Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Nini maana ya kulinda rasilimali?

Mimi naamini ni uwendawazimu kushabikia bomba la mafuta la Uganda ambalo tutalipwa ushuru tu wakati tulikuwa na nafasi ya kupata mapato makubwa zaidi kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kuwezesha uvunaji wa rasilimali za madini na gas.

Uganda wanamiliki 15% kwenye mafuta yao kwa kulipia hisa, sisi tulikuwa na sheria inayoipatia serikali umiliki wa bure 10% na kuruhusiswa kuwa na umiliki mwingine mpaka 15% kwa kununua hisa, lakini tunasema tunaibiwa. Maana yake ni kuwa mwenye umiliki wa 15% haibiwi ila mwenye umiliki wa 25% anaibiwa!

Tumelazimisha umiliki wa bure wa 16% na mrabaha wa 7% (6% royalty, 1% inspection fee), kila nwekezaji anaondoka. Wapya hakuna. Uwekezaji wa dola billion 30 ($30bn) umeenda Mozambique. Miradi ya gas Tanzania imesimama.

Kwangu mimi msimamizi wa rasilimali zetu mzuri ni anayewezesha rasilimali hizo kutumika kubadilisha maisha ya wananchi kwa kujenga na kuimarisha sekta nyingine za uchumi na huduma.

Dunia haisimamia kusubiria gas yako. Watu hawalali, kuna siku itakuja gas itakuwa haina maana kwa sababu nishati nyingine rahisi na nafuu zaidi zitakuwa zimegundulika.
 
Mi sioni cha maana kilichofanyika.. zaidi zaidi anazidi kutuondoa kwenye reli. Mwaka 2020 utafika na hakutakuwa na kitu tangible kilichofanikiwa zaidi ya hizi hadithi zenu za kila siku. ushuzi mtupu
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
Imagine,,tangu November 2016 una LIKES 5 tuu???????
 
*TANGU RAIS MAGUFULI AINGIE IKULU ... ~ Prt 3*

Tuendelee kuchambua mambo 10 mengine yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dk. John Pombe Joseph Magufuli* tangu alipoingia Ikulu mnamo Novemba 5, 2015. Leo tutamulika kuanzia nafasi ya 20 mpaka ya 30.

Tangu Rais Dk. Magufuli aingie madarakani tumeyaona haya yakitokea na kufanyika:-

21. Tumeshuhudia Rais Magufuli akifanya maamuzi magumu, ya haraka, sahihi na kwa wakati pindi Wananchi inapolalamika juu ya kukabiliwa na tatizo la kijamii. Ilishatokea kwenye hospitali ya Muhimbili pindi Mwanamama alipopaza sauti juu ya akina Mama wanaojifungua kulala chini, hapo hapo Rais Magufuli akaamuru zilizokuwa ofisi zibadilishwe na kuwa wodi, ikafanyika hivyo. Pia tusisahau Rais Dkt John Pombe Magufuli alivyowapa wakazi wa Bagamoyo, eneo la Magereza lenye ukubwa wa heka 65. Huyo ndio Dk. John Pombe Magufuli, mwenye maamuzi magumu, sahihi na kwa wakati.

22. Serikali ya Rais Magufuli imekuwa na desturi njema ya kulipa madeni ya ndani na ya nje. Mathalani tumesikia Serikali ikilipa madeni ya ndani ya Wakandarasi, watoa huduma, Waalimu n.k. Pia hivi karibuni Serikali kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Serikali imesema imetenga Tsh. Trilioni 1 kulipa deni la Taifa.

23. Serikali ikiacha umangi meza na kwenda palipo na Wananchi, palipo na shida za jamii. Si Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, wa Mkoa, Mawaziri ama Makatibu wakuu wote wapo field kuhakikisha wanaenda kuzitambua na kuzitatua shida za Wananchi. Mtindo wa viongozi kubaki baki ofisini zaidi kuliko kuwa site ulishakufa tangu Rais Dk. Magufuli alipoingia Ikulu.

24. Urasimu kuwaona Viongozi umepungua; Miaka ya nyuma kumuona Kiongozi wa Serikali ilikuwa kazi ngumu kuliko hata kuisaka sarafu baharini, huo ndio ukweli. Viongozi walio wengi walijiwekea ukuta kiasi Mwananchi wa kawaida kumvikia ilihitaji uvumilivu wa hali ya juu. Tangu Rais Magufuli aingie viongozi wenyewe wa Serikali wameweka mfumo mpya wa kiutendaji kwa kutenga siku maalum (siku 2 ama 3 kwa wiki) ambazo Mwananchi anaenda kumuona kiongozi moja kwa moja pasipo kupita kwa Katibu Muhtasari (Sekretari). Pia wapo baadhi ya Viongozi wakubwa wa Serikali wanatoa mpaka namba zao za simu za mikononi ama za wasaidizi wao ili Wananchi waweze kuwasilisha kero na matatizo yao moja kwa moja. Utaratibu huo umerahisisha matatizo ya Wananchi kuweza kufika kwenye mamlaka kwa wakati na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

25. Viongozi wamepewa meno zaidi; Tangu Rais Magufuli aingie madarakani tumeshuhudia Viongozi, mamlaka za kitaasisi zikipata meno zaidi ya kiutendaji tofauti na hapo awali kila kitu kuachiwa mamlaka ya Urais iamue, ulikuwa ni utegeaji wa hali ya juu. Mathalani leo hii tunashuhudia TAKUKURU ikipata meno zaidi ya kupambana na rushwa nchini hali iliyopelekea kesi za rushwa kuongezeka Mahakamani.

26. Kiwango cha nidhamu, uwajibikaji na uadilifu kwa Viongozi wa Serikali kimezidi kuongezeka. Tangu Rais Magufuli aingie madarakani yale mazoea yasiyo na tija ya viongozi kuzoea kazi hayapo, ule mtindo kiongozi akiharibu hapa anahamishiwa kule haupo, suala la kiongozi anafanya madudu na bado anabaki kwenye ofisi ya umma haupo tena. Kila Kiongozi ama kila Mtumishi wa umma yupo makini akichapa kazi vilivyo kwa nidhamu na uadilifu wa hali ya juu.

27. Ufuatiliaji wa utendaji, ufuatiliaji wa maagizo umekuwa wa hali ya juu. Tangu Rais Magufuli aingie Ikulu ameiambukiza sifa zake za uadilifu, uchapakazi, uzalendo na ufuatiliaji. Naam ufuatiliaji wa majukumu, maagizo, ripoti na tafiti zinazotolewa umekuwa wa hali ya juu. Pindi inapobainika madudu kufanyika ama jambo kutokufanyika kwa wakati Rais Magufuli hasiti kabisa kufukuza Mtu na baadhi yao kuishia mikononi mwa vyombo vya kisheria.

28. Utawala wa Sheria umezidi kuimarika. Rais Magufuli aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi iliyo na sheria, taratibu na kanuni, amefanikiwa katika hilo. Leo hii tunazidi kuona mihimili ya dola inapofanya kazi kiukamilifu pasipo mwingiliano, kila mhimili upo huru; Leo hii tunaona Viongozi, Wanasiasa, Watumishi wa umma wakipandishwa kizimbani na wengine wanahukumiwa kifungo jela pindi wanapokutwa na makosa ya kisheria. Hakika, utawala wa kisheria unaoonyeshwa na Serikali ya awamu ya 5 yake Rais Magufuli ni nguzo ya utawala bora.

29. Heshima ya Tanzania kimataifa imezidi kukua zaidi; Hali ya Tanzania kusikika zaidi ilikuwa juu sana kipindi cha awamu ya kwanza kutokana na uwepo wa Mwalimu Nyerere ambapo hii leo Tanzania imezidi kupata sifa zaidi kutokana na uchapakazi wa Rais Magufuli. Nchi mbalimbali Duniania zimekuwa zikivutiwa na Rais Magufuli kutokana na namna anavyopambana na rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya pesa za umma, namna Serikali inavyobana matumizi na namna Rais Magufuli anavyoonyesha uzalendo wa kulinda rasilimali za Taifa zimnufaishe Mtanzania. Hayo ni baadhi tu ya mambo yanayoifanya leo hii jina, hadhi na heshima ya Tanzania kuweza kupaa juu zaidi tangu Rais Magufuli aingie Ikulu.

30. Heshima ya Mwanamke imezidi kuimarika Serikalini na kwenye jamii. Dalili njema za Rais Magufuli kuweza kuheshimu nafasi ya Mwanamke ilianza kujitokeza pindi alipomteua Mama Samia Suluhu kuwa Mgombea mwenza wa Urais ambaye leo hii ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mama Samia ni Mwanamke pekee aliyeshika nafasi ya juu kabisa kiungozi katika nchi za Afrika Mashariki. Hata mara baada ya kuingia Ikulu Rais Magufuli ameongeza imani kwa kuwateua Wanawake kwenye nafasi mbalimbali za kiuongozi Serikalini. Pia amewateua na kuwapandisha vyeo kwenye nafasi za vyombo vya dola na hata wengineo kuwateua kuwa Majaji. Imani aliyoonyesha Rais Magufuli kwa Wanawake ni ishara tosha ya heshima kubwa aliyowapa Wanawake nchini.

*Na Emmanuel J. Shilatu*
 
Haijawahi tokea na haitotokea mchukieni amasishaneni kumtukana na kumnanga ila huyu Rais ana akili sana. Ana akili mpaka anawatafakarisha wale wanamchukua poa.

Rais Genius wa tanzania ndie rais pekee africa alie ingia ikulu nakukuta haina kitu pasipo kutukana wala mshambulia mwenzake alie ondoka akaziangalia fursa na sasa nina vyoandika hazina ina mzigo wakutosha kwa kipindi kifupi.

Genius Dr Magufuli ndie rais alie wafanya mafisadi wote Tanzania kukaa chini nakujikuta wakifanya majumba yao kuwa mahabusu zao za ndani. Jinsi anavyo deals namafisadi nataka kukuambia ewe mtanzania embu muombea huyu Rais maana hamjuwi kinaendelea pale kiotani. Watu wanaomba poooo Magufuli usione Lowasa alienda ikulu ukafikiri alitamani hapana pooo ndio iliompeleka ikulu. Magufuli nikichwa na nina takakuwaambia tumuombee watu wanasema poooo pooo Mzee tulitenda dhambi na vyombo vyetu vya ulinzi vinakazi nzuri Mpaka mvua yabaraka inashuka juu ya taifa.

Rais Magufulindie rais watanzania uwenda kwa sasa vyombo vingi vya kijasusi duniani vinafuwatilia mode ya uongoz wake na jinsi anafanikiwa maana haijawahi tokea na wanapata shida kwa uwezo anao ktk nyanja ya kiutendaji. Vyombo kama M6, KGB,CIA and MOSSAD ndio vyombo kwa sasa vinamtafakari kiongoz shupavu wa afrika ambaye amekataa mkate na asali ya ugaibuni na kwa sasa anavaa nguo za kitanzania na misos ya kibongo unapita wapi...

Rais Genius kutekeleza miradi mikubwa ya kujenga vinu vikubwa vyakufuwa umeme wa maji, Rel ya kimataifa, kuunda jiji la dodoma na majengo makubwa ya serikali na mambo mengine ndugu hajawahi tokea kiongoz kama huyu mwenye speed ya ajabu ktk kutekeleza miradi yamaendeleo.

Ununuzi wa ndege na meli kubwa kule Mwanza kwakweli inawatafakarisha wenye akili nakuamini kweli Tz imepata baba wa Taifa.

Jinsi ameushika upinzani pabaya ndio maana wanahaha kumsumbuwa ili wajifilie kwakufungwa chama lao waseme amewaonea ila kifo chao kitakuwa ktk kura 2020.

Magufuli amepita wote na baada yake hatokuwepo kwa miaka kadhaa na wale mnawaona wanafanana naye nataka kuwaambia sio kweli this men is unique created by God.

Mungu tunasema Asante kwa Rais wajamuhuri ya watu watanzania Dr John Pombe Magufuli
 
Wapinzani wanakukera nini wewe. Na upinzani ukifa unafaidika nini. Nchi uinaangamia wewe unachekelea! So sad
 
Ni genius kweli

Kafuta agenda ya ufisadi Kwa wapinzani
Kafuta Wiz wa Mali za UMMA
Kila nchi inataka uongozi wake
Watu wanamsingizia mambo mengi yupo kimya Tu haha
 
s
Haijawahi tokea na haitotokea mchukieni amasishaneni kumtukana na kumnanga ila huyu Rais ana akili sana. Ana akili mpaka anawatafakarisha wale wanamchukua poa.

Rais Genius wa tanzania ndie rais pekee africa alie ingia ikulu nakukuta haina kitu pasipo kutukana wala mshambulia mwenzake alie ondoka akaziangalia fursa na sasa nina vyoandika hazina ina mzigo wakutosha kwa kipindi kifupi.

Genius Dr Magufuli ndie rais alie wafanya mafisadi wote Tanzania kukaa chini nakujikuta wakifanya majumba yao kuwa mahabusu zao za ndani. Jinsi anavyo deals namafisadi nataka kukuambia ewe mtanzania embu muombea huyu Rais maana hamjuwi kinaendelea pale kiotani. Watu wanaomba poooo Magufuli usione Lowasa alienda ikulu ukafikiri alitamani hapana pooo ndio iliompeleka ikulu. Magufuli nikichwa na nina takakuwaambia tumuombee watu wanasema poooo pooo Mzee tulitenda dhambi na vyombo vyetu vya ulinzi vinakazi nzuri Mpaka mvua yabaraka inashuka juu ya taifa.

Rais Magufulindie rais watanzania uwenda kwa sasa vyombo vingi vya kijasusi duniani vinafuwatilia mode ya uongoz wake na jinsi anafanikiwa maana haijawahi tokea na wanapata shida kwa uwezo anao ktk nyanja ya kiutendaji. Vyombo kama M6, KGB,CIA and MOSSAD ndio vyombo kwa sasa vinamtafakari kiongoz shupavu wa afrika ambaye amekataa mkate na asali ya ugaibuni na kwa sasa anavaa nguo za kitanzania na misos ya kibongo unapita wapi...

Rais Genius kutekeleza miradi mikubwa ya kujenga vinu vikubwa vyakufuwa umeme wa maji, Rel ya kimataifa, kuunda jiji la dodoma na majengo makubwa ya serikali na mambo mengine ndugu hajawahi tokea kiongoz kama huyu mwenye speed ya ajabu ktk kutekeleza miradi yamaendeleo.

Ununuzi wa ndege na meli kubwa kule Mwanza kwakweli inawatafakarisha wenye akili nakuamini kweli Tz imepata baba wa Taifa.

Jinsi ameushika upinzani pabaya ndio maana wanahaha kumsumbuwa ili wajifilie kwakufungwa chama lao waseme amewaonea ila kifo chao kitakuwa ktk kura 2020.

Magufuli amepita wote na baada yake hatokuwepo kwa miaka kadhaa na wale mnawaona wanafanana naye nataka kuwaambia sio kweli this men is unique created by God.

Mungu tunasema Asante kwa Rais wajamuhuri ya watu watanzania Dr John Pombe Magufuli
sawa haya nenda kajojoe ukalale
 
Hata mimi nimeona anaakili mpaka Bashite anamtawala,na ameumbwa na huruma sana,amerudisha siasa ya kutaifisha na huku anyaka wawekezaji,wapinzani hoi huku anataka kuombewa,amelazimisha jengo lililotumoa sh bilioni 3 la CRDB kwa utafiti wake,amjenga uwanja wa ndege chato kwa kipindi cha miezi sita ni ndege yake pekee imetua,amenunua dawati bila madarasa, Acasia inauza migodi ili kujitarisha kufungua kesi na yeye anasubiri malipo,ningeendelea kumsifu jinsi alivyo na akili lakini
 
Nilijarib kufanya utafit Wang binafs, nikagundua jpm anapendwa sana na wananchi japokua watendaji kazi wake wanao msaidia ndo wana mwangushaxna, na kufanya wananchi baadhi kuilaum serkar ya jpm .ww kam maana jforums una maoni gan? Una mkubr au
 
Labda unampenda wewe na mkeo
 
Back
Top Bottom