Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania


Ukawa tuko imara na tunaendelea kuimarika kuliko wakati wowote ule ,
Zege hailali ni mpaka tuhakikishe tunapata katiba bora inayotokana na Maoni murua ya wananchi watanzania
 
imebidi niangalie umejiunga lini na JF. Wenye akili wote wanajua kuwa uwepo wa upinzani ni kitu cha muhimu sana. Kumbuka bila upinzani tusingejua WEPA, BUSAKI, RICHAD, wala CROW. Anyway, tuna RAIS ambaye ni makini na anatambua kuwa upinzani ni muhimu
 
Niambie Dada FF, nakumbuka mwaka jana tulibishana sana kuhusu kushuka bei ya umeme. Niambie, Je, imeshuka? mimi nilikwambia haitashuka, wewe mishipa ilikusimama ukisema itashuka. Haya jitetee na umtetee na yule ambaye tulikwambia anafanya vibaya ulingoni, ukaishia kusema tuna chuki naye kwa 7bu ya ... Sasa Dr. wa ukweli yuko ulingoni!!!! umeona kazi yake? Usichekecheke shambani, nyani watakuona -----, watamaliza shamba la mahindi, umesikia kashfa ya tirioni 1.2 tumeibiwa nasikia na wenye nchi. Ngoja Dr. JPM aje
Bora umeamua kurudi njia kuu.
 
maalim seif kashida lakini ndo maana ccm wameweka mpira kwapani kabla ya dakika 90! sidhani kama ni sahihi kumlinganisha na loser lowassa!

 

Umeme utashuka, subiri mradi ukamilike, mbona una kiherehere kijana.
 

Yangu macho jamani, napita tuu
 
nlitaka mtoko wa xmass ila najiuliza whatwould magufuli respond in case............
 
Magufuli anafanya vitu ambavo watu walifikiri haviwezekani. Magufuli aongeze kasi tu na a keep pace, ataheshimika mno kimataifa. Wazungu mpaka watasafiri kuja kumuona huyu Magufuli ndo nani.
 
Barabara ya mwenge-morocco waweke na njia ya mabasi yaendayo kasi kabisa, sio kufanya vitu mara mbilimbili.
 
Mbona mimi sioni la ajabu ambalo Magufuli kafanya mpaka hivi sasa..?

Habari za matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi na kutokuwa na vipaumbele vya maana ni jambo ambalo wengine tumelipigia kelele sana humu tokea JF ianzishwe miaka karibu 10 iliyopita.

Tumepiga sana kelele humu kuhusu watoto kukaa chini, kuhusu wagonjwa kulala chini, kuhusu aibu ya uwanja wetu wa ndege na kuhusu mengineyo mengi tu.

Tukahoji matumizi ya mabilioni ya shilingi yaliyotumika kwenye sherehe za miaka 50 ya uhuru huku madaraja yakiporomoka kwa kuzidiwa na mvua.

Halafu kuna wengine humu wakawa wanatetea huo ubadhirifu wa CCM kwa nguvu zao zote. Halafu leo hii wanajifanya ndo wapiga vuvuzela wa Magufuli.

Inastaajabisha kweli.

Mtu yeyote mwadilifu na mwenye common sense hatashangazwa na anachofanya Magufuli. Lakini, lazima angeshangazwa na jinsi serikali za CCM zilivyokuwa za kipumbavu maana hizo ndizo zimetufikisha hapa tulipo.
 
Mkuu, Kupiga kelele na kutenda ni vitu viwili tofauti.

Tuna mifano mingi hai ya wanasiasa wanaopiga kelele lakini hawawezi kuziishi kelele zao.

Hata Mbowe na genge lake walipiga kelele kwa zaidi ya miaka nane huku mapovu yakiwatoka kwenye mikutano wakituamisha ni wapambanaji wa kupinga ufisadi na matumizi mabaya ya kodi za wananchi lakini siku ambayo kiongozi wa ufisadi Lowassa na genge lake (kama walivyotueleza) walipobisha hodi kwenye milango ya ofisi zao, wakaanza kukana hata zile kelele walizokuwa wanazipiga. Hoja za kupambana na ufisadi wakaziweka kwenye makabati.

Hata lile gari la KUB alilokuwa anatuambia bora lipigwe mnada ili pesa zitumike kununua madawa aliamua kwenda kulichukua kinyemela.

Ni wanasiasa wachache sana nchini kama siyo ulimwenguni kote ambao wanaweza kufanya kile anachokifanya Rais Magufuli.

Ni lazima ujiulize, kwa nini kile anachokifanya Rais Magufuli kinaonekana cha ajabu katika sehemu mbali mbali duniani mpaka hata raia wa nchi za Magharibi wanataka awe 'benchmark' kwa viongozi wao wakuu wa nchi.
 

Ndio rais wa kwanza wa nchi ya Kiafrika kubana matumizi,si unajua tena sisi Waafrika ni maarufu kwa kutumia sana huku nchi zetu zikiwa dhohofu bin hali?
 

"Give credit where it is due"!! Kupiga kelele nyingi kwa chura hata wawe millioni hakujawahi kumkataza Ng'ombe kunywa maji kisimani!

Kwa kuwa JPM anayetekeleza anagalau haya kidogo uliyokuwa ukiyapigia kelele ni M-CCM vilevile! kwa mtu mwenye busara na akili timamu kabisa kabisa; Hana budi kutambua kidogo alichokifanya JPM so far; Kumbuka kwamba uadilifu sio jina la mtu Bali ni sifa ya vitendo vyake! Tunachokishangaa ni JPM kuwa mwana-CCM kwa itikadi lakini amekuwa Mwana-UKAWA kwa vitendo na uwajibikaji!! BRAVO JPM
 

Lini utaacha kuongopa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…