Mafao kwa watumishi wa sekta binafsi kusubiri mpaka miaka 55 ni wizi usiovumilika

Mafao kwa watumishi wa sekta binafsi kusubiri mpaka miaka 55 ni wizi usiovumilika

Wangooto

Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
20
Reaction score
5
MAFAO WATUMISHI SEKTA BINAFSI KUSUBIRI MPAKA MIAKA HAMSINI NA TANO NI WIZI USIOVUMILIKA

Utaratibu huu ulikuwepo zamani kwa watumishi wa sekta binafsi kuchukua mafao au michango yao mara tu wanapoacha au kuachishwa kazi. Mwenendo huu uliwasaidia sana watumishi hawa kujipatia kipata kujiendeleza baada ya kupoteza vibarua vyao.

Hali hii ilikuja kubadilika bada ya kutungwa kwa sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ambapo hivi sasa kwa Waajiriwa wa Sekta binafsi wale ambao ni Skilled (Wenye ujuzi) hawaruhusiwi kupatiwa pesa zao zote isipokuwa kuna kitu kinaitwa "Fao la Kupoteza Ajira" ambalo utolewa kwa Mtumishi aliyepoteza kibarua kulipwa asilimia thelathini na tatu (33%) ya Mshahara wake. Kitu ambacho si sawa kabisa na ukizingatia vibarua vingi huwa ni vya mkataba wa mwaka mmoja.

Ombi:-Wanasiasa waache kuleta sheria kandamizi na kuja na jibu muafaka litakalorejesha matumaini ya watumishi wa sekta binafsi.

Huwezi niambia kuwa nisubiri hadi nifikishe miaka 50 ndio nichukue mafao yangu wakati sina kibarua cha uhakika.
 
Back
Top Bottom