Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni , kiufupi JPM ni kiongozi mzuri , Mungu ampe maisha marefu , huyu mzee kafanya mengi sana.
Watanzania, ni mambo ya ajabu yamefanyika katika nchi hii, ya ajabu! Ninaposema ya ajabu... mtu alikua yuko radhi kuuza maisha ya watanzania kwa pick-up


Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais John Pombe Magufuli
 
Watanzania, ni mambo ya ajabu yamefanyika katika nchi hii, ya ajabu! Ninaposema ya ajabu... mtu alikua yuko radhi kuuza maisha ya watanzania kwa pick-up


Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki rais John Pombe Magufuli
Maneno ya unafiki tu haya na hayana polite. Mbona hajawahi kuongelea wizi wa nyumba za Serikali, Kivuko cha Bagamoyo, Meli ya Samaki, uwanja wa Chato wa ndege?

Mbona kamfukuza kazi Prof Assad CAG aliyesema mwaka 2016/ 17 kuna Tsh Trillion 1.5 hazionekani?
mama D, msifie Leo lakini subiri atakapotoka yeye uje u-comment tena. Tanzania haijawahi kuibiwa fedha nyingi kwa kipindi kifupi kama kwenye his awamu ya TANO.

Asidanganye kwa nini hasafiri nje. Tatizo ni afya yake mbovu ambayo ina pacemaker
 
Hahah ulienda kuzitafuta ukazikosa?

Wewe ni sawa na mwanamme ambaye unakuta nyumbani kuna kuku mwanamke kapika unafulahia kula hiyo kuku kisha unauliza mwanamke ili elfu kumi na tano ipo wapi? Wakati pesa ya kuku hukuacha na unafualahia kula.

Kisha unaanza kutangaza huko eti mwanamke kakuibia elgu kumi na tano wakati umekula kuku bila kuuliza pesa yake imetoka wapi?

Hizo ndege zinazonunuliwa magufuli anatoa pesa yake mfukoni kununulia taifa?
Mbona hamuulizi hizo ndege pesa imetoka wapi lakini mnapanda mkifulahia.
Ni awamu za CCM ndo zilimefanya hayo... Hata awamu hii zile 1.5T hazijulikani ziliko
 
Kiukweli Tanzania iligeuzwa Kama nchi ya kila mtu kupiga mpaka ufisadi na rushwa ikawa sehemu ya maisha yetu.Tumuache Magufuli atunyooshe aisee
 
Maneno ya unafiki tu haya na hayana polite. Mbona hajawahi kuongelea wizi wa nyumba za Serikali, Kivuko cha Bagamoyo, Meli ya Samaki, uwanja wa Chato wa ndege?...
Hapa umeingiza ushabiki wako wa kisiasa zaidi
 
Basi sawa, weka na yale manunuzi ya madiwani na wabunge upinzani, weka na namna alivyowashughulikia wapinzani - ni record yake pia
 
Wana JF

Wale waliokuwa wameweka vibanzi kwenye macho Huku wakitetea debate yenye ubishi na utata kwamba urban area is better than rural Area, sasa DK. Magufuli kavibadilisha vijiji kuwa na kila kitu. Maji, umeme, Barabara za lami, mahospitali, shule kila Kata.

Wale wabishi wa zamani wameanza kukubali wenyewe kurudi kijijini kwa hiari baada ya maisha kuwa magumu mjini. Mission town wote wameondoka, sasa hivi ukikutana nao utawasikia wakikubaliana na hoja kuwa kwa sasa rural area is better than urban area.
 
"Rural area".Inaweza ikawa kweli lakini hebu fikiria Dar es salaam imepata umeme miaka ya 40 na kijiji cha nata Serenget kimepata umeme 2007,je unaweza kusema Nata ni bora kuliko dar?

Dar ukizidiwa Mwananyamala hospitali unapelekwa Muhimbili,kwa mtu wa Nata kuipata Hospitali inayokaribiana na hadhi na Muhimbili ni lazima afike Bugando,je Nata ni bora kuliko Dar?

JPM kafanya mazuri lakini tusisifie mpaka tukawa kama punguani!
 
Ungejua waliopo vijijini wanatamani kuishi mjini usinge ongea..nadhani hua unapitaga tu..hujaingia na kuishi vijijini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…