Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kila mtetea mafisadi, wala rushwa anajitahidi kujitokeza kumtisha Dkt Magufuli kwa kadri anavyoweza. Ila wasichokijua na kuwa Dkt Magufuli na serikali hawatishwi hata kidogo, ndiyo kumekucha kabisa, vita dhidi ya mafisadi na wala rushwa ndiyo vinashughulikiwa kwenda mbele na kila jiwe lazima lipinduliwe ili nchi irudi kwenye mstari wa uadilifu.

Mwl Nyerere aliwahi simulia hadithi akisema rais anapokuwa katangaza vita na mafisadi na wala rushwa watajitokeza wachache wa kumtisha, kwanza watapiga makelele HILOOO, HUYOOOO, baadaye wakiona hatishiki wataanza kusema CHINJA CHINJA. Sasa baada ya wapinzani kuona rais hatishiki, wamekuja na staili mpya, ila uzuri ktk ile hadithi ya Mwl Nyerere anasema kijana yule hakugeuka nyuma bali aliendelea na hatimaye kuleta ukombozi.

Nasisi tunasema Dkt Magufuli GO! GO! GO!
 
Naunga mkono mapambano ya ufisadi, lakini ningependa zaidi yafanyike kwa uwazi, mimi nimeshangaa sana serikali kuzuia bunge kwa sababu zisizo na kichwa
 
Sikutegemea, rais aliyesimama imara dhidi ya majizi, walanguzi, madalali wa resources zetu, mafisadi na wahujumu uchumi, wapiga fursa za ujanja, eti asipate ugumu, eti asikutane na magugu eti asipambane na hali ngumu na hao wahujumu uchumi na wauza unga
Rais shikilia hapo hapo wananchi wa kawaida na watu wenye kuona mbele wako nawewe mkuu, hawataweza hata siku moja kukwamisha juhudi zako, waliotaja rais mwenye mamuzi ya papo kwa papo ndio wanaolia leo kwa sababu watu wenye kuwapa hizo dili wamehamia kwao na hakuna dili tena, hao wamarekani wanaanza kuchombeza unafiki kwa lengo lile lile walilofanya libya, hawataweza kwetu, wao wasubiri tu kuona stanbic bank yao ikiendelea kuzolota na mikataba ya madini sasa itawekwa kwa kipimo cha faida na sio walivyozoea, uwanyime wauza unga fursa utegemee kuongoza nchi kirahisi? No, uwazibe midomo walafi utegemee kuvuka kirahisi? No, uwatumbue nawakala wa ufisadi na kuanzisha mahakama kwa ajili yao utegemee kuongoza kirahisi? No, lakini mwisho wa yote tutavuka

Mtemi Nyakarungu
 
hhahah vipi bado unaandika haya kiongozi?
 
Mwl.Nyerere alikuwa na akiri sana, hata wakimwita nduli JPM ni rais shupavu kabisa, na ni lazima kila mtu hata vile vinavyofikiri vinaweza kushindana na serikali vifike hatua vielewe mkuu wa nchi ni nani, raisi ni nani na serikali ni nani. Serikali imara haimuogopi mtu wala kikundi chochote cha kihuni, naomba hiyo tarehe ifike ili wapuuzi wa Ukuta wapewe somo la kihistoria
 
Nimekua najiuliza sana,Huyu Mungu ni mwenye upendo kiasi gani,mbona huwakumbuka watu wake wakati muafaka wamuitapo?Magufuli,amefanya mambo makubwa ndani ya miezi 9 tu,

1. Elimu bure

2. Kila mwanafunzi anakalia dawati

3. Amefufua shirika la ndege ATCL, amenunua ndege 3

4. Ameanzisha mahakama ya mafisadi

5. Watu wanatii Sheria tena bila shuruti

6. Amekusanya kodi kwa kiwango cha juu sana haijawahi tokea

7. Wale matajiri sasa ni vichaa

8. Tanzanite sasa huuzwa live tena kwa mnada

9. Serikali yote Dodoma

10. Viwanda vinajengwa kwa kasi

Sasa wewe unaepinga nabaki na maswali mengi juu yako, wewe ni kibaraka wa nani?
 
Ninaunga mkono mambo yote mazuri serekali ya awamu ya tano chini ya Mheshmiwa,Mtakatifu Dr Magufuli inayoyafanya.Kuanzia kufufua shirika letu la ndege,kurejesha nidhamu ya matumizi serekali,kuendesha zoezi la kutafuta wafanyakazi hewa ingawa nilitarajia wale wote waliohusika na mzimu huu wakifikishwa mahakamani na nk.

Napinga kitendo cha serekali ya awamu ya tano kuminya demokrasia kwa namna yoyote.Sipendi jeshi la polisi kujihusisha na masuala ya siasa,sipendi uvunjifu wa katiba kwa kisingizio cha uchochezi wakati vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria na kazi yake kubwa ni kukosoa serekali.
 
elimu bure?
 
Kiukweli nimefatilia kuchunguza interest za wananchi wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe magufuli upo sahihi kabisa kwa kila hatua unayo chukua. Sisi wananchi, humu humu jamii forum, tulilalamika eti awamu ya nne walisafiri sana nje ya nchi. Mpaka magazeti yakawa yanaandika hii ni ziara ya 365 kwa Jk kwenda nje na gharama zake na kweli ulikuwa ukisoma gazeti unaona logic ya gharama zenyewe. Leo hii, watu wale wale wanasema Mheshimiwa hata aendi nje ya nchi? Watanzania interest zetu ni nini? Go magufuli, you are doing the right thing.
 
hahahahahahahahahahahaha
 
Akili za ukawa ndiyo zilivyo wao kulalamika ni jadi YAO daima.
 
Ndugu yangu hamna kazi ngumu kama kumuongoza Mtanzania, naomba niishie hapa
 
Wakiitwa nyu.mbu wanalalamika. Tanzania hii haiendelei hata siku moja kwa mentality hizi.

Juzi tu hapa Maalimu kaitwa shujaa kwa kukataa kushika mtu mkono, tena kwenye msiba...siku chache baadae Lowassa kaitwa 'mwenye busara, mkomavu kisiasa' kwa kusalimiana na Magufuli.

Hatujui tunachotaka.
 
Hata hii teua, thibitisha, tengua ipo sahihi kabisa. Hii nchi kuna watu waliweka mazoea mabaya sana hasa viongozi wa umma. Walijaa viburi na kejeli za kila aina. Hivyo kwenye hili pia mi naona upo sahihi kabisa.
 
ndio maana sikushangaa mh.JK kupewa nishani ya uongoz bora barani africa kama watanzania ndivyo tulivyo

hakuna tunachotaka.,mtu akianzisha tunafuata nyuma kama mikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…