Mafundi nguo mna shida gani? Kama mshono huuwezi bora useme ukweli

Mafundi nguo mna shida gani? Kama mshono huuwezi bora useme ukweli

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Kuna baadhi ya mafundi nguo wanakwaza sana, unampelekea mshono vizuri anatazama anasema anaweza kushona anataja bei mnakubaliana, unalipia gharamaza awali, akija kukukabidhi hyo nguo bora ungevaa gunia tu kuliko kuvaa hiyo nguo anayokuwa kakushonea.

Sasa kuliko kuharibu nguo ya mtu ambaye kaingia gharama si bora useme huo mshono siuwezi, mtu unashonewa nguo kama mfuko wa sadaka.

Inakwaza sana, sas mie nitavaa nini kwenye sherehe leo.
 
Screenshot_20260827-090619_Chrome.jpg
 
Ndiomaana sipendi kushona aisee, au bora utafute mafundi wanaofahamika kwa kazi nzuri kuliko kujiokotea hawa wa vichochoroni, wengi ni mafundi njaa tu.
Kuna hii style ya kushona nguo titi linakuwa halielewek linatoka au limebanwa aseeh wanawake mnakosha sana 😂

Mlikuja na ile ya mpasuo mbele naona hainogi ikapotezewa sasa mpasuo pembeni ya paja afu uwe na upaja broiler
 
Mimi nilisha acha miaka mingi sana kushona.
Either ready-made au hata kitenge nikute kinachonifit tofauti na hapo hapana aisee.
 
Ndiomaana sipendi kushona aisee, au bora utafute mafundi wanaofahamika kwa kazi nzuri kuliko kujiokotea hawa wa vichochoroni, wengi ni mafundi njaa tu.
Njoo nikushenee wewe acha vurugu zako.
 
Back
Top Bottom