Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania


Ukiwanacho haukithamini, kikiondoka ndo unalia kwa kukikumbuka. Atakumbukwa sana tu, kama wengine walivyokumbukwa
 
Maji je pamoja na kunyesha mvua mara zote lakini maji bado adimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mag3 we ni mchambuzi mzuri na bora sana. Wengi tunajifunza mengi toka kwako. Mabishano na ushabiki huu wa ccm na cdm unajidhalilisha kujiingiza humo
Umesema kweli ila naomba nikusahihishe kidogo...mimi Mag3, sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha kisiasa hapa nchini. Kama mwananchi huru naamini kwamba adui mkubwa wa taifa hili ni CCM toka ilipoasisiwa mwaka 1977 na pamoja na kwamba kilikuwa ni chama pekee cha kisiasa, niligoma kujiunga nacho kama nilivyogoma kujiunga na mzazi wake TANU.

Upepo wa Mageuzi ulipoikumba Tanzania nilifurahi sana. Ingawa mwanzoni niliunga mkono harakati za NCCR Mageuzi, sikujiunga nao kwani niligundua mapema njama na ujanja wa chama tawala kuukubali mfumo mpya shingo upande. Toka wakati huo nilikosa kabisa imani na CCM baada ya kugundua ni chama cha kigaidi na hivyo naamini adui mkubwa wa taifa hili ni CCM.

Ni kwa sababu hiyo watu wananihusisha na Chadema chama ambacho sijawahi hata kukanyaga ofisi yao wala hata kukutana na viongozi wake. Adui wa adui wako ni rafiki na uhusiano wangu na Chadema unaanzia na kuishia hapo. Kuikataa CCM kunahitaji ujasiri na bahati mbaya hapa Tanzania wajasiri wanahesabika kwani wengi wa wananchi wamechagua unafiki kama nguzo kuu ya maisha yao.

Tanzania yawezekana bila CCM.
 
Unapenda hadi unageuka kuwa kipofu?! Unaweza kunitajia project MOJA TU aliyofanay JPM kwa issue ya umeme zaidi ya kuendeleza project ya JK ya kutumia gas ambayo JPM amekuta imeshachimbwa na hata bomba limeshajengwa huku plant ya kwanza ikiwa imeshakamilika pale Kinyerezi!

Btw, huo mgao ulioisha ni upi?! Wanatukatia umeme kimya kimya bila kusema ukweli halafu unasema mgao umeisha?! Kwa upande wangu kwa mfano, juzi hatukuwa na umeme usiku! Na usiku wa leo, angalia wewe mweneyewe hapa chini:-
Unaona hapo juu, betri ndo inakata hiyo na umeme hamna halafu hapa nipo job (work at home), na kwa maana nyingine in no time, nitalazimika kufungasha virago wakati nina almost 5 hours yamebaki!
 
Unazungumzia mahali gani huko ambako hamna mgao wa umeme? Maana huku nilipo mgao kama kawaida hadi imeshakuwa kero. Ila wewe ni mjinga, haiwezekani utoe misifa kibao pasipo kujiridhisha na unachokisifia.
 
Wapi huko aliko maliza hilo tatizo la kukatika katka kwa umeme?.wilaya ya kinondoni juzi tuu umeme ulikatika kuanzia asubuhi hadi saa moja kasoro,na hiyo inatokea mara kwa mara
 
Du ndio unetumwa ?
Angala nafahamu maeneo ya Temeke Changombe
Bahari beach na jirani
Upanga
City centre
Kila wiki basi mara 4 kuna mgao wa masaa kadhaa.
Na sasa hawataki hata sorry


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mgao upo siku zote. Ila hautangazwi sana. Nilishuhudia juzi hapa tu chuo kimoja cha serikali, hakukuwa na umeme wa uhakika kwa wiki nzima. Mara ukatike kutwa nzima, mara usiku wote. Lakini haikutangazwa popote.

Ni kama vile serikali ilivyopiga marufuku matangazo ya kamari kwenye luninga na redio, halafu mtu anakuja na kuisifia serikali kwa kudhibiti au kuondoa kamari. Kamari ipo tu, ila matangazo ndio yamesitishwa.
 
Mag3 we ni mchambuzi mzuri na bora sana. Wengi tunajifunza mengi toka kwako. Mabishano na ushabiki huu wa ccm na cdm unajidhalilisha kujiingiza humo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ni mchambuzi mzuri na bora sana anawezaje kuja na hoja chovu namna hiyo ya kutumia tukio moja kuwa ndio mtaji wake wa kisiasa? Wachambuzi wazuri na bora hutumia policy badala ya matukio.
 

Aisee sisi bado sana... hukumbuki walipigwa marufuku KUTANGAZA mgao wa umeme? kutokuwepo kwa mgao sehemu unayoishi siyo kigezo au mwenzetu wewe unaishi "nchi nzima"?
 
TAFAKARI YA LEO!

Walipofanya warusi habari zikaenea ulimwenguni,walipofanya waamerika vitabu vikaandikwa na tukavisoma sana na kufundisha vizazi vyetu kwamba hizo ni zama za mapinduzi ya viwanda ulimwenguni. Tukajifunza na mengine juu ya ustaarabu wa binadamu.

Walipoibuka wachina na wengine wimbo ukaendelea ule ule lakini sasa Afrika ilipoanza kuchomoza Kwa kuacha kufikiria Kuwa bila wao walioitwa wa dunia ya kwanza sasa wimbo umebadilika zikaongezwa aya za demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, ukikwaji wa haki za binadamu, utawala bora, mapambano dhidi ya hili na lile na mengine mengi kama hayo.

Tanzania ilipobadilisha msimamo wa kukaa wakati wengine wanaruka hoja sasa zinazoibuka ni fulani kasema hili Leo BBC au VOA au DW au CNN nk ilimradi tu tupoteze mwelekeo wa ujenzi wa SGR, mradi wa kuzalisha umeme wa Stiglers Gorgle,utoaji wa elimu kwa watoto wetu, uimarishaji wa shirika letu la ndege, uboreshaji wa miundombinu yetu ya barabara, uboreshaji wa kilimo chetu n.k.

Ni vyema basi leo tukumbuke kuwa nasi sasa tunapita katika njia sahihi ili vizazi vyetu visiendelee kusikia mabaya tu ya nchi yao bali waone mema mengi ya mama Tanzania na kuyalinda Kwa gharama yoyote ile.

TAFAKARI NAMNA BORA YA KUILINDA NCHI YAKO NA USITHUBUTU KUMVUA NGUO MAMA TANZANIA. MUNGU AKUBARIKI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…