BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Wakati mgomo wa wafanyabiashara katika soko kuu Mafinga mkoani Iringa ukiinga siku ya nne nne leo, wafanyabiashara wa matunda, nafaka pamoja na samaki wamelalamikia wakisema mgomo huo unawaathiri kibiashara.
Mgomo huo umesababisha adha kwa wananchi na wafanyabiashara wasio na maduka, wakisema wanayategemea maduka hayo kupata bidhaa za kuuza.
Mwenyekiti wa soko hilo, Philinus Mgaya amefafanua kuwa wafanyabiashara hao wamefunga maduka kutokana na kupanda kwa kodi ya pango ya vibanda hivyo Sh80,000 jambo ambalo wamedai bei hiyo ni kubwa kwao.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba alipoulizwa kuhusu mgomo huo, leo Jumatatu Agosti 26, 2024 amemtaka mwandishi kuwauliza wafanyabiashara wenyewe.
“Mimi sina majibu, wafanyabiashara ndio wanaweza kuwa na majibu ya mgomo huo kwa sababu wao ndio wameutengeneza,” amesema Serukamba.
Akizungumzia mgomo huo, mjasiriamali wa matunda, Alice Mwagala amesema changamoto ya kufunga maduka hayo imeleta athari kubwa kwao kwa kuwa wanauza bidhaa za vyakula zinazoharibika haraka.
“Tunaomba Serikali isikilize kilio cha wafanyabishara kwa sababu tunapoteza mitaji na hatuelewi tutapata wapi, ukizingatia wengi wetu tuna marejesho ya Vicoba,” amesema Mwagala.
MWANANCHI