Moja ya simulizi ninayoipenda ktk biblia takatifu na vitabu vya kiada za neno la Mungu ni simulizi ya uasi wa shetani dhidi ya Mungu. Ikumbukwe kuwa jina halisi ya shetwani au Ibilisi ni Lusifa. Lusifa alikuwa ni malaika mkuu kule mbinguni alikuwa ni moja wa kiumbe muhimu na wa karibu sana na Mungu km ingekuwa ktk muundo wa serikali yetu hapa nchini huyu Lusifa angeweza kuitwa Waziri Mkuu, Lusifa alikuwa ni mchapakazi hodari alipendwa na Mungu na hata malaika wenzake moja sifa pia ya huyu Lusifa alikuwa muimbaji mwenye sauti ya kuvutia, Lusifa aliweza kutoa sauti mwaroro saba tofauti akawa kiumbe muhimu ktk uongozi mbinguni lakini cha ajabu baada ya Lusifa kupata sifa zote hizo akaja kujawa na kiburi na dharau. Kumbukeni sisi wakristo tunaamini ktk utatu mtakatifu Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho mtakatifu kitu pekee kilichomfanya Lusifa kuasi ni uroho wa Madaraka akitaka afanane na Mungu na kuanza mashindano na Mungu na kujiona yeye ni bora kuliko kiumbe chochote mbinguni na Duniani jambo lilifanya Lusifa kuasi na kushawisha nusu ya theluti mbili ya Malaika kumuunga Mkono wakadhani wangeweza kuangusha ufalme wa Mungu kisa hiki wengi mwakifahamu, kwanini nimekitumia kisa hiki? Hapa Tanzania kuanzia Mwaka 1995 tulitengeneza kiongozi mwenye ulka ya Lusifa ndani ya Chama Cha Mapinduzi huyu kiongozi kiukweli alijitahidi kujipambanua kuwa ni mchapakazi, jasiri, mpenda watu na hasa wanaccm, Kiongozi huyu alipata ushawishi mkubwa toka kwa wafuasi, wapenzi, washabiki na wanachama wa ccm akaaminika na kupewa vyeo mbalimbali ndani ya chama na serikali hadi kufikia ngazi ya Waziri Mkuu. Kiongozi Hutu akajipa kiburi kuwa bila yeye hakuna ccm akawashawishi mashabiki wake kuanzisha vita na Mkiti wa ccm Taifa na Rais wa JMT Dr Jakaya Kikwete. Mambo yalipomshinda kiongozi Huyo alliwashiwishi watu muhimu ndani ya chama na kuhasi chama wakaondoka mpk waasisi wa Tanu na ccm akiamini kuwa kuondoka kwako ingesambatisha ccm. Lusifa Huyu wa Tanzania akatupwa nje ya ccm na malaika zake lakini ccm bado imara. Tutakukumbuka daima Dr Jakaya Kikwete kwa uzaledo wako kwa wana Tanzania kuokoa Tanzania toka mkononi mwa iblisi wa bongo na malaika zake. Ukitaka kuepukana na inzi hakikisha unaondoa uvundo ndani ya Imaya yako. Lusifa wa Bongo sasa amebaki anawaywaya kila kona akiwarubuni watanzania kuwa alionewa ndani ya ccm. Enyi wana wa Tanzania tujiunge psmoja kumpiga vita Lusifa asije akawarubuni na kuwapeleka moto wa Jehanam. Mungu Ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais Wetu Dr John Pombe Magufuli