Leo tumeshuhudia uzinduzi wa Barabara ya juu yaani Flying over Tazara huu Ni muendelezo wa miradi mingi inayotekelezwa na uongozi wa serikali YETU ya awamu ya tano chini ya Rais Dk J.P.Magufuli.Tanzania kwa miaka mingi tumekuwa tukipiga kelele juu ya uwepo wa utashi wa kisiasa Katika serikali YETU.Tulifika mbali na kuomba Bora hata tutawaliwe na dikteta ili atusaidie kupata maendeleo huku tukisahau Historia juu ya udikteta wenyewe.Tanzania inasonga mbele kimaendeleo,nitaeleza
Serikali ya awamu ya tano imejinasibu kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.Tumeshuhudia viwanda vikijengwa kwa kasi ya mwendo kasi.Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia uzinduzi wa wa kukamilika kwa mradi mkubwa wa umeme kwa kutumia gesi ujulikanao Kama Kinyerezi two 240CCPP,Upanuzi wa mradi wa umeme wa Kinyerezi one yaani Kinyerezi one extension project,Ujenzi wa SGR,Ujenzi wa reli ya umeme haya yote Ni maendeleo kuelekea Tanzania yenye uchumi wa Kati.
Je wapinzani wa maendeleo haya Serikali yetu kwa Nini tusiungane na Mh Rais Katika juhudi za kuliletea Taifa letu maendeleo?