Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ndugu zangu Watanzania mimi sina chama cha siasa.

Ila ukiangalia huyu Magufuli ni kama Mungu aliipatia Tanzania zawadi baada ya Nyerere.

Huyu Baba anavyohangaika kuwatumikia Watanzania hadi unaweza kutoa machozi, amewanyanya Watanzania wote kutoka chini na sasa Tanzania imebadilika.

Ukimwambia mzungu, Rais Magufuli anasomesha watoto wa kitanzania bure hawalipi ada hawawezi kukuamini wanasema hilo hadi ulaya limeshindikana, ukiwaambia wazungu huyu Baba amepeleka umeme kila kijiji Tanzania wanaduwaa wanasema kwao vijijini wanatumia solar.

Sisi ambao sio watu wa siasa jukumu letu limebaki kumuombea na kumpigia kura huyu Baba mwenye huruma na upendo kwa Watanzania
Asante sana Magufuli kwa kututoa kimasomaso Tanzania.
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Rais Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Rais Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati..
KASHUSHWA KUWAOKOA WATU KUPITIA CCM? ILELE? WEWE NI EMPTY HEADED KABISA 🤣🤣🤣🤣😃
 
Watanzania hasa wachache tuache kujifanya hamnazo na badala yake tuzidi kuumunga mkono Rais wetu mpendwa Dr John Pombe Magufuli

Dr John Pombe Magufuli ndio Kiongozi pekee tunayeweza kujivunia kwa kulisuka upya Taifa ambalo siku za nyuma lilipoteza mwelekeo Kabisa

Watanzania wanaitaji maendeleo na Kiongozi mahiri ambaye amebeba maono lukuki kuhakisha Nchi inasonga mbele kwenye Medani zote na si mwingine zaidi ya #JPM ambaye tarehe 28 October 2020 anapata kura za kimbunga ili amalizie Mraba wake wa miaka mitano

Jukwaa la Uchumi duniani ( World Economic Forum- WEF- 2019) imeitaja Serikali ya Tanzania kuwa ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa Fedha za Umma na kuziacha nyuma zaidi ya Serikali 150 zikiwemo Botswana 37, Msumbiji 69, Kenya70, Uganda100, Malawi106. NI JPM- KAZI IENDELEE!
 
Rais Magufuli ameyafanya yasiyowezekana yawezekane Tanzania.

Mathalani utolewaji wa elimu bure; mapambano ya kweli ya rushwa na ufisadi; maboresho ya utendaji kazi Serikalini;
Utoaji wa huduma kwa jamii mijini na vijijini, mathalani leo hii umeme upo karibia vijiji vyote, maji mijini na vijijini, huduma bora za afya mpaka maeneo ya vijijini. Kuipeperusha Corona Tanzania.

Kwa misingi ya kuchagua kiongozi mwenye sifa zote za kuleta maendeleo, Rais Magufuli ndio suluhisho na matumizi sahihi ya kura yako ya ndio kwake. Mpe 5 tena Rais Magufuli. OKTOBA 28, 2020 USIFANYE MAKOSA


WhatsApp Image 2020-10-21 at 14.48.23.jpeg

Kumchagua mwingine nje ya Rais Magufuli ni kujirudisha nyuma miaka 50.
 
Ndugu Rais wangu John Pombe Magufuli naomba unisamehe, kwa muda mrefu nilikuwa nakupinga kuhusu uongozi wako lakini nimegundua kuwa I wrong.

Ukweli ni kwamba wewe ni shujaa wa taifa, askari wa taifa, na mjenzi wa taifa, nakuombea kwa mungu akusimamie katika majukumu yako.

Nawaomba Watanzania wenzangu tumuunge mkono rais wetu.

Mheshimiwa rais naomba unisamehe sana.
 
Mimi sasa naishi kwa amani kwani mungu ametuletea mtu sahihi nahatimaye naamini atashinda kwani yeyote afanyaye mazuri mungu humuongoza. Kazana baba kwan Taifa letu linakuhitaji
Basawaaaaaa
 
Wadau, huu ni uzi maalumu wa kuangazia na kujadili mafanikio ya Rais Magufuli katika kipindi chake hiki cha mwisho (2020 - 2025) kwa mujibu wa katiba tuliyonayo.

Kwakuwa ndio kwanza ngwe imeanza, tutakuwa tunaupdate mara kwa mara.

Viva Magufuli viva
 
Amefanikiwa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi... madogo sasa hivi wanalipa chini ya 5% ya mkopo wa elimu... walimu ajira bwerere...yaaani yupo njema eti!!!
 
Mpaka sasa ameshafanikiwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani. Ameitegua mitego yote iliyowekwa kuchafua amani ya nchi yetu kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Sasa uchaguzi umeisha, kazi ya ujenzi wa Taifa itapamba moto.

Hakuna maendeleo bila amani...
 
Mpaka sasa ameshafanikiwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani. Ameitegua mitego yote iliyowekwa kuchafua amani ya nchi yetu kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Sasa uchaguzi umeisha, kazi ya ujenzi wa Taifa itapamba moto.

Hakuna maendeleo bila amani...
Kabisa mkuu
 
Amefanikiwa kubomoa zaidi uhuru,umoja na ustawi wa taifa letu. Binafsi najisikia vibaya kuona wana ccm wakijinasibu ushindi japo wapo waliopambana na ni waungwana.
 
Back
Top Bottom