Nadhani huyu GT anayemlinganisha Mako-meo na Nyerere, hamfahamu Nyerere.
Kwa waliokula sukari nyingi wala hawawezi kufikiria kuwalinganisha hao wawili. Ni sawa na kulinganisha milima ya Dodoma na Kilimanjaro. Sawa, yote ni milima lakini hailinganishwi.
Huyu wa sasa kafanya nini cha maana kiasi cha kuwapa watu ujasiri wa kumlinganisha na Nyerere? Nyerere alikuwa jabali na huyu wa sasa ni jiwe tu. Kama wa sasa ni bwawa basi Nyerere alikuwa bahari. Kwa wale wanaodai kuwa Nyerere hakufanya kitu na vitu vingi vimefeli, wanajidanganya. Baadhi ya miradi mikubwa kabisa ya Nyerere ni kuanzisha nchi inayoitwa Tanzania. Je, imefeli (kama itafeli itakuwa chini ya hawa wa sasa lakini si chini ya mamlaka ya Nyerere). Nyerere aliamini katika ukombozi wa Afrika jambo ambalo limefanikiwa sana.
Wee! Unamlinganisha Mako-meo na Nyerere? Julius alimtwanga Idd Amin wa Uganda. Huyu wa sasa sidhani hata keshasimamia mapigano na vibaka, achilia mbali jambazi.
Ingawa binadamu ameumbiwa faraja kubwa sana ya kusahau, na wakati mwingine kutumia fursa hiyo kubadili ukweli wa kihistoria, bado Nyerere hana mfano wake. Kwa taarifa yako, wakati wake hakuna ambaye angethubutu kutoa makontena bila kulipa ushuru. Tafuta kwenye historia vita dhidi ya wahujumu uchumi, upate muziki wake. Acheni kumtania Mako-meo maana hata mwenyewe anajua kuwa ama mnamvika kilemba cha ukoka au mmebobea katika kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Huo ni uatani m-baya sana kwa rais wa nchi!