Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Pole sana.
Viwanda vipya 3000. Viko wapi? Waweza kuvitaja?
Makinikia ? Wenzio wameshaachia. Yanakwenda.
 
Kamlalamikie Kijana Mzee Pole pole, anachepusha posho yenu.
Watakuja wale jamaa wa ufipa street watakwambia uende ukachukue buku saba pale Lumumba.

Yaani yote hayo uliyoyaandika thamani yake ni malipo ya shilingi elfu saba tu!.
 
Reactions: BAK
Tatizo lake kubwa ni kuruhusu vyombo vya dola kuwatoa roho na kuwatesa wanaomkosoa pale anapokosea..Akubali tu yeye ni mwanaadamu ana sifa ya kukosea
Achana na kukosoa tafuta shughuli nyingine ufanye !
 
Siwezi kuelewa hili bandiko mpaka nitakapolipwa pesa yangu ya KOROSHO
 
Reactions: BAK
Akili za nzi hizi akiamka pua juu juu kutafuta wapi kuna mavi.Umesahau kuweka namba ya simu kwa ajili ya uteuzi.
 
Reactions: BAK
Magu ni Rais bora wa viwango tatizo nina wasiwasi akimaliza muda wake kuzungumzia sifa zake chanya itakuwa ni sawa na kuzungumzia Azimio la Arusha kama alivyosema Mwalimu lazima uwe na moyo kama wa mwendawazimu kwahiyo huu ndio muda wa kutangaza mema yake kwa nguvu hakuna ajuaye kesho
 
UPUUZI MTUPU! mwizi, mzinzi, muongo, fisadi, mbadhirifu, mtekaji, mtesaji, mbambakiaji kesi FAKE na MUUAJI. Mtu hatari sana kwa mshikamano na amani ya Watanzania na janga kubwa la Taifa.
...alikubakia nani wako !?
 
Nampenda kumpongeza Raisi wangu John Pombe Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti wa SADC.Pia nimpongeze kwa mafanikio makubwa katika kuandaa na kufanya mkutano mkubwa wa viongozi wa SADC.

Nimeguswa na mambo mawili makubwa,la kwanza likiwa kuhusu Zimbabwe na la pili ni kuhusu utajiri tulio nao Wafrika hasa wanachama wa SADC.

Kuhusu suala la Zimbabwe ni ukweli ulio wazi ya kuwa Wananchi wa Zimbabwe wanateseka na kuumia kutokana na vikwazo nchi ilivyowekewa na jumuiya ya Kimataifa.Wakati wote wa kuomba kuondolewa vikwazo tumeshindwa (mimi na viongozi wangu) kujiuliza swali la “kwa nini Zimbabwe iliwekewa vikwazo na kwa nini bado vinaendelea?”.Tukiweza kujibu swali hili na kuchukua hatua stahiki Zimbabwe itaondolewa vikwazo kama Tanzania ilivyofutiwa madeni!!

Kuhusu utajiri wa Africa,hili nalo halina shaka ingawa washauri wa Raisi wanashindwa kutekeleza wajibu wao.Raisi wetu ni mtu wa “hard sciences” na kuna mambo ambayo kidogo yanahitaji apate kueleweshwa na watu wa Historia,Uchumi na sayansi ya jamii.Iran na Venezuela zina utajiri kuliko sisi lakini leo ziko wapi?Huwezi kupata jibu la hili swali mpaka upitie historia,sayansi ya jamii na uchumi wa Kimataifa.Tujiulize,leo inakuwaje Marekani inaiwekea vikwazo URUSI na URUSI inapata maumivu?

Historia ya kwetu hapa inatueleza ya kuwa 1967 kupitia azimio la Arusha tuliweka njia zote za uzalishaji chini ya umiliki wa Umma.Ni nini kilitokea wote tunajua.Mwalimu Nyerere aling’atuka tukiwa katika majadiliano na vyombo vya fedha vya “kibeberu”.

Nihitimishe kwa kumpongeza tena Raisi wetu kwa Uenyekiti na pia nichukue fursa kumuomba achukue fursa kuijua historia,uchumi wa dunia na Sayansi ya jamii.Naamini atafanya vizuri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…