KWELI Mafinga imenyesha Mvua iliyoambatana na Barafu

KWELI Mafinga imenyesha Mvua iliyoambatana na Barafu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimesikia na kuona vipande vya video fupi vikidai Mafinga ilinyesha Mvua iliyosababisha barafu kuzagaa mitaani hadi baadhi ya maeneo barabara zikawa nyeupe, nimeona video hizo ila nikapata ukakasi isijekuwa ni video za nje ya Tanzania zimewekewa sauti tu.

1000151137.jpg


Je, ni kweli hapo ni Mafinga na kulitokea barafu hizo?


 
Tunachokijua
Mvua ya baarafu ni matone yanayodondoka kutoka angani na kufika katika uso wa dunia kama mvua katika mtindo wa barafu

Kumekuwepo na picha na vipande vya video vikionesha hali ya uwepo wa barafu iliyotokana na mvua zikiwa zimeambatana na ujumbe unafafanua kuwa hali hiyo imetokea Mafinga mkoani Iringa. Video hizo zipo hapa, hapa na hapa. Miongoni mwa waliochapisha mapema picha na video kuhusiana na tukio hilo ni Mufindi Fm Redio ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Iringa.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa inayopatikana nchini Tanzania huku pia ikiwa ni miongoni mwa mikoa yenye baridi kwa kiwango cha juu.

Ukweli Upoje?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa suala hilo na kubaini kuwa ni la kweli na limetokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa ikiwemo eneo la Changarawe.

JamiiCheck imepata taarifa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya kuaminika ambavyo vipo Mafinga Iringa ambavyo vimethibisha kuwa tukio hilo ni la kweli.

Aidha, katika video zilizopo mtandaoni, tulibaini kuwa Mufindi Fm ya Iringa waliweka picha na kipande cha video mapema zaidi kabla ya sehemu nyingine kikionesha uwepo wa barafu hizo barabarani na kwenye maeneo ya makazi ya watu, ambao nao Wamethibitisha kuwa ni kweli, na walibainisha kuwa kumekuwa na mvua mkoani humo kwa siku ya 30.09.2024 na 01.10.2024 ikiwemo mvua ya barafu kama inavyoonekana kwenye picha hizo na video.
Baadhi ya maeneo ya Mafinga Mjini, mkoani Iringa, jana yamepata mvua za barafu ambayo kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wakisema haijawahi kutokea huku wakiifananisha na ile ya nchi za Ulaya.

Siku ya jana Oktoba 1, ilinyesha mvua hiyo ya barafu na kusababisha theluji kutanda barabarani na kwenye paa za nyumba.

Hali ya hewa ya wilaya hiyo imekuwa na muonekano karibu sawa na ule wa Ulaya kipindi cha baridi.
 

Attachments

  • FB_IMG_1727887406019.jpg
    FB_IMG_1727887406019.jpg
    37 KB · Views: 8
Nimesikia na kuona vipande vya video fupi vikidai Mafinga ilinyesha Mvua iliyosababisha barafu kuzagaa mitaani hadi baadhi ya maeneo barabara zikawa nyeupe, nimeona video hizo ila nikapata ukakasi isijekuwa ni video za nje ya Tanzania zimewekewa sauti tu,

Je, ni kweli hapo ni Mafinga na kulitokea barafu hizo?

Utawasikia TMA nchini wanajitokeza na kukanusha kama ile ya Njombe 2022
 
Sifa zisizo na maana, hapo sio ulaya hata kwa ndoto tu hapawezi kufanana na ulaya wenye ulaya yao wanawacheka kwa dharau sana

Sifa zisizo na maana, hapo sio ulaya hata kwa ndoto tu hapawezi kufanana na ulaya wenye ulaya yao wanawacheka kwa dharau sana
Ndiyo maana kasema kama Kwa kumanisha kafananisha na ulaya ambako mara nyingi ndiko swala la barafu hujitokeza
 
Mitaa hiyo lawaida tu kipindi cha baridi,ukiskia mvua ya mawe ni hizo barafu zinadondoka km mvua.
Huwa hazikai hata,zikimwagika zinaondoka.ni vibarafu vidogo kmpunje ya mahindi
 
Back
Top Bottom