Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Wewe ni kilaza kweli
 
Miaka mitatu hatujmuona akisafiri popote zaidi ya kubaki katika nchi yake,akiwa pamoja na watu wake.karibu miaka kadhaa iliyopita huko nyuma alisimamia mambo fulani makubwa ndani ya nchi.mwanzoni watu walishangazwa na ujasiri aliokuwa nao lakini baadae wakakasirishwa na bidii yake na dhamira yake wakajaribu kumrudhisha nyuma.sasa anajaribu Tena kuwasaidia watu wake Kama zamani safari hii akiwa mkuu.

Anaendelea kufanya mambo ya ajabu ambayo kwa kweli watu wengi wanashangaa,hata wanaulizana:"mtu huyu alipata wapi hekima hii na matendo haya yenye nguvu?wanasema:"je,huyu si mshirika mwenzao chamani?Basi alipataje kujua mambo mengi haya yote?"

Watu wanafikiri kwamba jp Ni mtu wa business as usual.wanawaza hivi,"tulimwona toka mwanzo akiwa na wale,Basi anawezaje kuwageuka?kwa hiyo licha ya uthibitisho wote-kutia ndani mafanikio yote na mabadiliko -wanamkataa.kwa kuwa tu wanamfahamu ,hata watu wake chamani wanakwazika kwa sababu yake, na hivyo Mimi ndege JOHN nasema:"nabii anaheshimiwa kila mahali isipokuwa katika eneo lake la nyumbani na hata katika nyumba yake mwenyewe".

Kwa kweli,hata yeye anashangazwa na uoga wa kusema ukweli walio nao watu wake .kwa hiyo , anaendelea kufanya miujiza kimya kimya ili wasiendelee kupiga kelele kwa sauti wakisema"waonee huruma waizi wa madini,waonee huruma wanaotapeli wakulima ,waonee huruma watakatishaji fedha".

swali: Kwanini watu wamekuwa waoga kusema ukweli na hawajui kutofautisha kiongozi mzuri na mtawala muovu?
 
Kwanini kila anachogusa kinamwendea mrama? Kuanzia kuuza nyumba za serikali, kununua kivuko kibovu, kukurupuka kukamata samaki, kukurupuka kuvunja mikataba, kukurupuka kununua ndege zinazoendelea kuongeza hasara kwa mabilioni, sukari, korosho, na sasa dollars?

Hebu tupe hayo unayodai ni ya kinabii tupate kuelimika.
 

Kwao wapi???
 
Hiyo Title Na Ulichoandika Ndani Haviendani Kabisa. Unasema Nabii Hakubaliki Kwao, Contents Za Andiko Lako Hazina Uhusiano Na Kichwa Cha Habari.

Kwanza Nikuulize, Unajua Maana Ya Nabii, Na Hayo Maneno Umenukuu Wapi Na Yanamlenga Nabii Gani Katika Kipindi Hichi???

Isitoshe Kajifunze Kuandika.
 
Bila shaka watamuuliza Nabii," Ikiwa ewe ni nabii wa Mungu wakate mishahara wateule wako na watunga sheria na majemadari wako wakuu ili ukawaongezee wale wazalendo wa kweli kule chini wanaolipwa mshahara sawa na posho ya siku moja ya wateule wako."

Bila shaka kwa sasa watu wa nyumbani kwake Nabii ni marafiki zake na wateule wake ambao wanamkubali kwa kila Jambo mana wanakula mema ya nchi kwa mishahara minono isiyo na hasara zaidi ya faida wakati wafanyabishara wanasota mchana kutwa ili kupata hako kafaida ka sh. 100,000 kwa siku kwa kukimbizwa na kujificha wasije wakakutana na akina Zakayo.
 
sio madili yetu kumsema sema babaπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mambo Shaghalabaghala. Lakini unapata tabu ipi mbona wananchi wengi wanamkubali hadi wabunge na madiwani wa vyama upinzani wanakubali kuachia uongozi wao kwa kuvutiwa na utendaji wa Sirikali ya awamu ya 5. Hao wachache si tuachane nao tu Mkuu kwa sababu wengi wanaunga mkono? Au ni kinyume Mkuu?
 
Ni kwanini, kila anachofanya kinakwama? Kuna toba inatakiwa nchi hii ili tusonge mbele, vinginevyo tutabaki hapa hapa na kurudi nyuma. Tutaumia vijana, wazee hawa wanaotusababishia laana hii kwa nchi yetu baada ya miaka 50 ijayo hawatakuwepo, ila vijana wa leo ndotutakuwa na wakati mgumu.
 
"this man anapractice scientific politics wala Hana propaganda hata kidogooo...
#ipo siku MTAMMISS"...

Mmh!!! Scientific politics ni ipi? Mkuu.
 
Kwenye keyboard yako unatumia lugha gani?

Kikweli sijakuelewa hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…