"Kwa nini hela zangu zitungiwe sheria za ajabu?" Amesikika mdau mmoja aliyeachishwa kazi na bahati mbaya kupata ajira nyingine imekuwa ngumu kwake.
Alipofuatilia mafao yake NSSF kaelezwa akae miezi sita ndio atalipwa stahiki zake na atakuwa akilipwa asilimia 33 ya mshahara wake wa awali
Huyu ndugu kakata tamaa na analaani waliopitisha sheria iliyoondoa FAO la kukosa ajira kwani ana akiba yake NSSF lakini anateseka na familia yake. Nani awe sauti ya wanyonge kama hawa? Nani awasaidie kupaza sauti zao ili sheria kandamizi kama hii ifutwe kabisa ili watu wapate haki zao kwa muda mwafaka wakajifanyie shughuli mbalimbali za maendeleo?
Nani anajali?