Mafisadi wanainyonya KQ?

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
9,424
Reaction score
11,320
Nimestuka kidogo ndiyo maana nimeleta kama swali.
Inaeleweka kuwa umiliki wa KQ umegawanywa kwa GOK, KLM, KG lenders na public. Na inaeleweka kuwa si lazima shirika la ndege liwe na ndege zake lenyewe ili kujiendesha, linaweza ku-lease na biashara ikaendelea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka baadhi ya Wabunge na vyombo vya habari wanasema ndege nyingi za shirika la Ndege Kenya zinamilikiwa kwa siri na Wanasiasa au vigogo Serikalini. Hii haihusiani na ndege ambazo huwa tunaambiwa kwamba zimekuwa leased, hizi ni zile miongoni mwa ndege zinazosemwa zinamilikiwa na KQ. Ina maana kuwa kuna 'wajanja' huwa wanachukua chao mapema ndiyo maana Shirika likiyumba linapewa bail out.

Link hapo chini ya gazeti la Daily post imemnukuu Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji akishangazwa kuwa kumbe katika ndege 28 zinazofanya kazi ni ndege tatu tu ndiyo za KQ nyingine za 'cartels', politicians etc.
http://www.kenyan-post.com/2019/02/shock-as-it-emerges-kq-own-3planes.html

NB: Habari nyingine ni kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Kenya Aviation AUTHORITY pia ni Mwenyekiti wa bodi ya Commercial Bank of Kenya ambayo inamilikiwa na familia ya Kenyatta.

Kuna Watu wanakula mema ya Nchi duh!
 
Hakuna cha ajabu hapo Kenya ni capitalist na sifa kubwa ya ubepari ni kutegemea kodi tu from sekta binafsi

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Hakuna cha ajabu hapo Kenya ni capitalist na sifa kubwa ya ubepari ni kutegemea kodi tu from sekta binafsi

Sent using my iPhone using jamiiforum app

Capitalist wannabe.
Kama kuna kosa kubwa la 'Waswahili' ni kubebwa na fikra za ubepari kama fasheni.

Sina hakika kama umesoma nilichoandika na nilichoambatanisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
siku zote nimekua na mashaka na loss wanazopost KQ kila mwaka..........


ndio loss zipo, ila inaelekea loss zao zinakua juu sababu ya ufisadi uliokububu pale KQ........


wajanja watakua wanachukua faida yote then wanaandika loss........ uhuru na ubepari wote ule ile loss ya ksh4b aitazame tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…