Wenye akili tulijua ngoma ya watoto huwa mwisho saa 12 jioni, leo hatuoni tena safari za kushitukiza kama zamani, hatusikii tena 'nitumbue nisitumbueeee', kilichobaki ni kuzindua madaraja, huku wasaidizi wake wakiishia kuhudhuria matamasha ya wakata viuno. Hatusikii viwanda vikifunguliwa tena, zile mbwembwe za kwenda bandarini kuokota vichwa vya treni zimepungua kama sio kwisha kabisa.
Watu wanapiga dili kama kawaida, serikali inapinga dili 1.5, safari za nje wanakwenda kama kawa, TRA walianza kutangaza mapato kila mwezi baada ya kuona yanashuka wakaacha eti ni siri, Flow meter ya bandarini inaendelea kuhujumiwa kama kawaida, kiki ya dreamliner imefubaa siku hizi hatuonyeshwi kina polepole wakipanda kama mwanzo, uhakiki wa wafanyakazi hewa hauishi kila mwaka wanarudia.
Pamoja na mbwembwe zote hizo sioni tofauti kubwa kati yake na mtangulizi wake.
Ndio maana kuna watu wanahoji Kikwete aliwezaje kuwapa mkopo wanafunzi wote wakiwepo wanafunzi hewa, aliweza vipi kuongeza mishahara na kupandisha madaraja wafanyakazi kila mwaka bila kuhakiki wafanyakazi hewa.
Kuongoza nchi siyo kazi ndogo hasa ukiwa huziamini taasisi na watendaji uliowakuta. Mbwembwe hazisaidii.
Leo siandiki mengi nawahi appointment ya kuunga juhudi kabla deadline haijafika.