OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kesho ni Mai Mosi ambapo kimsingi unategemea kusikia maazimio mazito kutoka kwa TUCTA juu ya mambo ya msingi katika kusimamia maslami mapana ya wanachama wake.
Wanachama wao wamekuwa na changamoto kadhaa zisizo patiwa majibu na serikali. Moja ya kilio kikubwa ikiwa na kikokotoo cha kifisadi.
Kwenye mambo ya msingi wa kuundwa kwao huwezi kuwasikia. Utawaona tu wakigawa tshirt kuelekea Mei Mosi. Utawaona wakigawana posho nene nene kwa ajili ya misafara ya sherehe za Mei Mosi ambazo hazina tija tena.
Hata kesho hatutegemei jipya zaidi ya hotuba za kuandikiwa na CCM kwa ajili ya kujipendekeza kwa Mheshimiwa.
TUCTA na watu wao kina TUGHE nk ni vyema wakabadilisha usajili ikawa Chama cha kugawa Tshirt badala ya kupigania maslahi ya wanachama.