Ni kweli- mke akimjali na kuonyesha confidence kwa mumewe katika kila alifanyalo, humpa ari zaidi na msukumo unaopelekea mafanikio.
Hata hivyo inabidi kuweka angalizo: Kuna wanaume unaweza kuwaonyesha kuwaamini, na wapo ambao huwezi kuwaamini.Hwa wanatakiwa kuchungwa kama watoto maana ukiwapa kisogo tu umeumia. Hawa ni wale wasiojituma kwa lolote au wasioweza kujua vipaumbele ni vipi. Ukiwachekea na kuwaacha wafanye watakalo kwa kuogopa kuonekana una gubu basi utashangaa maana familia yako itakuwa mkia kila siku!
Je wanaume hawa wa kundi la pili wanatakiwa kufanywaje? Kipi bora kuwachochea waweze kuamka na kufanya lolote au kuwaacha wapotee?