Wanabodi,
Nimetafakari sana katika kipindi cha takribani mwezi mmoja na zaidi, sijasikia na wala kuona Rais wangu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli akizungumza katika vyombo vya habari. Ninachokiona ni Makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hasani akiwa na Mawaziri wake katika mkoa wa Tabora. Vilevile namwona Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa Majaliwa naye akichanja mbuga kunyoosha mambo serikalini katika mikoa mbalimbali. Style hii mpya ya uongozi nimeipenda na imewavutia watu wengi. Nadhani mtindo huu alioamua kuutumia ni mzuri sana na una tija kubwa kwa taifa.
Licha ya watu kuendelea kuzunguka katika nchi za Ulaya na Marekani kuponda mazuri unayoyafanya hapa Tanzania, wewe endelea kukaa kimya na endelea kumtumia vizuri Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Dr. Mahiga. Nchi imesimama vizuri na mambo yananyooka. Wewe endelea kuvuta pumzi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao kwani CCM watakupitisha kuwa mgombea wao. Sina mashaka kabisa na utendaji wako na uaminifu wako kwa taifa.
Nelson,
Uvinza, Kigoma.