Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Issue ni mwanafunzi anachangia elimu? Acha kuongea vitu visivokuwa vya msingi
 
Maajabu ni yepi? Ungesema, serikali yatimiza ahadi yake ya kutoa elimu bure kwa gharama ya bilioni 23 Kila mwezi. Unaposema imefanya maajabu inakua kama vile imefanya jambo ambalo haliwezi fanyika duniani ila kwa miujiza tu. Sasa hapa kuna miujiza gani kama serikali inakusanya kodi na ikaamua kiasi fulani cha kodi kiende kwenye kutekeleza ilani ya chama ya kutoa elimu bure? Maajabu hapo ni yepi? Ingekua serikali imeamua kutokutoza kodi kabisa na haikopi halafu ikaweza kutoa elimu bure kweli hapo ingekua imefanya maajabu
 



Ukiwa nje ya tasnia ya Elimu waweza ona kama kuna jambo la maana katika hoja ya Elimu bure,lakini ukweli kinachoitwa "Elimu bure " chaweza kuwa ndiyo msumari wa mwisho kwenye jeneza la Elimu ya watoto wetu.

Kwa Shule za msingi serikali hutoa sh.1000 kwa mwezi kwa kila mtoto na kati ya hizo ni sh.500 tu ndiyo inayoingizwa kwenye account ya Shule,sh.500 nyingine zinatengwa kwa ajili ya Vitabu.

Kama serikali inatenga sh.500 kwa mwezi kama ruzuku ya kila mtoto wa Shule ya msingi,je sh.500 ndiyo inatosha kughalamia Elimu ya mtoto kwa mwezi?Hata katika ngazi ya familia zetu ni kweli sh.500 inatosha kughalamia Elimu ya mtoto?

Tuache usanii,kinachoitwa Elimu bure ni propaganda za kisiasa ambazo haziwezi kuwa muarobaini wa changamoto zinazoikabili Elimu ya watoto wetu,kuzorota kwa Elimu nchini kunachangiwa na hiki kinachoitwa elimu bure!

Kama sh.500 zinatosha kughalamia Elimu ya mtoto kwa mwezi,kwa nini watoto wao hawasomi kwenye Shule za umma?Kwa nini watoe mamilioni kusomesha watoto wao kwenye Shule za kimataifa wakati Elimu hiyo hiyo inaweza kupatikana kwa uwekezaji wa sh.500 kwa mwezi?

Kuwaelewa viongozi wetu unapaswa kuwa na uzezeta wa kiwango cha SGR,bila uzezeta wa kiwango hicho huwezi kuwaelewa na yumkini ukaishia kuwapinga na kujikuta upo mtaroni au kwenye sandarusi ukielea majini!
 
Reactions: ELX
Huu ndio Ukweli Mchungu viongozi wetu hawataki kuusikia. Kwenye majukwaa utakubali lugha taam na kuvutia, ila uhalisia haupo. Mitaala mipya ila hamna vitabu husika, Case study Ukosefu Vitabu darasa LA nne wanaojiandaa kufanya mtihani wa taifa mwaka huu, Anayebisha aniprove uwepo wa vitabu hivyo. Tunaua Elimu yetu kwa kutosema ukweli
 
Wadau
Serikali ya JPM haitanii linapokuwa suala la kuboresha huduma za jamii nchini.
Serikali hiyo sikivu imetenga fedha za kutosha kujenga Jumla ya Hospitaki zenye hadhi ya Wilaya 67 nchi nzima.
Viva JPM
Viva CCM
 
Hapo sasa.
Yaani atakaekula za baba kama kala sumu
Shauri zenu
Yaani hapo kuna watu wanashangilia na kuanza kukaa mkao wa kula
 
UONGO ULIOKITHIRI!!!! Hospitali hazina vifaa muhimu mbali mbali vya kutendea kazi zao madawa hakuna ya kutosha, mishahara ya madaktari na manesi ni ya chini mno katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki, Madaktari na Manesi wahitimu toka vyuoni chungu nzima wanakosa ajira halafu unatuletea huu upuuzi humu ili kumpamba huyo muongo na dhalimu!!!!

Wadau
Serikali ya JPM haitanii linapokuwa suala la kuboresha huduma za jamii nchini.
Serikali hiyo sikivu imetenga fedha za kutosha kujenga Jumla ya Hospitaki zenye hadhi ya Wilaya 67 nchi nzima.
Viva JPM
Viva CCM
 
Hivi walikuwa wapi miaka 60 wakiwa wao ndo kwenye uongozi. Vip kuhusu zahanati na vituo vya afya maana haiwezekani ata yule anayeumwa kichwa aende hospitali.

Ila CCM bana yaani kama pepo mchafu yaani BELTHEBULI(yule wa biblia)
 
Usiseme unatuletea sema unaniletea kwani Mkuu upo na nani hapo?
 
Wadau
Serikali ya JPM haitanii linapokuwa suala la kuboresha huduma za jamii nchini.
Serikali hiyo sikivu imetenga fedha za kutosha kujenga Jumla ya Hospitaki zenye hadhi ya Wilaya 67 nchi nzima.
Viva JPM
Viva CCM
Mna bajeti mahela meeengi ambayo hata hamjui pa kuzipata. Huo ni utaahira wa Hali ya juu.
Naibu waziri wa afya kasema serikali Haina hela ya kununua MRI scan Na CT scan sasa nakushangaa mpiga zumari maneno mengi ya uwongo umeyapata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…