HABARI zinazotoka chunguni zikiwa bado moto kabisa ni kwamba sasa mafisadi wamenuia kwa udi na uvumba kuteka nyara na kumiliki kila kampuni inayohusiana na masuala ya simu na intaneti nchini.
Kwa mujibu wa habari hizo kampuni ya simu iliyoingiza njia mpya ya mawasiliano hapa nchini inamilikiwa kwa kiini macho na Watanzania waliokuwa katika nyadhifa za juu nchini miaka si9 mingi iliyopita na hivi sasa wamegeuka wafanyabiashara wakubwa vyanzo vya mitaji yao vikiwa havijulikani.
Hata hivyo inasemekana wamiliki halisi ni mafisadi wale wale wa EPA na waliokwishachota fedha kwenye mabenki, chama fulani cha kisiasa na ambao wana monopoly haramu kwa baraka za serikali zilizotoka na iliyoko madarakani.
Nia ya jamaa hawa ni kuhakikisha kuwa wanashika biashara yote ya serikali ikiwemo shule za msingi na sekondari na vyuo vikuu ili wachune buzi na kuamka matajiri kwa kwenda mbele milele.
Hata hivyo, inafahamika fika kwamba vyuo vikuu vikipewa vianzio vyenyewe vina uwezo wa kuwa watoaji huduma za intaneti na mawasiliano mengine.
Kwa njia hiyo vyuo vikuu vitakuwa sio tu vimeepuka gharama zitakazobebeshwa na mafisadi hawa bali pia vitajitengenezea pato sio haba na kupambana vyema na ukata unaokabili vyuo hivyo.
Hili, hata hivyo linakuwa gumu kwa sababu ya kizito mmoja katika wizara ya elimu ambaye anasifika kwa kupenda kitu fedha na amewaweka hata viongozi wa juu mikononi mwake. Ofisa huyo anang'ang'ana kwamba lazima vyuo vinunue huduma za intaneti na televisheni na redio toka kwa washirika wake wa kisiri kibiashara.
Inaaminika Ikulu na Rais mwenyewe hawana habari kabisa na ishuu hii (ambayo kama ile ya sekta ya madini, nishati na mali asili) habari anazopata zinaonesha kila kitu ni safi lakini mambo yemeoza na wale anaooamini wanamsaidia kuonekana kiongozi bora ndio wanaomfanya aonekane kiongozi wa ovyo kabisa.
Kiongozi huyo katika wizara ya elimu ana sifa ya kuwasomesha watoto wake wenye bongo lala sio tu kwenye vyuo vikuu nchini bali hata nchi za nje. Na kutokana na ushawishi na fedha aliyonayo husafiri hata nje kwenda kuona watoto wake wasio na akili wanafaulu kwa janja janja tupu!
Ni dhahiri kuwa kutokana na utatu huu usio mtakatifu kati ya mafisadi, makatibu wakuu wa wizara na wafanyabiashara laghai Watanzania wasitegemee nafuu yoyote kwenye sekta ya habari na mawasiliano.