Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wabunge wa kusini wanashangaza sana. Hawawaongelei bungeni wakulima wao wanaodhulumiwa kupitia mifumo ya kishenzi ya kangomba na wala maua, wao wanakwenda kuongelea mgao wa mfuko wa korosho, mfuko ambao ni wa wapigaji wachache.

Hii nchi kila mtu ilifika hatua akageuka dalali wa tajiri fulani. Siku zote dhuluma huwa na mwisho, jasho la mtu haliwezi likapotea milele lazima atatokea mtu wa kulitetea.
 
Ulikuwa kipofu na kiziwi umepona leo nn
 
Ngoja waje wale wa buku 7
 
Kwa sababu wanafahamu, hao wa Kakomba waliibuka baada ya serikali kushindwa kutengeneza mifumo imara itakayohakikisha bei bora ya korosho!

Ilifikia wakati hadi watu wanaenda kuokota korosho kwa kutegemea kuzikaanga wenyewe na kuziuza barabarani! Na hata pale the so called Vyama vya Ushirika walipotangaza kununua korosho; waliishia kuzichukua tu toka kwa wakulima bila kuwalipa hata senti na kwenda kuzifungia kwenye maghala!

Wapo ndipo wakaaibuka watu wa Kakomba na bei za dhuluma lakini more often than not, in terms of CASH! Ingekuwa wewe ungekutaa wakati hata pesa ya kununua sare za shule kwa wanao hauna?!

Therefore, hao Kakomba ni matokeo ya mifumo mibovu!

Tuje hivi sasa. Mara Wanajeshi hivi, mara Wanajeshi vilee! Mara JKT watabangua hata kwa meno mara hivi, maar vile... ukiuliza hadi leo hata 25% ya korosho hazijanunuliwa!

Wakati zaidi ya 75% ya wenye korosho wana korosho zao ndani, njaa na emergencies hazisubiri hayo mambo yenu!

Bahati mzuri, nimekufahamu Bukilo hapa JF muda mrefu sana na leo sio mara ya kwanza kukutana kwenye mada!

Mtu aliyekuwa anakula mikate ya Ikulu tangu enzi za Mwalimu katu hawezi kuijua njaa!

But all in all, itakuwa unawaonea hao Wabunge wa Kusini! Suala la Kangomba limeanza kupigiwa kelele miaka nenda rudi na hao hao Wabunge wa Kusini na ndio maana, hata wewe ambae haielekei kwamba ni mtu wa Kusini, leo hii unaifahamu Kangomba!

Tuje hilo la Mfuko wa Korosho! Tell me baada ya serikali "kupora" yale mabilioni ya Mfuko wa Korosho hatimae wameyarudisha kutekeleza kazi yake huku yakiwa kwenye mikono salama!

Wakulima wengi ukiongea nao wanalalamika msimu huu kukosekana kwa madawa stahiki kwa viwango na ubora stahiki hata kama mnataka kusingizia kupungua kwa mavuno kumetokana na mabadiliko ya hali ya leo!

To save your energy, hata kama ulitaka kuleta hoja ya mabadiliko ya hali ya hewa, moja ya kazi za madawa ya korosho ni kukabiliana na hali ya hewa! Kwa mfano, sulfur ina-absorb moisture ambao ni hata kwa ukuaji wa tunda la korosho kwa sababu unafunika maua!
 
Kiukweli kikwete katika hili ali fail sana. Yeye alijichukulia alivyoweza na kuwaachia wengine nao wachukue walivyoweza.hii nchi ingefikia hatua ingekuwa imenunuliwa. Jamaa alipaswa kutumiwa zile sheria za china.basi tu katiba inamlinda.
 
Aliempiga Risasi Lissu ni nani? Hivi tafsiri ya Mafisadi kubanwa ni Maisha kuwa magumu zaidi kwa Wananchi au maisha kuwa mazuri kwa Wananchi? Mimi bado sijaona kama huo ubanwaji wa Mafisadi umereflect katika maisha ya Mwananchi wa kawaida hila ndio kwanza maisha yamezidi kuwa magumu.Na wewe unaonekana ni beneficiary wa Serikali hii,Hila kiukweli Katiba inapaswa irekebishwe ili Serikali iwe moja kusiwe na hii dhana ya awamu hii na ile,Serikali ni moja tu tuweke misingi kikatiba.
 
mkuu kwaio waliomchapa Lissu risasi ni kina nani tena?
 
Tutamfanyaje huyo Kikwete? So kuna mahakama ya mafisadi? Tumeshindwa nini?
Mahakama hiyi sio kwa viongozi au watawala wastaafu.Changa la macho,bado kuna watu wanasifia as if walikuwa malaika,wakati wao ndio vinara wa majanga yote ya kifisadi.
 
Mahakama hiyi sio kwa viongozi au watawala wastaafu.Changa la macho,bado kuna watu wanasifia as if walikuwa malaika,wakati wao ndio vinara wa majanga yote ya kifisadi.
Umenena mkuu hii ni ya watawaliwa . kashifa zote zilizopita hakuna kiongozi hata moja? na Magufuli yupo na wimbo wa mafisadi kila siku?
 
Nasikia huko Jamhuri ya watu wa kusadikika wamekagua benki kuu yao wakaona hakuna pesa za kigeni. Yani reserve ya pesa za kigeni ni ndogo sana kiasi kwamba haitoshi kufanya purchase nje kwa miezi kadhaa ijayo. Kwahiyo wameamua kwenda kuzitafuta kwenye maduka ya kubadili fedha. Wanaamini zimefichwa huko. Kwamba wenye maduka wamezibana na hawataki kuziachia. Kwahiyo wameamua kwenda kuzisaka kwa mitutu ya bunduki. Songombingo za Kaboka mchizi.!

Ngoja niwape shule kidogo. Sababu za msingi za kupotea kwa 'dola' katika nchi hiyo ni hizi hapa.

#Mosi; nchi huwa inapata pesa za kigeni kwa kuuza bidhaa na huduma nje. Lakini nchi ya kusadikika imezuia kuuza mazao nje. Nasikia huko mahindi yanaozea ndani, mbaazi ndo kwisha habari yake, tangawizi hata ukitupa watu hawaokoti. Hivyo vyote vilikuwa vina soko kubwa nje ya nchi na vinaingizia nchi hiyo pesa nyingi za kigeni. Lakini mfalme wao akapiga marufuku wasiuze nje. Leo wanamtafuta mchawi. Maajabu.!

Koro-show nasikia nayo imezuiwa kuuzwa nje. Serikali ktk nchi ya kusadikika imesema itanunua yote. That means hakuna pesa zozote za kigeni nchi hiyo itaingiza. Kama makampuni binafsi kutoka nje yangeruhusiwa kununua yangekuja na 'dola'. Wangechange na kupata madafu ya kulipa wakulima. Hayo 'madola' yaliyochenchiwa yangeingia kwenye mabenki na hatimaye benki kuu. Kwahiyo serikali ingeongeza reserve yake ya pesa za kigeni. Lakini wameamua kununua koro-show zote wenyewe, leo wanatafuta dola kwa mitutu?

Na mfalme wao amesema akikosa soko atamwambia kila mtu kwenye nchi hiyo ale ratili mbili za koro-show. Hizo ratili mbili kwa kila raia zinanunuliwa kwa pesa ya madafu na zitaliwa na raia wa humohumo ndani. Kwahiyo koro-show zote zinaweza zikaisha bila kuingiza hata dola moja kwenye nchi hiyo. Hii ni biashara kichaa ktk historia ya biashara duniani.!

#Pili; nchi inapata pesa za kigeni kupitia mikopo na misaada mbalimbali ya kimataifa kama vile kutoka Benki ya dunia, IMF, na mataifa wahisani kama Marekani, Umoja wa Ulaya etc. Sasa nasikia Benki ya dunia imesitisha mikopo na misaada kwenye nchi hiyo. Baadhi ya mashirika ya kimataifa nayo yamesitisha shughuli zake huko. Umoja wa Ulaya nao unafikiria kusitisha misaada yote kwa nchi hiyo, na tayari balozi wao ameshafurushwa. Kwahiyo hakuna 'foreign grant wala loan' ambayo inaingiza pesa za kigeni kwenye nchi hiyo kwa sasa. Lakini wanaenda kutafuta pesa za kigeni kwa AK47 kwenye maduka ya kubadili fedha. Hekaya za Abunuasi.!

#Tatu; Nchi inapata pesa za kigeni kwa kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa wingi (Foreign investors). Mwekezaji akienda kujenga kiwanda katika nchi fulani haendi na pesa za madafu, anaenda na dola. Akifika huko hizo dola anazibadili na kupewa madafu. Dola zinaingia kwenye system na kuongeza reserve ya pesa za kigeni.

Lakini kwenye nchi ya kusadikika foreign investors wanafokewa na kunyang'anywa passport. Kiongozi akishashiba 'ugali tembele' anaropoka tu 'mnyang'anyeni passport'. Matokeo yake wawekezaji wanahamisha mitaji na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Leo nchi ya kusadikika iko busy kutafuta nani kaficha pesa za kigeni kwenye sandarusi. Harakati za pimbi.!

#Nne; nchi inaingiza pesa za kigeni kutokana na jinsi inavyouza utaalamu wake nje ya nchi. Lakini kwenye nchi ya kusadikika wataalamu wamezuiwa kwenda kufanya kazi nje. Serikali yao imesema mtu yeyote anayepata kazi nje ya nchi inabidi aombe kibali kwanza akiambatanisha mkataba wa ajira. Na serikali inaweza kumruhusu au kumkatalia. Leo serikali hiyohiyo ipo 'busy' kutafuta dola kwenye maduka ya wahindi. Futuhi.!

#Tano; Njia nyingine ya kumaintain pesa za kigeni ni kuregulate kiwango cha kununua na kuuza bidhaa na huduma nje ya nchi. Unatakiwa kuuza zaidi kuliko unavyonunua. Hakikisha unanunua nje vitu vya muhimu tu. Vingine vitengeneze mwenyewe. Hii ni kwa sababu kila unapoagiza bidhaa yoyote nje ya nchi unapunguza reserve yako ya pesa za kigeni. Lakini kanchi ka kusadikika kanatumia reserve yake ya pesa za kigeni kununulia hadi toilet paper, halafu leo kanatafuta pesa zilikofichwa. Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un.!

Malisa GJ
 

Upupu mtupu walahi
 
Ana block mashimo yote ya kupiga hela.anazingatia kanuni vizuri.anatumia jeshi vizuri kudhibiti upigaji.popote pale ambapo Kuna udanganyifu Magufuli anapatia hofu.msukumo mkubwa haupo kwa wananchi wazuri wachapakazi was taifa Bali upo kwa viongozi wa taasisi ikiwemo mawaziri.kila sehemu hakika panafuka Moto au sio.ole wako uibe ukikatwa msala wake kwanza utakaa rumande na baadaye ukajionee jela.tahadhari hii natoa mpaka kwa Wana jf ambao mnavunja sheria.jeshi la magereza wame wameli reform ukifungwa unalima.kwa hiyo Ni kiwewe kwa wapiga deal.tupo na nyakati muhimu Sana kwenye hii Vita ya kiuchumi .Ni TANZANIA pekee ndio Imeweza kuonyesha misimamo yake wa jumuiya za kimataifa na wawekezaji na imetuma ujumbe wake kwamba haitaki michezo ya kiujanja ujanja Wala deal chafu.tuiache serikali I run Mambo.wito wangu kwa Rais nakupongeza sana.umeonyesha inayopaswa kufutwa na kiongozi yoyote wa dunia.JamaniJPM anatosha atatupa utajiri.magufuli mwendo wa kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…