KERO Mafao ya Wanajeshi waliopigana vita ya Kagera imekuwa ahadi isiyotekelezeka

KERO Mafao ya Wanajeshi waliopigana vita ya Kagera imekuwa ahadi isiyotekelezeka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mwezi Julai 2025 ndipo ahadi ya Serikali kuwalipa mafao wastaafu wa jeshi waliopigana vita ya kagera.

Taratibu za kuwakusanya wazee hao zolifanyika uku wakitoka sehemu mbali mbali za nchi na kukusanyika mahali walipo pewa taarifa kukutana ili wapate mwongozo.. wakapewa mwongozo wakafungua account za benki.. wakapiga na picha ( passport Size) na kuahidiwa muda si punde pesa zitaingizwa kwenye account.

Hadi leo wazee wanasononeka na kusema kwanini walitudanganya, wangetuacha tuendelee na maisha yetu tuliyokuwa nayo tumezoea kuliko kutudanganya.. tumeuza mifugo, tumeuza shamba kupata nauli na pesa za kufungulia account za bank pasipo mafanikio.

NI KILIO CHA MMOJA WA WASTAAFU WA JESHI LA JWTZ ALIYEPIGANA VITA YA KAGERA NA HAKUPATA MAFAO HADI SASA.

Pia soma ~ Mwigulu Nchemba: Maveterani wa Vita ya Kagera wataanza kulipwa mwaka huu wa fedha
 
Back
Top Bottom