kidunula1
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 6,305
- 6,341
Hivi Chama na Mafisango ni wachezaji wenye calibre zinanozoendana? Mbona wako tofauti sana? Chama si shughuli kama Marehemu Mafisango. Chama ni soft sana ukilinganisha na Mafisango, Chama si mkabaji sana kama Mafisango n.kMimi kama mpenda soka, shabiki na mwanachama wa klabu ya Simba naomba nizungumze kitaalamu sasa ili tuelewane naweka mihemko yangu pembeni maana najijua.
.
Mafisango ni binadamu aliyeleta ukamilifu wa neno KIUNGO WA KATI Katika soka la bongo aliutendea haki mpira Mafisango.
Miguu yake ilikuwa na maamuzi ya Kifaransa miguu ambayo inavutia kuitazama muda wote wa mchezo awapo uwanjani.
Mafisango alikuwa chini ya Milovan Cirkovic wakati ule ulikuwa unataka nini huwezi kukipata kutoka kwa Patrick Mafisango utaalamu wa chenga? Shahidi Shedrack Nsajingwa au Godfrey Taita kiungo wa chini mwenye akili ya mpira watakueleza.
Jezi yake namba 30 muda wote imelowa jasho, Jasho la ukweli.
Mwaka 2012 Patrick Mafisango na Mwinyi Kazimoto wakicheza nyuma ya Haruna Moshi Boban kuwazunguka Emanuely Okwi,Felix Sunzu na Uhuru Sulemani na kuipa adhabu Yanga kwa jumla ya goli 5-0 ilikuwa ni kazi ya Mafisango.
Leo hii tuna Clatous Chota Chama mchawi wa pasi kutoka Zambia unaifahamu Zambia?
Na Chama ndie Mafisango mpya moja kati ya viungo wenye uwezo mkubwa sana katika kulitendea haki eneo la kiungo la Simba kwa sasa mchezaji ambae hachoshi kumtazama awapo uwanjani and this was what Mafisango was doing.
Kwa sasa kikosi cha Simba kinabebwa sana na uwepo wa Clatous Chota Chama katika eneo la kiungo Chama anautuma mpira na mpira unamtii ni viungo adimu sana kuwahi kuonekana miaka ya hivi karibuni Simba inajivunia sana huduma ya Chama
Chama ni mtaalamu wa pasi za kila aina pasi za mbali na pasi fupifupi za karibu Chama kapunguza majukumu ya Jonas Mkude na kurahisisha kazi ya upachikaji magoli.
Chama Anakupatia Burudani uwanjani, pasi za uhakika na anafanya kila kiungo anaecheza kando yake kumiliki sehemu ya kiungo vyema yani wote kwa pamoja Chama anafunga magoli matamu (solo goal) hivi unataka nini cha zaidi kutoka kwa Clatous Chama?
Nimechoka na huyu ndiye Mafisango mpya. Rest easy Patrick