Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 2,620
- 6,780
Watu wengi wanaifahamu demand and supply kama concept inayohusiana zaidi na biashara na uchumi. Lakini je, tumewahi kujiuliza kama kuna uwezekano kwamba dhana hii ina maana pana zaidi inapohusishwa na maisha ya mwanadamu na mchango wake katika Dunia?
Skia sasa, katika nyuzi nyingi nilizowahi kuandika humu ndani, nimekuwa nikieleza kwamba hakuna mtu aliyezaliwa bahati mbaya katika hii Dunia. Kila mtu ana eneo ambalo anaweza kutoa mchango wake, kwa namna moja au nyingine, katika kuifanya Dunia iwe sehemu bora, yenye furaha na salama zaidi kwa watu kuishi.
Na kwenye hili eneo la utumishi huwa kuna watu walio katika kundi la high priority, wengine wako kwenye kundi la medium, na wengine wako kwenye kundi la average.
Tofauti yao haionekani katika uwezo walionao, bali pia katika namna wanavyoelekezwa, wanavyopata nafasi na jinsi wanavyokuja kutambulika katika maeneo wanayohusika nayo.
Ili tuelewane vizuri hapa, wacha tuchukulie mfano wa mpira wa miguu.
Ukiangalia katika historia ya Dunia wapo watu wengi ambao wamecheza mpira. Lakini tunapozungumzia majina kama Pelé na Maradona, tunakuwa tunazungumzia watu ambao mchango wao umevuka mipaka ya kawaida ya kushiriki mchezo na kufanya majina yao yawe sehemu ya historia ya mchezo wenyewe.
Vivyo hivyo, katika muziki wa reggae, Bob Marley amebaki kuwa alama kwenye eneo hilo, tangu 1980 hadi leo vijana waliozaliwa miaka 2000 ukiwatajia hilo jina wanaelewa ni nani huyo mtu, lakini pia tunaona katika hip-hop, Tupac Shakur ana nafasi isiyofutika kwa mashabiki wengi wa muziki huo. Na katika filamu za mapigano, Bruce Lee aliacha alama iliyovuka mipaka ya uigizaji na kadhalika.
Kimsingi ukiangalia ni kwamba watu wengi walikuwepo katika maeneo hayo, lakini si wote waliokuja kuacha alama inayofanana.
Hapa ndio unaweza ukajiuliza sasa. Ni nini kinachomfanya mtu mmoja awe sehemu ya historia ya eneo fulani, wakati mwingine anashiriki eneo hilo hilo lakini maisha yake yanabaki katika kiwango cha kawaida?
Jibu ndio lile nimelisema hapo juu, ya kwamba kuna watu wako na high priority, medium na wale wa average.
Hawa wote safari zao huwa hazifanani, kuanzia kutoka kundi hadi kundi ila pia kutoka mtu hadi mtu.
Kwasababu kuna wale ambao demand yao ni kubwa so hii inafanya uwezo wao uweze kuonekana mapema, kuna wale ambao wanahitaji muda, mazingira na demand ili uwezo wao ujidhihirishe. Na kuna wale ambao wanaweza kutumia muda mrefu wakitafuta mahali ambapo kile walichobeba kinaweza kupata nafasi ya kutumika (hawa ndio wale wa average sasa)
Hawa wa kundi la mwisho ndio walionifanya niandike huu uzi.
Kwa sababu hili ndio kundi ambalo watu wake wanaweza kuishi hadi kufa pasipo kujua wapi wanapaswa kuhudumu na hii yote ni kwasababu ni kundi lenye watu wengi na ni rahisi kujikuta kwenye eneo moja na ikapelekea iwe ngumu kutumika.
Na hapo ndipo dhana ya demand and supply inapoingia.
Kimsingi huwa universe inanamna ya kutufanyia maamuzi pale ambapo inataka kututumia na katika nyakati hizi ndio huwa kuna mambo mengi yanaweza kutokea katika namna ambayo si ya kawaida na walio wengi katika matukio ya nyakati hizi ndio hujikuta wakiamini kwamba kweli Mungu yupo.
Kwamfano unaweza kuwa unaishi mkoa fulani, hali yako ya kiuchumi ikiwa ngumu. Na katika nyakati hizi unaweza kuwa na watu wengi unaowasiliana nao, lakini hakuna anayekuwa katika nafasi ya kukusaidia kwa wakati huo.
Kisha ghafla, mtu ambaye hukumuweka hata kwenye hesabu zako anakutafuta na kukuambia uende alipo. Anakupa nafasi ya kukaa, unapata mazingira mapya, unakutana na watu wengine, na baada ya muda unajikuta ukiingia katika shughuli ambayo hukuwa na mpango wa kuifanya.
Na haimaanishi kwamba once ukifika mahali fulani ndio kila kitu kitabadilika mara moja. Wakati mwingine unaweza kukaa miezi kadhaa, au hata mwaka mzima, kabla hujaelewa kwa nini uliishia kuwa katika mazingira hayo.
Na haya ndio mambo ya ki hatima yanavyokua, na haya ni matukio ambayo mtu anapokutana nayo anapaswa aujue kwamba kuna possibility kubwa ya kwamba yupo kwenye hatua ya mabadiliko kwenda kwenye msimu mpya na kitu cha ukizingatia ni kwamba si lazima mwelekeo huo wa msimu uonekane wazi tangu mwanzo, wala si lazima kila mtu auelewe kwa wakati huo huo ila uhalisia hauwezi kubadilika.
Kwasababu wakati mwingine tunaelewa maana ya jambo baada ya kupita ndani yake. Wakati mwingine tunalitambua baada ya miaka kadhaa. Na wakati mwingine tunaweza kuendelea kuishi bila kujua ni kwa namna gani matukio fulani yalichangia kutufikisha tulipo.
So, kitu cha muhimu hapa ni kujua kwamba maisha yana patterns na Kila pattern huwa inamaana kubwa katika kuiendea hatima yako.
Na nikisema hatima namaanisha hakika na hakika huwa haiingii kwenye tatizo kwa maana kila tatizo huwa halikosi kuwa na suluhisho ila ukiona tatizo lipo na unalijua ni tatizo ila unashindwa kupata suluhu yake jua hiyo ni hakika na ikishakua hakika jua ni hatima na hatima haibadiliki.