Wakubwa Habari ya asubuhi
Gari ya jamaa yangu ni automatic transmission (sio manual), akipiga moto gari yake (hasa kwenye mlima) inastuck, inakuwa kama inagoma kupanda, hivyo anakuwa anakanyanga mafuta Kwa kuvizia vizia , akikanyaga mafuta sana (mlimani) gari inakuwa nzito, inagoma kwenda na hata kuzima, ikishazima akiwasha inaweza isiwake, mpaka ikae Kwa muda Ndio akiwasha inawaka na anaanza safari.
Aidha, gari likienda Mwendo mrefu, mfano 50km huanza kuonyesha taa za check engine, VSC na 4wd endapo ataendelea kuendesha gari litakosa nguvu/ litaanza kuonyesha kugoma kwenda - kama nilivyoeleza hapo juu, na wakati mwingine Ukiwa kwenye foleni ya muda mrefu gari huanza kuwasha taa zoote kwenye dashboard na hata kuzima, and kama halijazima ukikanyaga mafuta litaanza Mwendo Kwa shida Sana na kuchanganya taratibu
Au, iwapo litazima ikitaka kuwasha litashindwa kupiga starter, itabidi ukae kama nusu saa hivi na ukiwasha litawaka utaendelea na safari yako kwa umbali wa hata km 20 then Tatizo kusita kwenda speed linaanza tena.
Je Tatizo ni nini, ?