Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Habari za mtu huyu zimeenea katika miji yote ya Galilaya na jerusalem..hakika ningependa kumfahamu mtu huyu..yeye ndie masiha ama tungoje ajae?
 
NyaniNgabu ni kweli kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kustaajabu haya. lakini pamoja na yote ni kitu ambacho wengi hawakutegemea. wengi tulijua ccm business itakuwa as usual japo bado ni mapema kumtathimini kiujumla ila kwa kuegemea muda huo huo mfupi amefanya vitu ambavyo wengi haswa hambao hawakumpa kura hawakutegemea kabisa. africa tuna matatizo ambayo yamekuwa ndo maisha yetu na watu mentality tumeshakubali kuwa sisi tupo hivyo na tunastahili kuwa hivyo na huwa tunajipa moyo kwamba Mungu ndo kaamua tuwe hivyo. ndo maana akija kiongozi na kufuta hali ya maisha hayo tuliozoea lazima watu wastaajabu sio kawaida
 
Last edited by a moderator:
Mkuu@Nyani Ngabu kelele ni kweli zilikuwepo lakini je zilifanyiwa kazi? kiuhalisia wengi hawakutegemea JPM kuyafanya haya akiwa katika nyumba ileile.. lakini Leo hii anadhihirishia ulimwengu kwamba inawezekana..

Nadhani tumpe muda na kumsapoti...kuendelea kuponda na kutounga mkono jitihada zake ni kujitafutia stress kwa miaka mingine kumi ijayo!
 
Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji. Tumezidi mno kumsifia Magufuli na kwa Style hii sijui kama atafanya vizuri. Tunamsifia mpaka atakosa changamoto na mwisho ataboronga.
 
Wabongo Tunarogeka Kirahisi kweli. Magufuli kafanya nini cha upekee ambacho hakuna kiongozi mwingine Alifanya. Sasa zimeongezeka tu promo through mitandao Ya kijamii lkn hakuna kipya Magufuli anarukaruka tu nashangaa watu wameshasahau shida zote. kisa Muhimbili vimeongezwa vitanda utafikiri nchi nzima vimeongezeka. Nilikuwa karibu nanasa kwenye mtego wa Magufuli lkn nimestuka Magufuli ni CCM na atafanya vile CCM wanataka.
 

Sikuwa mfuasi wake lakini kwa hili nampongeza. Sasa unaposema huoni cha ajabu, hv mambo magumu kama haya unapoyasemea jf yanatekelezwa? Tulitaka mtu mwenye maamuzi magumu haya ndio maamuzi magumu sasa. Baba alinifundisha UKIKOSA ULICHOKIPENDA PENDA ULICHOKIPATA. Wasaaalam.
 
Nyie mnaosema kua hakuna la ajabu alofanya..hebu jitokezeni hadharani halaf muyaseme hayo mnayoyaandika...Nyumbu nyie!!
 
Anayesema haoni cha ajabu kwa anachokifanya magufuri akapimwe akili aina za viongozi kama magufuri wanaoguswa na matatizo ya wananchi wao ni wachache sana.
 
Rais Magufuli anashangaza dunia kwa sababu hiki anachokifanya sio kawaida ya watawala (viongozi?) wengi wa Afrika.Watawala wengi wa Afrika ni wezi wakubwa na wapenda matanuzi na anasa.Wengi wana kaliba ya Mfalme Nebukadreza.Mfano Dos Santos wa Angola,Ali Bongo wa Gambia,Jacob Zuma wa SA n.k.
 

Mimi binafsi nilijua hatuna president makini tangu 2005 nov.
Yapo mambo ya msingi yaani basic ambayo president anatakiwa kufanya, na hicho ndo magufuli anafanya.

Ukiwa una kiwango cha mh. JK then utaona Kama JPJM anafanya makubwa but those are basic things to be done at the level of presidential position.

Sasa mi nasubiri afanye beyond that level kwa mtupo wangu wa jicho( my scope)
 

Umezungumuza ukweli mchungu ambao wengi hawataki kusikia lakini hicho ulichosema ni sahihi kabisa.

Naweza nikasema Mungu ameiona Tanzania kama Tungepata kiongozi kama aliyepita sijui ingekuwaje ndani ya miaka kumi ijayo?
 

We we nimpenda sifa tuu, ubovu wa walio mtangulia unamfanya magufuli aonekene mzr. We we kelele zako zili zaa matunda gani?
 
Anachofanya ni cha kawaida sana, raisi yoyote anatakiwa kufanya hivyo, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuimarisha uchumi, kuboresha huduma za jamii na kuweka uongozi bora.
The big question is; je, umewahi kuona maraisi wa kiafrika wakifanya hivyo? Wanatumia zaidi ya wanachopata, wakiwa madarakani wanajisahau na kujiona miungu watu...
Hem ona hayo madudu yanayoibuka kila siku, as if the country was in autopilot for 10yrs.
 

Hivi aliyoyafanya mpaka hivi hayakuwahi kabisa kufanywa na Nyerere?

Au kwa vile wengi wetu tuna kumbukumbu fupi?

Au kwa vile wengine walikuwa hata hawajazaliwa kipindi Nyerere yuko madarakani?

Hem ona hayo madudu yanayoibuka kila siku, as if the country was in autopilot for 10yrs.

Hata hayo madudu wala si mapya. Tokea kipindi cha Mwinyi yalikuwepo.

Kipindi cha Mkapa yakawepo.

Hata kwenye zama za maisha bora kila Mtanzania yalikuwepo.

Kwa hiyo hakuna kilicho kipya sana ambacho kimeibuliwa katika hizi wiki nne.
 
Jana nimenunu petrol nikashangaa nagongewa dirisha....eti napewa risiti za EFD bila kuomba...nilishindwa kujizuia nikaanza kuwacheka....MTANYOOOKA....lazima mlipe kodi...!!!!!!!

Naweka mafuta kwenye hiki kituo kwa muda mrefu sikuwai jua hata kama wana EFD
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…