Ibrahimeliza
Member
- Nov 25, 2020
- 37
- 26
Hivi ushawahi kujiuliza miaka ya nyuma namaanisha karne kadhaa zilizopita, watu walikuwa wanafanyaje biashara
Je, walikuwa na mawazo makubwa ya biashara kama sisi? Walikuwa wanawekeza katika biashara? Walikuwa wanajifunza vipi biashara? Shule? Kwakurithi? Moja kwa moja kwa mfanya biashara...?? Walikuwa wanafanyaje biashara? Walikuwa wanafanya matangazo? Wanashirikiana kwenye biashara?
Turudi nyuma kidigo kama sio sanaa, hivi ushawahi kujiuliza, miaka mingi iliyopita kabla ya watu kuanza kulima, embu vuta picha unaamka katika zama za kuwinda na kukusanya matunda na mizizi.
Vuta picha unaamka asubuhi katika kibanda namaanisha nyumba, unapoishi na familia yako unachukua upinde na mshale wako unajiandaa kwaajili ya kwenda kuwinda kutafuta kitoweo (chakula) kwaajili ya familia yako na jamii iliyokuzunguka, unaaga familia yako kisha unaenda kwa baba juma kumpitia, unafika kwake unamkuta mkewe kisha anakwambia baba juma kaenda bondeni, pembezoni kidogo na sehemu ya makazi yenu.
Unafika unamuona baba juma anachimba chini kisha anafukia, anafanya hivyo tena amachimba kisha anafukia, tena na tena na tena, unamsalimu kisha unamuuliza unafanya nini hapo baba juma,
Baba juma; nalima bwana.
Wewe; unalima? Ndokufanyaje hukoo.?, kwahiyo vipi kuhusu kuwinda leo...?? Na kukusanya matunda je?
Baba juma;; Ndiyo siendi leo, huku kulima kutanipa matunda ya mwaka mzima kwahiyo sitohitajika tena kwenda mbali kwaajili ya kukusanya matunda.
Wewe;; Sijakuelewa bwana, yani huko unapokuita kulima unafukua kisha unaweka tunda chini halafu unafukia ndokutakupa matunda ya mwaka mzima?
Baba juma;; Ndiyo, ya mwaka mzima sitohitajika kwenda mbali kwaajili ya kukusanya matunda.
Unahisi wewe utamuelewa baba juma?, utahisi kapataje wazo kama hiloo? Mbona kama anafanya mzaa? Kweli kufukua, kuweka mbegu kisha kurudishia kutaweza kutulisha kama jamii? Utajiuliza maswali mengi sanaaa.
Lakini, hatimae muda wa mavuno umefika, hapo ndounaanza kumuelewa baba juma na jamii yote inaanza kuelewa kuhusu kulima sasa, shukrani kwa baba juma jamii inanufaika hata kama haikumuelewa awali.
Vipi kuhusu zama za viwanda? Mapinduzi makubwa ya umeme, Watu wanaweza kudhania umeme ulikuwepo miaka elfu moja nyuma au miaka mia tano, Hapana unamkumbuka Thomas Edison mwanasayansi aliyegundua umeme ilikuwa ni miaka ya tisini tu hapo, inastaajabisha mafanikio makubwa na yote haya ya viwanda, umeme haujaanza muda sanaaa, embu fikiria kwamba mtu unabonyeza batani tu umeme unawaka ilikuwa ajabu kiasi gani kwao?
Fikiria ilikuwa ngumu kiasi kama ukitaka kuwasiliana na ndugu zako mpaka utume barua ambayo huenda ikachukua hata miezi kumfikia na kurudisha majibu itachukua miezi tena mpaka majibu yarudi, kama mkeo au mwanao akipata tatizo asubuhi kama ushatoka mpaka urudi ndoujue au anaweza akafariki asubuhi kama ushatoka mpaka urudi ndoujue, uchungu kiasi gani kwasasa hivi tunaona yalikuwa maisha magumu kiasi gani, watu wanatembea na kufanya shughuli zao bila simu mkononi au mfukoni, hivi kwazama za sasa mtu aliyezoea Instagram, Facebook, Twitter, Jamii forum na mitandao mengine mingi ataweza kuishi katika zama hizo?
Kwenye ulimwengu wa bila simu? Wala mitandao ya kijamii?, Hakika mambo ndivyo yalivyo zama zinabadirika, muda unakwenda na taratibu za maisha zinabadirika pia, jamii zinabadirika kifikra, kimtazamo, kimionekano, na hata katika utendaji wao na mfumo wao wa maisha kiujumla hata tamaduni pia zinabadirika.
Wakati kila zama zinapobadirika kuna watakao faidika zaidi na hiyo zama na kuna watakao baki nyuma na hii ndo sheria ya ulimwengu ilivyo kuna watakao tangulia na kuna watakao chelewa lakini cha umuhimu wote tutafika.
Historia ni alama ya mafanikio na mafanikio yanaacha alama, tunajifunza nini kama mtu mmoja mmoja? kama familia? Kama jamii? Kama nchi? Kwa wenzetu walio tutangulia? Katika biashara? Kiuchumi? Kijamii? Tunajifunzaje kwawaliotutangulia?
Hivi hakuna zama au miaka ambayo tulikuwa sawa na mataifa makubwa kiuchumi? Ilikuwaje tukawasawa? Wametupita wapi? Walifanyaje fanyaje? Kuna mbinu zozote? Tunaanzia wapi? Tutaweza kumudu? Tunaweza kuanza? Mbona tunazidi kuwa nao mbali? Kuna ujanja wanaotumia?
Fikiria hayo mafanikio yanasababu nyingi, ila wote kama nchi au jamii tunaweza kufanikiwa,Ndiyo tunaweza tukiamua tunaweza.
Chakuzingatia hakuna mafanikio yakikundi ila kuna mafanikio ya mmoja mmoja simahanishi watu wawe wabinafsi, hapana ila namaanisha kila mtu anatakiwa ajitume katika kutoa mawazo, mchango wake katika jamii.
Tumia akili ya mwanao au tumia akili ya kitoto kufikiria hili, vuta picha tumekusanya pesa za watu wote tanzania za bakhresa, mo dewji, rostam, gsm, diamond, harmonize, ally kiba, ya mama muuza vitumbua, jirani yako, fikiria pesa za watu wote tumekusanya halafu tuzigawe sawa sawa, mfano kila mtanzania katika mgawo apate millioni moja.
Hivi jiulize baada yamuda unaweza ukampita mo kwa hela kama mkianza sawa? Vipi kuhusu bakhresa? Mama muuza vitumbua atampita gsm? Unahisi kwanini?
Ninachojua pesa itarudi katika mfuko ulio toka, sijabahatisha najua hilo kwasababu mafanikio yanamfata mtu kivipi?
Ahsanta..🇹🇿✉💼

Upvote
2