- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimesikia na kuona vipande vya video fupi vikidai Mafinga ilinyesha Mvua iliyosababisha barafu kuzagaa mitaani hadi baadhi ya maeneo barabara zikawa nyeupe, nimeona video hizo ila nikapata ukakasi isijekuwa ni video za nje ya Tanzania zimewekewa sauti tu.
Je, ni kweli hapo ni Mafinga na kulitokea barafu hizo?
Je, ni kweli hapo ni Mafinga na kulitokea barafu hizo?
- Tunachokijua
- Mvua ya baarafu ni matone yanayodondoka kutoka angani na kufika katika uso wa dunia kama mvua katika mtindo wa barafu
Kumekuwepo na picha na vipande vya video vikionesha hali ya uwepo wa barafu iliyotokana na mvua zikiwa zimeambatana na ujumbe unafafanua kuwa hali hiyo imetokea Mafinga mkoani Iringa. Video hizo zipo hapa, hapa na hapa. Miongoni mwa waliochapisha mapema picha na video kuhusiana na tukio hilo ni Mufindi Fm Redio ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Iringa.
Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa inayopatikana nchini Tanzania huku pia ikiwa ni miongoni mwa mikoa yenye baridi kwa kiwango cha juu.
Ukweli Upoje?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa suala hilo na kubaini kuwa ni la kweli na limetokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa ikiwemo eneo la Changarawe.
JamiiCheck imepata taarifa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya kuaminika ambavyo vipo Mafinga Iringa ambavyo vimethibisha kuwa tukio hilo ni la kweli.
Aidha, katika video zilizopo mtandaoni, tulibaini kuwa Mufindi Fm ya Iringa waliweka picha na kipande cha video mapema zaidi kabla ya sehemu nyingine kikionesha uwepo wa barafu hizo barabarani na kwenye maeneo ya makazi ya watu, ambao nao Wamethibitisha kuwa ni kweli, na walibainisha kuwa kumekuwa na mvua mkoani humo kwa siku ya 30.09.2024 na 01.10.2024 ikiwemo mvua ya barafu kama inavyoonekana kwenye picha hizo na video.