Maajabu ni yepi? Ungesema, serikali yatimiza ahadi yake ya kutoa elimu bure kwa gharama ya bilioni 23 Kila mwezi. Unaposema imefanya maajabu inakua kama vile imefanya jambo ambalo haliwezi fanyika duniani ila kwa miujiza tu. Sasa hapa kuna miujiza gani kama serikali inakusanya kodi na ikaamua kiasi fulani cha kodi kiende kwenye kutekeleza ilani ya chama ya kutoa elimu bure? Maajabu hapo ni yepi? Ingekua serikali imeamua kutokutoza kodi kabisa na haikopi halafu ikaweza kutoa elimu bure kweli hapo ingekua imefanya maajabu
Ukiwa nje ya tasnia ya Elimu waweza ona kama kuna jambo la maana katika hoja ya Elimu bure,lakini ukweli kinachoitwa "Elimu bure " chaweza kuwa ndiyo msumari wa mwisho kwenye jeneza la Elimu ya watoto wetu.
Kwa Shule za msingi serikali hutoa sh.1000 kwa mwezi kwa kila mtoto na kati ya hizo ni sh.500 tu ndiyo inayoingizwa kwenye account ya Shule,sh.500 nyingine zinatengwa kwa ajili ya Vitabu.
Kama serikali inatenga sh.500 kwa mwezi kama ruzuku ya kila mtoto wa Shule ya msingi,je sh.500 ndiyo inatosha kughalamia Elimu ya mtoto kwa mwezi?Hata katika ngazi ya familia zetu ni kweli sh.500 inatosha kughalamia Elimu ya mtoto?
Tuache usanii,kinachoitwa Elimu bure ni propaganda za kisiasa ambazo haziwezi kuwa muarobaini wa changamoto zinazoikabili Elimu ya watoto wetu,kuzorota kwa Elimu nchini kunachangiwa na hiki kinachoitwa elimu bure!
Kama sh.500 zinatosha kughalamia Elimu ya mtoto kwa mwezi,kwa nini watoto wao hawasomi kwenye Shule za umma?Kwa nini watoe mamilioni kusomesha watoto wao kwenye Shule za kimataifa wakati Elimu hiyo hiyo inaweza kupatikana kwa uwekezaji wa sh.500 kwa mwezi?
Kuwaelewa viongozi wetu unapaswa kuwa na uzezeta wa kiwango cha SGR,bila uzezeta wa kiwango hicho huwezi kuwaelewa na yumkini ukaishia kuwapinga na kujikuta upo mtaroni au kwenye sandarusi ukielea majini!