Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Huu ulaghai haukubariki aiseeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM huwa mnatuona watanzania hatuna uwezo wa kufikiri
Hawa watu ni shida kwa nchi hii na ustawi wetu.Hawana Sera wala itikadi yoyote ya kuwaletea Watanzania maendeleo.Wamebobea kuhadaa wananchi kwa slogans nzuri nzuri kila wakati wa uchaguzi,wakiingia madarakani wana kiburi cha kuangamiza wanaowakosoa/wanaohoji utendaji wao.
 
Haya ni matokeo ya kukosa mlo kamili. Ukipata mlo mmoja kwa siku tena usio kamili lazima uwezo wa kufikiri utakuwa mdogo.
 
Janja ya nyani hio.

Ukitaka kukamata kuku kwa urahisi mdondoshee punje za mahindi mpk ndani kwako,akiingia ndani funga mlango mchinje.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUNATEKELEZA:
Vijiji zaidi ya 8000 kati ya vijiji 12000 nchini Tanzania vimefikiwa na umeme wa REA.Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 ni vijiji 2000 pekee ndio vilikuwa vimepata umeme

Hivyo ndani ya miaka minne ya mheshimiwa Rais Magufuli madarakani vijiji zaidi 6000 vimepelekewa umeme.
Huu ni utekelezaji wa ahadi uliotukuka.

Ikumbukwe wakati Rais Magufuli anaingia madarakani vibaraka wa mabeberu pamoja na wapinga maendeleo walipeleka umbea ughaibuni na hatimaye Serikali kunyimwa fedha za MCC zilizokuwa zitumike kupeleka umeme vijijini.

Serikali madhubuti ya CCM chini ya Babalao Magufuli ilijidhatiti na kuendelea kutumia fedha za ndani na hatimaye leo hii tunashuhudia matokeo chanya na ya haraka.

VIVA MAGUFULI VIVA CCM YA MAGUFULI

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 

kajitahidi lakini unavyosema sio ukweli kamili . Umeme uliongezeka sana wakati wa Millennium Fund ya George Bush na ilivyosimama baada ya uchaguzi Magufuli akaendeleza. Lakini kusema yeye ndiye kaleta umeme kwa 73% ya vijiji si kweli! Na sehemu nyingi umeme tayari ulikuwa umefika vijiji vingine vya karibu. Naona kama kawaida ya wengi kuna vitu kwa maksudi mnajisahaulisha. Wakati wa Kikwete umeme uliwekwa zaidi sema tu pesa ilikuwa sio yetu kama sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…