Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mkuu, sasa unategemea nini mtu kama Mmawia ambaye anaishi kwa kuuza mwili wake? Wateja wake wamepungua siku hizi
 
MIMI, si mwepesi wa kutoa pongezi, ila kwa hotuba yako ya jana nipo tayari kutukanwa na wanakada wenzangu ambao tumezoea, kutukanana wenyewe kwa wenywe,

ukweli ni ukweli tu yakuwa nchi hii ilifika hapa, ka sababu ya vigezo vya kishenzi, eti experience? what is experience, hivi ni mtumishi gani wa govt unajitamba mbele z watu eti una experience? hipi kama sio ya kutuibia mali zetu?

nakushauri Rais Yohana, mpe ukurugenzi wa ikulu idara ya habari huyo kijana maana kuna mizee inamendea hiyo nafasi inatamani kijana afe leo,
pili fanya mabadiliko ya baraza lako la mawazili maana waliopo wanafanya kazi kw mazoea, na vigezo mshenzi vya uzoefu, mfano waziri wa sheria, na wengine wakijitokeza ntakushauri maana najua unassoma maandiko yangu, ndio maana ulinisema live kuwa nimemtaja mteulewako kuwa hajasoma anafanya kazi sinza kumbe anamastaz, ila kwa ili stanii kuna mawaziri hawatokufikisha kileleni.
 
Napenda kutoa shukrani za dhati kwa Mhe rais JPM alipokuwa akiwahutubia Wakurugenzi wa Majiji,Manispaa,Miji na wilaya alipozungumzia juu ya Watendaji wa Kata,vijiji Jamaa hawa wako karibu na wananchi wanaongoza kwa kuwa kama Miungu watu pale wanapofanya maamuzi wananyang'anya haki RAIA hasa kama wafugaji wanapata shida sana wakurugenzi hawa wakawasimaie hawa watendaji wawahudumie RAIA wote bila upendeleo watoe haki pale panapostahili
 
Mheshimiwa Rais,kwanza nikupongeze kwa kazi ngumu, nzito na ya hatari ya kuhuisha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwenye Serikali, Taasisi za Umma na Halmashauri zetu.

Nchi hii ilikwishaharibika vibaya kimfumo na kiutendaji.Mambo yalikua holela holela kila mahali.Uzembe, wizi, mazoea, rushwa, kiburi, kutojali na kujuana ilikua kawaida.Hakuna kuwajibisha, kuwajibika, kuwajibishwa wala kuwajibishana. Ni mwendo wa holela holela mithili ya gari bovu liendalo kuzimu.

Mheshimiwa Rais umekabidhiwa basi ambalo lina hali mbaya, abiria wake ni wagonjwa na barabara ya kupita basi hilo mbovu. Yote matatu yanahitaji kwenda sanjari; kutengeneza gari, kutibu wagonjwa na kutengeneza barabara. Ni mambo mazito lakini amtegemeaye M/Mungu hana cha kupoteza.

Ni hayo tu Mheshimiwa Rais.
 
Ni kweli kabisa, mtu akipitia kwa makini sehemu mbalimbali za baadhi ya taasisi za umma kuna madudu mengi kiasi cha kutisha. Pengine suala la hiki chuo halijafika kwa wahusika ile waweze kuchukua hatua stahiki.

Kwa ufupi haya ni miongoni mwa yaliyofanywa na kuendelea kufanywa Chuo cha Ufundi Arusha:

a)Mkuu wa chuo alianza kufanya kazi chuo cha ufundi Arusha mwezi Septemba 2010. Mkuu wa chuo aliishi Hotelini kwa kipindi cha miezi mitatu (3) kuanzia Mwezi Oktoba, 2010 hadi mwezi Januari 2011. Wakati Mkuu wa chuo akiishi hotelini chuo kilikuwa na nyumba kwa ajili ya Mkuu wa chuo. Fedha iliyotumika kulipia hoteli wakati chuo kilikuwa na nyumba kingetosha kununua madawati mangapi ili kuondokana na tatizo la watoto wa shule kukaa chini?

b)Mkuu mpya wa chuo alianzisha utaratibu tofauti wa Mkuu wa chuo kuishi nje ya Chuo na hivyo kusababisha matumizi yasiyo ya lazima kwa chuo na serikali. Wakuu wote wa Chuo waliotangulia wakiwepo Wajerumani walikuwa wakiishi na familia zao kwenye nyumba ya Mkuu wa chuo iliyopo eneo la Chuo. Nyumba hiyo ilikataliwa na Mkuu wa chuo Bwana Richard J. Mushi Masika kwa hivyo kwa sasa wanakaa watumishi wengine. Kitendo cha Mkuu wa chuo kukaa nje ya chuo kimekuwa kikigharimu kila siku kuchoma mafuta ya kwenda kumchukua asubuhi na jioni kumrudisha kitu ambacho hakikuwepo hapo awali. Fedha ya mafuta na uchakavu wa gari kwa ajili ya kumfuata na kumrudisha mkuu wa chuo kwa mwaka ingetosha kununua madawati mangapi?

c)Zaidi ya Tsh 70,000,000/= zilitumika kukarabati nyumba ya chuo iliyopo eneo la Korido Kijenge jijini Arusha ili ifae kwa matumizi ya Mkuu wa chuo. Nyumba hiyo ilikuwa akikaa Mtaalamu wa Korea ambaye alifukuzwa kutoka katika nyuba hiyo kama kibaka ili ikarabatiwe kwa ajili ya Mkuu wa chuo. Fedha hii iliyotumika pasipo lazima zingeweza kununua madawati mangapi?

d)Zaidi ya Tsh 700,000,000/= zilitumika kukarabati jengo la Utawala la Chuo huku sababu kubwa ikiwa ni kuifanya ofisi ya Mkuu wa chuo kuwa na ukubwa mkubwa pasipo sababu ya msingi. Ofisi ya Mkuu wa Chuo peke yake ni sawa na ofisi tatu za kawaida. Wakati ofisi ya Mkuu wa chuo ikiwa kubwa kiasi hicho bila sababu yoyote ya maana, wafanyakazi wengine na hasa waalimu wanabanana kwenye ofisi ndogo huku wakiwa hawana hata samani za ofisi. Kiasi chote hicho cha pesa iliyotumika kuongeza ukubwa wa ofisi ya mkuu wa chuo zingeweza kujenga madarasa mangapi? na kama zingenunua madawati zingeweza kununua madawati mangapi?

e)Katika kipindi cha Januari 1999 mpaka Februari 2000 Bwana Richard J. Mushi Masika hakufanya kazi ya utumishi wa umma katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kuwa inafahamika alikuwa akifanya kazi kampuni ya Ujenzi ya KONOIKE mjini Arusha lakini alilipwa mshahara na serikali bila kuufanyia kazi kupitia cheki namba 3781513. Fedha hii iliyolipwa kwa mtu ambaye hakufanya kazi zingeweza kununua madawati mangapi?

f)Tangu mwaka wa fedha 2010/11 Mkuu wa chuo amekuwa akilipwa tofauti na cheo chake. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2013/14 Mkuu wa chuo alilipwa kiasi cha Tsh 1,183,200/= zaidi ya alivyostahili. Kwa mwaka mmoja zililipwa kiasi cha Tsh 14,198,400 ambazo zinaweza kuchukuliwa kama malipo hewa. Hali ni hiyohiyo kwa mfano tena, mwaka 2011/12 Mkuu wa chuo alitakiwa kulipwa Tsh 3,330,700/= kwa mwezi, lakini alilipwa kiasi cha Tsh 4,303,400/= kwa mwezi na hivyo kwa mwaka huo zililipwa kiasi cha Tsh 14,006,880 kama malipo hewa kwa mkuu wa chuo. Fedha yote hiyo ingeweza kununua madawati mangapi?

g) Sehemu kubwa ya matumizi ya fedha za chuo ni kwa ajili ya shughuli za kuendesha chuo (malipo kwa ajili ya Bodi ya chuo, malipo ya safari za uongozi wa chuo, Mafuta na matengenezo ya magari yanayotumiwa na viongozi wa chuo allowance mbalimbali za uongozi wa chuo) na siyo kwa ajili ya kufanyia mambo ya taaluma (training materials, technical materials, teaching materials nk)

Yote haya yamefanyika wakati chuo kina Bodi ya Uongozi lakini Bodi inakuwa na kigugumizi kwa kuwa sehemu kubwa ya Wajumbe wa Bodi hiyo ni watu/ndugu wa karibu na Mkuu wa chuo. Kwa mfano, Mkuu wa chuo ni Mushi, wajumbe wa Bodi ni Lema, Makileo, Ukio, Mosha, Njau na Nyahumwa akiwa school mate. Hivyo inaonekana kuwa msingi wa mambo kufanyika kwa njia ya kutafuta ni wapi pana fedha ya kuchukua/kuiba ni Bodi ya Chuo.
 
 
ndio maana tulimchagua Dr Magufuli kuwa mtawala wa TZ ndio atatuvusha kwenda nchi ya ahadi
 

Acha kujikomba mwanaume hajikombi anajenga hoja. Wewe kuna siku utampelekea........ Kwanza Mungu hayupo!
 
kwa mtu unaechukia bila kujua unacho chukia huwezi sema amejitahidi,ila kidogo amejitahidi!
 
Kuna baadhi ya mambo namuelewa ila ktk kuminya demokrasia simuungi mkono kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…