Chei chei wanagenzi
DIBAJI
Bandiko hili si kwa ajili ya kumsifia au kumtukuza Dr. Magufuli, hasha, bali ni baada ya kuyarejelea matendo ya watangulizi wake na serikali zao kwa kuzunguka nyuzi 360 upande mmoja na kuuchukua mwendo huo huo kuwatathmini watanzania hasa wapenda siasa, wanaoijua siasa, wachambuzi wa siasa na wale bendera fuata upepo. Ndipo lilipozaliwa wazo hili DR. MAGUFULI ALAMA YA UZALENDO NA UWAJIBIKAJI.
Nimekua mfuatiliaji wa siasa za Tanzania tangu utawala wa Rais Mh. BWM, nimeona maovu mengi kuliko mema.
1998-99 wakiwa amua kwa sidhani Kama Ni elimu na utashi wa matumbo yao kiua TPDC.
Nimeona utapiamlo wa kisiasa, nimeona na nimesoma miradi kede kede iliyochapwa na kunakshiwa kwa uzuri na uturi, nimeona pia mipango mikakati chekwa chekwa ikitumia mabilioni ya Watanzania katika vikao tendaji rejelea MKUKUTA, MKURABITA,
(EPZ/SEZ) Nk.
Rais Mh. BWM, hakuwa mtu wa maneno mengi na wananchi yeye, alikua akiongea Mara nyingi kupitia vitabu vyake vilivyokua vikichapwa na aliyekua Kampaini Maneja wake Mzee Walter Bugoya mmiliki wa kampuni ya uchapaji ya MKUKI NA NYOTA, vitabu hivi vikiitwa UWAZI NA UKWELI.
Lugha iliyokua ikitumika katika vitabu hivi ilikua Ni lugha ya KIMKAKATI, ilikua ni lugha ambayo haikuhudhuria darasani tu bali ilifanya vizuri sana katika mtihani wake wa mwisho.
Tukipenyezewa za chini ya kapeti eti moja ya chumba ndani jumba jeupe kiliwaka moto na chanzo ni pasi ya umeme, (hili kama ndivyo lilivyo linafikirisha).
Tukashuhudia ubinafsishaji wa benki yetu ya NBC 1997 ukifanyika kwa kile ninachoweza kiita STUPIDITY AT IT'S EXTREMELY QUALITY.
*********
Mwaka 2005, wakati CCM wakiwa Dodoma kumpitisha/kumtangaza mgombea wao ilikua majira ya saa 11-12 jioni zilisikika shangwe kubwa mji ukazizima, nilikua maeneo ya Jangwani, ilinibidi nitafute sehemu nami niwe shuhuda kwa yajayo.
Yajayo yalifurahisha kwakua ndani ya miaka miwili tu, tulishuhudia nchi ya wapigaji, nchi ya wachumia tumbo, wakina unanijua mimi nani wakitamalaki katika kila nyanja, Bar, Barabarani (Marehemu Ditopile Mzuzuri) na hata katika sehemu za kazi wakijaa wakina unanijua mimi nani?
Tulishuhudia adha ya kelele za Majenereta kwa takribani saa 16 kila siku, mfumuko wa bei ukatamalaki sukari toka shilingi 400-450- 900, Unga wa ugali 250 hadi Mia 600 (tarakimu hizo hapo juu zinatofautiana kulingana na mazingira na mikoa pia).
Tukashuhudia matukio mawili ya hovyo kuwahipo kutokea, lakwanza Ni kuchomekewa noti ambazo zinachuja rangi (noti ya shilingi 5000 ulikua ukitumia tishu ule uzambarau ubakia kwenye tishu).
Na tukio la pili, Serika kukiri kushindwa kwa vitendo pale walipo jaribu kuondoa 500 ya noti (hela ambayo ikipita kwenye mikono ya watu 5 haifai tena kutumika) na kutambulisha 500 ya sarafu, sababu kubwa ikiwa eti Kuna wajanja wanazinunua na kuziyeyusha Kisha kutengeneza Vito vya Silva.
Kama hilo halitoshi, tukimshuhudia Mh. Kikwete akibembea na First Lady huko majuu, tukipata picha za Steven Sigga na Mh. Wakitabasamu, huku Boyz II men nao hawakuacha mbali na mengi yenye mfanano huo wa sura.
Hapa Mh. Mbatia alitoa tathmin yake kwamba katika miaka 10 Basi mitano alikua nje ya nchi.
Ama hakika yaliyokuja yalifurahisha kwakua ndicho kipindi ambacho Wanafamilia walithubutu kuweka ngoma na ubwabwa wa kutosha kisa mtoto kapata kazi TRA au TPA.
Huyu yeye akaamua kuongea na wanywa kahawa wezie wa Shibamu na Saigon (wazee) kati ya kila mwezi au miezi miwili akiwasmailia nao wakamsmailia back, kwakua walikua mwisho wa kusmailiana itifaki itazingatiwa (BAHASHA ZA KAKI)
DR. MAGUFULI ALAMA YA UZALENDO NA UWAJIBIKAJI.
Ama kwa hakika Rais ajae, atapata imma wakati mgumu au wakati rahisi, atapata wakati mgumu kwakua watanzania sasa wanacho cha kukifanyia mzania, watanzania wanajua sasa kwamba kama Rais akitaka kulipekea Taifa kuwa pango la walanguzi na wahujumu uchumi, linawezekana au kuiongoza nchi kuwa ya Maziwa na Asali.
Kwanini unaweza kuwa wakati mzuri kwa Rais ajae, Ni rahisi sana kwakua tayari atakuta kile kisima kilichokua kikilalamikiwa kwamba maji yatokayo humo husababisha muwasho wa ngozi ukiyakoga kitakua Kisha safishwa na maji yake si kuoga tu bali hata kwa matumizi mengine pia.
Aidha kuna vi exclusive amekua akitupenyezea kutupa picha ya kwanini URAHISI sio RAHISI kama vile Mchezo wa kufungulia mabwawa ya kuzalisha umeme ili kina kishuke wazime mitambo akina AMITA BACHANI pale Mtaa wa Sikukuu waweze ku import makontena ya Majenereta.
HITIMISHO
Kwa miaka hii minne na ushee sasa, Dr. Magufuli kama sio kafanikiwa Basi kaonyesha kuyafikia maendeleo ya kweli haya hayakwepeki;
1. Ushikaji kwenye kazi hakuna ( Mh. Kitwanga, Mh. Prof. Mhongo)
2. Muda wa vikao mkakati na vikao tendaji hauna tena nafasi.
3. Haijalishi wewe ni nani unapokaa kwenye njia unaondoka tu (Dr. Kipilimba)
4. Tanzania ni kubwa na muhimu kuliko mtu yeyote.
5. Fedha ni za kwako, ardhi iko chini ya uangalizi wake, (Habinda Seth, Rugemarila) nk
NAIPENDA AFRIKA, NAIPENDA TANZANIA MUNGU IBARIKI KAZI YA MIKONO YETU.
Sent using
Jamii Forums mobile app