GE2025 Maftaha Nachuma: Nilihama CUF baada ya kugundua Viongozi walikuwa wanashirikiana na CCM

GE2025 Maftaha Nachuma: Nilihama CUF baada ya kugundua Viongozi walikuwa wanashirikiana na CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
"Nilikuja kugombea Mtwara wakati sina uhakika kama je wana Mtwara mtanichagua kuwa Mbunge ama lah, lakini kwasababu niliapa kwa Mwenyenzi Mungu wana Mtwara mlikuwa mnaonewa sana, wana Mtwara mlikuwa mnapigwa sana, Bodaboda walikuwa wanaonewa sana, barabara Mtwara kulikuwa hakuna, maji hayakuwepo, bandari ya Mtwara ilisahauliwa wakati ule, kila kitu kilikuwa kibovu Mtwara. Wakati kabla sijawa Mbunge mwaka 2015 Mtwara ilikuwa inatajwa kwenye utabiri wa hali ya hewa tu kwenye taarifa ya habari kwamba jua litachomoza Mtwara, litazama Kigoma kwa Zitto Kabwe

Soma pia:
Kazi ya kuwatetea Mtwara ni kazi ya Mwenyenzi Mungu, nikaamua kutafuta sehemu ya kufanyia siasa. Mimi ninayezungumza nilikuwa Makamu Mwenyekiti wa Tanzania wa CUF nikagundua kwamba viongozi wenzangu ninaopigana nao, usiku wanakuwa CCM, mchana wanakuwa CUF kuanzia Mwenyekiti wa Chama mpaka ngazi ya wilaya wakawa wanatuchezea Shere wakishirikiana kupora matokeo na ukimwambia Katibu wa Chama azungumze na Mkurugenzi atoe tamko, anazima simu nikabaini kwamba hiki sio Chama cha siasa nahamia ACT Wazalendo niongoze mapambano Mtwara."- Maftaha Nachuma, aiyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini na Makamu Mwenyekiti wa CUF akieleza sababu za kuondoka CUF na kujiunga na ACT Wazalendo jana Julai 12, 2025 kwenye mkutano wa hadhara Mtwara Mjini




​
Chanzo: Jambo Tv
 
Back
Top Bottom