Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Habari wakuu,

Kama tuna kumbukumbu kidogo miaka ya nyuma tatizo la mgao wa umeme lilikuwa kama kansa inayoitafuna nchi hii nchi ilikuwa haimalizi mwaka bila kuwa na mgao wa umeme mara maji Mtera yamepungua mara hivi mara vile yani zilikuwa sarakasi zisizokuwa na mwisho kiasi cha kwamba wajanja wacheche walijinufaisha kupitia tatizo la upungufu wa umeme.

Tumeshuhudia mikataba mingi mibovu iliyoitikisa nchi na kulitia taifa aibu na hasara ya hali ya juu. Tumeshuhudia mikataba kama Richmond na Escrow ikiingizia taifa hasara kubwa sana na kusababisha baadhi ya mafisadi kama mzee lowassa kujiudhulu na baadae kukimbilia katika CHADEMA baada ya kutambua hakuna nafasi ya madudu chini ya mh rais Magufuli.

Tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani zaidi ya miaka mitatu nyuma, suala la mgao wa umeme limekuwa historia.

Mh. Rais amejitahidi sana kumaliza tatizo hili hivyo kupelekea kuleta unafuu kwa viwanda ambavyo viilikuwa vinatumia gharama kubwa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta pia kuwaondolea hasara waliokuwa wanapata wafanyabiasha ndogo ndogo kama mabutcher, wauzaji wa soft drink pamoja na wamama wauza mabarafu na ice cream.

Vijana na wananchi wengi tunakubali sana utendaji wa mh Rais hatuyumbishwi na wazurulaji watanzania tunataka maendeleo
Nchi gani hyo maana Mimi nipo MASASI hapa mtwara umeme ni changa namba mbili baada ya maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu since Mh magufuli aingie lini kulikuwa na mgao wa umeme
Waulize wakaazi wa dDAR NILIKUWA HAPO WIKI JANA MITAA YA TGT MBONA UMEME HAUKWEPO KUANZIA SAA 4 ABH HADI SAA 10 JIONI SIWEZI SMA MGAO LABDA ILIKUWA HOTILAFU
 
Habari wakuu,

Kama tuna kumbukumbu kidogo miaka ya nyuma tatizo la mgao wa umeme lilikuwa kama kansa inayoitafuna nchi hii nchi ilikuwa haimalizi mwaka bila kuwa na mgao wa umeme mara maji Mtera yamepungua mara hivi mara vile yani zilikuwa sarakasi zisizokuwa na mwisho kiasi cha kwamba wajanja wacheche walijinufaisha kupitia tatizo la upungufu wa umeme.

Tumeshuhudia mikataba mingi mibovu iliyoitikisa nchi na kulitia taifa aibu na hasara ya hali ya juu. Tumeshuhudia mikataba kama Richmond na Escrow ikiingizia taifa hasara kubwa sana na kusababisha baadhi ya mafisadi kama mzee lowassa kujiudhulu na baadae kukimbilia katika CHADEMA baada ya kutambua hakuna nafasi ya madudu chini ya mh rais Magufuli.

Tangu utawala wa awamu ya tano uingie madarakani zaidi ya miaka mitatu nyuma, suala la mgao wa umeme limekuwa historia.

Mh. Rais amejitahidi sana kumaliza tatizo hili hivyo kupelekea kuleta unafuu kwa viwanda ambavyo viilikuwa vinatumia gharama kubwa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta pia kuwaondolea hasara waliokuwa wanapata wafanyabiasha ndogo ndogo kama mabutcher, wauzaji wa soft drink pamoja na wamama wauza mabarafu na ice cream.

Vijana na wananchi wengi tunakubali sana utendaji wa mh Rais hatuyumbishwi na wazurulaji watanzania tunataka maendeleo
Masenu njaa tu zinakusumbua.

Kwa akili kama hizi Mkeo akipata mimba utampongeza rais kwa juhudi zake za kuhakikisha "mnafyatua" ili asomeshe bire

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
unazungumzia mgao wa umeme sehemu gani mkuu? mkoani najua kunasehemu umeme ni kishefuchefu na wana bwawa
 
Tangu aingie madarakani rais John Pombe Magufuli,amefanya mambo mengi mazito,mazuri na ya ajabu kwa kiwango chake.
Pamoja na mambo anayoifanyia nchi yetu kuwamekuwa na baadhi ya watanzania wenzetu ambao wao wameamua kuziba macho na kutokuona lolote jema alifanyalo.
Ukweli ni kuwa mh rais Fanya kazi ambayo kila mtanzania anaiona hata wale wanaojifanya hawaoni ipo siku kama si mioyoni mwao watatamka hadharani kwamba wewe ulikuwa rais makini,mzalendo,mchapa kazi na mwadilifu.
Sifa ya mwanadamu ni kukataa kilichopo,Ila siku kikitoka atakitamani tena kwa sifa kemu kemu.Asili ya watanzania tunaijua,ni wanafiki,wavivu,waongo,wafitini na wapenda vya dezo.
Pambana jemedari wetu siku ukiondoka madarakani tutayataja mazuri yako ya kununua ndege,kujenga madaraja,kutoa elimu bure,huduma za maji,afya na umeme,kuondoa uzembe kazini,uzalendo usio na shaka,uaminifu na uadilifu wako katika utumishi Wa umma.
Usiogope kusemwa,hata aliyewaumba wanadamu anasemwa,tena kwa kashifa,wewe ni zaidi maana ni mwanadanu tu unaishi Leo kesho haupo.Timiza wajibu wako kwa watanzania na Mungu atakubariki.
Viva Maguduli,daima mbele,nyuma ni mwiko.
 
Ndugu msiwe na jazba tafadhali hebu mpeni nafasi ajieleze kidogo,
Ndugu mtoa mada wewe unakaa wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mimi nakaa sinza e hakuna mgao wa umeme dar nzima hakuna mgao wa umeme watu wanashindwa kutafautisha mgao na umeme kukatika kutokana na matengenezo kama kusogeza nguzo kupisha upanuzi wa barabara au kubadilisha nguzo zilizochoka
 
Kinachoendelea Tabata kila J4 na J5 ni mgao wa pipi?
mkuu embu jifunze kutofautisha kati ya mgao na umeme kukatika kwa ajili ya matengenezo na maboresho ya huduma kama kubadilisha nguzo na kusogeza nguzo kupisha ujenzi wa barabara
 
Back
Top Bottom