Ziara za magufuli na maagizo makali havikuwa vitu vipya kwangu kwani ata Mjomba alikuwa hivyohivyo.
namuona Raisi wangu anafanya maamuzi. Bila kujari yuko sahihi kiasi gani kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosolewa na wachache kuliko kuogopa kufanya uamuzi. Ameanza kuikata kiu ya maamuzi magumu niliyoitamani kutoka kwa Lowassa.
Nashauri baada ya kuunda balaza la mawaziri Raisi wangu awapangie majukumu mazito mawaziri wake na awasisitize wawe wepesi kufanya maamuzi juu ya wizara zao na kuweka utaratibu utakaowezesha kujua na kusimamia hadi ngazi za chini kabisa ya idara zao.
Mfano waziri wa fedha aweze kuwajibishwa kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ubadhilifu kwenye halimashauri
Au waziri wa elimu aweze kuwajubishwa kwa utoro na uzembe unaofanywa na walimu shuleni
Au Waziri wa afya awajibishwe kwa miji kujaa taka kila kona .
Hii inamaana kubwa sana hawezekani raisi agundue uozo mkubwa kwenye idara chini ya wizara unayoongozwa na waziri fulani na kuchukua hatua alafu waziri abaki salama. Waziri anasimamia wizara moja tu wakati raisi anaangalia wizara zaidi ya kumi na tano.
Hivyo hivyo waziri akigundua uozo kwenye idara iliyo chini yake sana mfano waziri wa elimu agundue shule fulani walimu hawahudhurii shuleni kabisa anatakiwa amwajibishe mkurugenzi na afisa elimu kwa tukio hilo kwani haiwezekani waziri agundue uozo chini alafu mkurugenz abaki salama wakati waziri anaangalia Tanzania nzima na mkurugenzi anaangalia halimashauri moja tu.
Pia mkurugenzi adili na wakuu wa shule.
Hivyo basi Rais wa ngu ukikuta uozo dili na mawaziri tu mawaziri ndio watajipanga, Na waziri wa kwanza kumfukuza hiyo wizara yake uisimamie wewe kwa muda ili mawaziri waone mfano.