Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Duh
 
Tutamtetea mahali panapostahili kutetewa, na tutampinga mahali panapostahili kupingwa

Ila kwa rais huyu anamengi sana ya kupingwa kuliko yale machache ya kutetewa

Kwa kifupi huyu rais hafai kuwa kiongozi wa kitaifa, sioni hata nafasi moja inayomfaa kwa sifa zake alizo nazo zisizojali misingi ya utu na uvumilivu kwa wale wanaompinga

Huyu hafai hata kuwa mwenyekiti wa familia
 
Po Poor and Poverty mentality..unajiita mnyonge..!! Lofa kabisa wewee.
 
Watanzania wengi hivi sasa wanatembea wameinama utadhani ni watu wa maombi sana kumbe wamejawa shida, njaa na kukosa matumaini!
 
Patriotism means to stand by the country. It does not mean to stand by the president or any other public official, save exactly to the degree in which he himself stands by the country. It is patriotic to support him insofar as he efficiently serves the country. It is unpatriotic not to oppose him to the exact extent that by inefficiency or otherwise he fails in his duty to stand by the country. In either event, it is unpatriotic not to tell the truth, whether about the president or anyone else.
Theodore Roosevelt
 
"nataka kuwahakikishia tukikosea tumepotea maana Uwenda ikachukua muda mpata Rais wa aina hii kiasi wenye hekima wanatafuta jinsi yakuhakikisha vision yake anaimalizia.
Ndugu zangu wapo watu wanataka ile nafasi kwa matumbo yao ila huyu Rais hapana."

Mhh!!!! uenda ametumwa na Mungu ni neema kwetu watu wa dini mtueleze
 

Tatizo ni mkabila.OVER
 
Tunataka vision ya taifa na sio mtu mmoja mkuu. Huyo ni binadamu kama walivyo binadamu wengine
 
Tusimame naye Kwa kuweka traffic light Chato, tusimame naye Kwa kujenga uwanja wa ndege chato bila hata Bunge kupitisha matumizi hayo, tusimame naye Kwa kujenga bandari chato bila ya hata Bunge kupitisha matumizi hayo, tusimame naye Kwa kujenga hospitali ya rufaa chato bila hata ya Bunge kupitisha matumizi hayo, Tusimame naye Kwa kufanya ununuzi WA ndege bila hata ya Bunge kupitisha matumizi hayo.
Tusimame naye kwenye huu utekaji wananchi unaotokea kwenye hiki kipindi chake Tu.
Acha longolongo shikamana naye wewe mwenyewe na familia yako
 
Nchi haaiwezekani kuendelea kamwe kama ina raia vichaa kama wewe kazi kusifia wenzao
 
Kwa mtizamo wako unaona mambo yako sawa.Ila sisi tunaona baada ya hiyo miaka saba iliyobaki nadhani wengi wetu tutakuwa tumekufa kwa njaa na maradhi.Wanaomsifia wengi kama sio wanafiki wanakuwa ni watu wa kanda yake.Awamu hii imekuwa na upendeleo wa wazi kabisa bila kificho.Watu wa Kimara hadi Mbezi wamevunjiwa nyumba zao bila fidia na Watu wa Mwanza raisi kazuia wasivunjiwe eti ndio waliompa kura.
 
duh... mkuu unafahamu kuwa kwa mara ya kwanza ile taswira ya kisiwa cha amani imepotea..
 
Ina maana mnajua kabisa hakubariki ama?? Au siye watanzania tunapenda marais wa hovyo mpaka tumkatae yeye kama ni rais wa karne???
 
Miradi hiyo inajengwa kwa mikopo na sisi na vizazi vyetu tutalipa hiyo mikopo.Unapohamasisha watu wajenge viwanda wakati una kiwanda kikubwa cha URAFIKI kinaoza bila uzalishaji hapo tunahitaji maelezo.Au unajenga SGR unaagiza reli na mataruma kutoka China na Turkey na kiwanda cha Mangula kinaendelea kuoza.Au chuma kipo Mchuchuma na Liganga?Umesimamisha safari za nje ila misafara ya ndanI ni mikubwa na gharama kubwa huenda hata hiyo ya nje ambayo haikuwa na watu wengi.
 
kumekuwa na maneno maneno mitaani kuwa mbona mh rais hasemi kitu kuhusiana na suala la kutekwa kwa Mo Dewji. mnataka aseme nini? yeye si mnafiki.anajua anachokifanya. mwacheni msimsumbue. kuna watu wengine ni wanafiki wanaweza kukukanyaga kwa makusudi halafu wakakupa pole au kusikitika. hiyo ndo tabia wanayopenda watanzania. mh rais hayupo hivyo. akisema amesema.

kuna kauli nyingi ambazo mh rais aliwahi zitamka na zikawa kweli kwa sababu yeye husema ukweli.wewe usipopenda ni juu yako ila amekupa ukweli. sasa watanzania mnakuwa wanafiki mpaka unafiki unakuwa ninyi.mnataka mh rais aseme ana huzuni? anasikitishwa,ana majonzi?ana omboleza? mnataka tamko gani na la nini? kwa nini mnataka kumfundisha mh uongo na unafiki?

sisi na yeye tutapiga kazi tu.na wale walio tayari kufanya nasi kazi tutafanya nao wasio tayari tusilaumiane sisi tutakapokuwa busy hatutaki maneno maneno.yeye atawapumzisha walio na mizigo nawalio tayari kumwendea.wengine mizigo yao itawalemea na mwishowe watakuja huku kulia lia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…