Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ni 'men' siyo 'mens' mkuu,rekebisha.
 
Abaki Jiwe peke yake maana hataki mawaziri wake wapate sifa anataka sifa zote ziende kwake peke yake.
 
Kiukweli hata Bunge halihitajiki kwa vile nchi inaendeshwa kwa decree au matamko. Rais analitumia Bunge lenye wabunge wengi wa chama chake kama muhuri wa kubariki maamuzi yake.

Mawaziri hawana uhuru wa kufanya maamuzi ambayo wamebuni. Kazi yao ni kutekeleza maagizo ya Jiwe
 
Abaki Jiwe peke yake maana hataki mawaziri wake wapate sifa anataka sifa zote ziende kwake peke yake.

Huenda aliona PM kwenye safari zake anapata ujiko mpaka watu wanasema 2025 awe rais, huku yeye anampango wa kukaa zaidi akaona na yeye ngoja aingie front line.
 
Mawaziri wa awamu hii wengi wao wana majukumu makuu mawili; kumsifia mkuu wao muda wote, na kuzurura tu mikoani kwa lengo la kujilipa posho.
 
Rais Magufuli ni binadamu, anamapungufu yake makubwa tu, ana jazba, anakasirika haraka na kutoa kauli zisizopendeza(kama ile ya yule mama kule Songwe) ila pamoja na hilo bado ni kiongozi mzuri mwenye nia ya dhati ya kupambana na umasikini wa Watanzania.

Tunapaswa kumuung mkono atekeleze miradi mingi(sio yote) ambayo ina maslahi mapana kwa nchi, miradi kama bwawa la Nyerere huko mto Rufiji, reli ya kiwango cha kati, kufufua na kupanua bandari zetu, kuthibiti ujangili wa wanyama wetu nautoroshaji wa wanyama nje ya nchi na miradi kadhaa ya maendeleo. Ukiachilia mbali miradi mingine ya kawaida kama ujenzi wa shule, hospitali, barabara na mambo kama hayo hii ni kawaida kwa uongozi wowote ule kutelekeza ila hii miradi mikubwa michache ina naslahi mapana ya nchi, hii inatekelezwa na visionary leaders peke yao, kwaba hata akifa siku moja bwawa la Nyerere litakuwepo, reli itakuwepo, wanyama wetu watabaki.

Pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu na unafiki wa wasaidizi wake kupenda kumtukuza kupita kiasi ila bado ni kiingozi mwema mwenye nia njema na nchi hii. Tumpe muda wa miaka 5 atekeleze miradi yake hiyo yenye maslahi mapana ya nchi. Pamoja na hilo siungi mkono mwazo ya kitaahira kwamba Magufuli atawale maisha eti kisa hakuna kama yeye nchi hii yenye watu zaidi ya milioni 55, haya nayaita mawazo ya kitaahira na Mwl. Nyerere aliwahi kusema ukiona watu wanakupigia kelele uendelee tu kutawala kwa kukupamba kua hakuna kama wewe basi ujue hawaisemei nchi bali wanasemea matumbo yao na familia zao ambao hawana uhakika kama takaekuja atawabakiza kwenye hizo nafasi.

Mwisho haya ni mawazo yangu na maoni yangu binafsi whether you like it or not.
 
Miaka mingi tilikuwa tunasikiliza maneno mazuri ya viongozi na ahadi hewa
Kumbe walikuwa wanatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa wanatudanganya wakigeuka nyuma wanaenda kupora mali zetu

Hatuhitaji hotuba nzuri kwa sasa zinazojenga matarajio hewa tunahitaji utendaji tu
Watanzania tumechoka kusikiliza story

Magufuli amejua hilo anaongea ukweli ukitaka uchukie au unune nyeupe ni nyeupe na nyekundu ni nyekundu

Ukiangalia hotuba za Magufuli sio za kubembelezana tena km watanzania walivyozoea kubembelezwa na kudanganywa
Magufuli amejua kutunyoosha maneno kidogo utendaji 100%
Keep it up Magufuli
 
Kuunga mkono si tatizo, lakini haiwezekani iwe kuungwa mkono tu lakini kuoneshwa changamoto mkukosolewa iwe tabu, yapo anayopatia hapo anaungwa mkono lakini akubaliane pia na wale wanao mkosowa yaani kwa maana nyingine wale wanao muonesha njia mbadala, yeye na wanaompotosha kwa kumsifia watu hao ni maadui kwake na kwa kisingizio cha si wazalendo,
Hilo ndilo halikubaliki, ukikubali kupokea kubali na kutoa.
 
Sawa ,tumekusikia ila asikilize mawazo ya watu wengine,akubali kukosolewa ,ashauriane na wengine huwezi kuwa perfect 100% kabla ujafanya maamuuzi shauriana na wasaidizi wako sio kila kitu jazba tuu na maamuzi yako ndio yako hatuendi hivyo hata kama unasaidia wanjonge ,halafu wepi hasa ?wa nchi ipi ,mkoa upi kama kila mahali tunalia tu tena hali inazidi kuwa mbaya wakati tunaona wachache wananeemeka
 
Utendaji wa bila kufuata utaratibu mliojiwekea kama Taifa ni dharau na ujuaji, kwani kuna shida gani kufuata utaratibu? Ama kuondosha mkingano huu unaoendelea basi KATIBA MPYA tena ile RASIMU YA MZEE WARIOBA ifufuliwe na ianze kufuatwa si mambo ya one man show, na ndio utaona kauli za nikiondoka nani ata ata ata ... huu ujinga ndio hamtakiwi kuushabikia,
 
MAENDELEO HAYANA CHAMA

Sisiem oyeee

"Nitahakikisha mpaka 2020 hakuna mpinzani(chama pinzani) Tanzania"

Sisiem oyeee


MAENDELEO HAYANA CHAMA
 
Yaani huu utawala bora mkoloni, maana umejaa unafiki na mbaya sana watu wa kusema hapana hapo umekosea hawafanyi hivyo, viongozi wa dini ndio wameuza imani zao kabisa
 
NAONA ASUBUHI NA MAPEMA VIJANA WAMEINGIA KAZINI TAYARI



"WANANCHI LIPENI KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA"


"KAMWAMBIE MUME WAKO DIWANI NA M'BUNGE ULIEMCHAGUA WAKUPATIE MAJI"


Sisiem oyeee.. maendeleo hayana chama


ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI
Dawa ni kutokulipa hizo kodi tu
 
Kama Alishindwa Kuendeleza Chato Zaidi Ya Miaka 20 Aliyoitawala Ataweza Tanzania ? Watu Mkoa Wa Geita Wanaishi Kwenye Umasikini Yeye Anawaza Maendeleo Ya Vitu Kujenga Uwanja Wa Ndege Sijui Ndege Zitabeba Nyani"?
 
Huko ndo kujimwambafy mwambafy kunakosemwa. Kujifanya mjuaji hukosei hupingwi hupangiwi huulizwa...Dah full umwambafy!
 
Kwa tanzania utaratibu ni kuruhusu upigaji na wizi. Kiutaratibu kabisa kalamu ya 1000 inatakiwa inunuliwe kwa elf 10000. Huo ndio utaratibu wa manunuzi tuliojiwekea kama tukiamua kuufuata.
 
The end [result] justifies the means! Kwa maana nyingine, haijalishi njia tunayotumia, cha muhimu ni kupata matokeo tunayokusudia.
 
Kwa tanzania utaratibu ni kuruhusu upigaji na wizi. Kiutaratibu kabisa kalamu ya 1000 inatakiwa inunuliwe kwa elf 10000. Huo ndio utaratibu wa manunuzi tuliojiwekea kama tukiamua kuufuata.
Huo ndo uelewa mnaoeleshwa, hivi shida ipo wapi kuleta hiyo RASIMU YA KATIBA YA MZEE WARIOBA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…