni kosa la jinai na jinai hairipotiwi wizarani bali inaripotiwa polisi!! Wenye taaluma ya upelelezi siyo Maafisa wa Wizara ni Jeshi la Polisi!! Waliopaswa kwenda kuchunguza ni Jeshi la Polisi na siyo Wizara!! Afterall kitendo cha Paul Makonda 'kuikacha' Tume ya Nape Nnauye na hivyo kutoipa ushirikiano wa kitaarifa hakuhalilishi kauli ya kusema kuwa Makonda 'alivamia' na hakumfanyi Makonda kuonekana kuwa ana hatia!! Japokuwa mimi si mwandishi wa Habari lakini ninafahamu kwamba kama kuna tuhuma zozote za uvunjifu wa maadili ya taaluma/ tasnia ya habari bhasi shauri hilo lilipaswa kuripotiwa kwenye Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kabla ya kufika Wizarani kwa hiyo kitendo cha Nape kuunda Tume on the spot ilikuwa ni ukurupukaji kwa sababu Waziri ni Mamlaka ya Rufaa na ni Mamlaka ya Juu sana kiasi kwamba ni lazima mamlaka za chini ziwajibike kwanza ndipo mamlaka ya Waziri ifuate na ndio maana huko wizarani kuna bodi ya washauri wa waziri (Ministerial Advisory Board). Sasa Nape alishauriwa kuunda tume na hiyo Bodi Saa ngapi???
Aidha; kwa mujibu wa Maelezo ya Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Vipindi vya Clouds ni 'dhahania' yangu kwamba, siri ya 'uvamizi' wa Clouds anajua Ruge mwenyewe na Makonda!! Na wagombanao ndio wapatanao!! Kama Mkuu wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alikwenda na Maaskari pale Clouds huwezi kusema kuwa ni 'uvamizi' kwa sababu haijafahamika hasa lengo lililompeleka pale ni lipi, na kwa cheo chake ana mamlaka ya kufanya hivyo na hakuna aliyeripotiwa kupigwa, kuumizwa au kujeruhiwa na hakuna hata mmoja aliyejaza PF3. kwa hiyo hilo jambo ni tata na 'angeacha wafu wazike wafu wao'
Kutokana na maelezo yoote niliyoyatoa hapo juu, bado dhamira yangu inanishuhudia kwamba Rais Magufuli yupo sahihi kutokana hatua alizochukua, na ninampongeza kwa hilo!!
Utendaji Mzuri wa Nape kipindi akiwa Katibu wa CCM wa NEC Itikadi na Uenezi sio kigezo cha kumfanya Nape asichukuliwe hatua kutokana na ukurupukaji wake!! Hao wanaomwita Nape kuwa ni 'Shujaa' ndio wale wale waliosahau wema wooooote ambao Dr. Willbroad Slaa aliwafanyia kipindi alipokuwa Katibu Mkuu wa Chama chao na kumwona kuwa si lolote na si chochote!! Kwanini Dr. Slaa alipomkataa Lowassa hawakumuita Dr. Slaa shujaa licha ya kwamba walikuwa wamegawanyika 50/50?? Maana wengine walimkubali Lowassa na wengine walimkataa!!
Hao ambao walikuwa wakimtusi Nape kwa kila ya aina ya matusi kutokana na kile kilichokuwa maarufu kama 'bao la mkono' leo ndio wanamuita Nape kuwa ni shujaa!! Huo ni uzandiki wa hali ya juu!!
Hao wanaotuita sisi kuwa ni Makasuku wa CCM wanasahau kuwa waliimbishwa nyimbo za ufisadi wa Lowassa na baadae wakaja kula matapishi yao wenyewe!!!
HITIMISHO!!
1. Sisi kama WanaCCM tunausifu utendaji uliotukuka wa Nape Nnauye kipindi alipokuwa Katibu wetu wa Idara ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Itikadi na Uenezi japokuwa utendaji wake huo haudhoofishi utashi wa Dkt. John Pombe Magufuli na haubatilishi busara za Mwenyekiti wa Chama chetu.
2. Maamuzi ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ni sahihi, yamejaa hekima, busara, utulivu na umakini wa hali juu kiasi cha kupaswa kuungwa mkono na Watanzania wote pamoja na wanachama wote wa CCM na yeyote ambaye hamuungi mkono Mwenyekiti wetu Dkt. Magufuli kwa hatua anazozichukua ni dhahiri kwamba huyo si mwenzetu na hana nia njema dhidi ya CCM. Tukumbuke kwamba hakuna hata siku moja itakaa itokee kwa Upinzani kuiombea mema CCM nia yao ni sisi CCM tuharibikiwe, tuvurugane na tumalizane ili wao wachukue nchi kirahisi!! Hilo halikubali abadan! Hasilan!! Ukiona Mpinzania anakuponda ujue kuwa unapatia na ukiona anakusifu uje kuwa ndio unakosea!! WanaCCM tuzinduke!! Na tuwe macho!!!
3. Kanisa la Mch. Gwajima linapaswa kufungwa kwa sababu ni kanisa la kichochezi ambalo halitekelezi wajibu wake wa kutunza imani za kondoo wa mungu bali limekuwa ni mimbari ya mipasho, kukuza chuki, kustawisha uhasama, na kupika majungu ambayo yameleta taharuki miongoni mwa umma kwa kufanya jamii ya watanzania kujadili majungu na kusahau dira ya kuelekea kwenye nchi ya viwanda chini ya kauli mbiu yetu ya hapa kazi tu.
Ikumbukwe kwamba, mtumishi wa mungu aliyetumwa na mungu huwa anahubiri upendo, msamaha, kuchukuliana, kuombeana na kuwafaya watu waongoke na siyo kuwaelekezea mapepo na kufanya vitendo vingine mubashara kama hivyo vinavyofanywa na mchungaji huyo!! ni imai yetu kwamba, Msajili wa Vyama vya Kijamii/Makanisa atachukua hatua za haraka dhidi ya kanisa hili!!
4. Suala la kutekeleza haki, usawa na ukweli miongoni mwa walionaacho na wasio nacho sio jambo rahisi!!! ni jambo gumu linaloweza kugharimu maisha ya mtu!!! tukumbuke kwamba sisi sio wa kwanza kulalamika!! Hata wana wa Israeli walipokuwa jangwani wakati walipokuwa wakielekea nchi ya ahadi walimlalamikia Musa na Walimchukia Musa!!! Ilifikia mahali wakakumbuka masufuria ya nyama waliyokuwa wanayakomba kule Misri kipindi walipokuwa watumwa na walitamani kurudi Misri lakini Mungu aliwatia nguvu na kuwafikisha katika nchi ya ahadi!!! Hivyo bhasi!!! Na sisi tupo katika zama zinazofanana na zama zile za wana wa Israeli walipokuwa jangwani!!Badala ya sisi kumlalamikia Magufuli kama wana wa Israeli walivyokuwa wakimlalamikia Musa ni vyema tukamunga mkono Rais wetu!!! Vita ya Mafisadi, vita ya walitumbuliwa majibu, vita ya watumishi hewa, vita ya walanguzi wa sukari, vita ya wauza madawa ya kulevya, vita ya wanaokatwa 15% ya HESLB n.k ni vita vya kichinichini, ni vita vya kiuchumi, ni vita ambavyo havitumii bunduki lakini nguvu yake ni kubwa sana na lengo lake ni kumwangusha Rais Magufuli!!! Mzee Magufuli hafanyi anayoyafanya kwa ajili yake la hasha ni kwa ajili yetu!! Huyu Mzee anaitwa John!! Mtakatifu somo wake ni Mt. Yohane wa Msalaba na Mtakatifu Yohane Mbatizaji!!! "Tengenezeni Njia ya Bwana yanyoosheni Mapito yake" kwa hiyo hawa Mayohane kazi yao ni kutengeneza na ndicho anachokifanya Magufuli!!! Badala ya kumkatisha tamaa, tumuunge mkono!!! Tutafika tunakokutaka, tutayafuta machozi yetu na kusahau haya maumivu tunayoyapata kwa sasa!!! Kumbukeni hakuna tajiri anayempenda Maskini wala kumuona Maskini akipata haki isipokuwa Mungu Mwenye na Serikali zake alizotuwekea huku duniani!!!
5. Kwa usalama na uhai wa Paul C. Makonda ni lazima aendelee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar!! Kitendo cha Makonda kupigwa chini ndio kifo cha Makonda kitakuwa kimewadia ikiwa ni majibu ya chuki ya wauza madawa ya kulevya!!! Makonda kupigwa chini ni ishara ya ushindi wa wauza madawa ya kulevya!!! Makonda kupigwa chini ni ishara ya ushidi wa Gwajima!!! Hili la kupigwa chini kwa Makonda halikubaliki!!! Kama Hayati Amina Chifupa yalikumkuta yaliyomkuta kutokana na vita hii ya kupambana na madawa ya kulevya, halafu yamkute tena Makonda kama anavyoombewa yamkute, Je, ni nani kati yetu atakayekuwa tayari kuutosa uhai wake, familia yake na kazi yake kwa ajili ya kupambana na dawa za kulevya??? Kwangu mimi Makonda ni Shujaa!!! Ni Kiongozi Shupavu na Jasiri na anapaswa atetewe, aungwe mkono na asaidiwe!! Ili Taifa hili lifike pale tunapotaka lifike!!!
6. Tuache ushabiki wa kijinga, tuache uvivu wa kufikiri, turudi kwenye utaifa wetu na uzalendo wetu!! Taifa halijengwi kwa majungu na kujadili watu badala ya hoja!!! Taifa hujengwa kwa dira na hoja thabiti!! Tusiyumbishwe kama watoto wachangw kwa kupewa hoja na majungu ambayo hayatusaidii kwa lolote bali tusimame imara kila mmoja kwa nafasi yake katika kutekeleza wajibu wake!! Dira yetu kukuza kipato chetu na kuelekea kwenye nchi ya viwanda!!! Embu turudi huko!!! Tunavyomjadili Gwajima ndio tunazidi kumpa kick pamoja na 'cheap popularity' jambo la kufanya ni kushikamana na kurudi kwenye mstari.
Ninahitimisha hoja hii kwa kusema kwamba, Mwenye sikio na asikie!!! na wenye akili bila shaka mmenielewa!!
Paul C. Makonda chapa kaziiii!!
Magufuli endelea mbele WanaCCM tunaojielewa tupo nyuma yako!!!
Kidumu Chama cha Mapinduzi!!!
Alamsik!!
Unalitumikia tumbo lako huna lolote uliloliandika hapo.Njaa mbaya sana.Na Donati Salla

Kumbe wewe ni mume wa mkuu wa mkoa wetu???Mume
Ha ha ha, sio mahali pake mkuuWachaga mnampiga vita Magu sana. Mlizoea kuiba sasa kawabana kila kona.