Mafundi Sanifu Maabara wa sekondari wamewakosea nini Walimu

Mafundi Sanifu Maabara wa sekondari wamewakosea nini Walimu

k-bee

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2017
Posts
1,023
Reaction score
1,185
Malenga wapya muhali gani?? Me muhenga naendelea vyema na ombi langu kubwa ni Mola atuvushe katika hali yetu ya Taifa kwa sasa.

Kuna uzi uliwekwa humu kama kero za mafundi sanifu maabara wakiiomba(kuitaka) serikali kuangalia upya maslahi yao na miundo yao ya mishahara na hata uboredhaji wa mazingira na vitendea kazi mahali pakazi.
Ajabu ni kwamba kuna watu wakajinasibu ni walimu wakiwashambulia Mafundi sanifu Maabara swali unalojipa/nalojipa kichwani ni kwamba Taifa letu kwa sasa lina changamoto kubwa sana ya AFYA YA AKILI...Jambo halikuhusu wewe unapondea kwanini wewe nawe usipambanie kada yako upate maslahi bora.

Walimu acheni utoto na muache roho mbaya na ndio mana jamii kwa sasa haiwaoni kama tumaini maana mmekuwa mkitumika kwa mengi na kisha kutupwa.

Mwalimu unatakiwa ujue maslahi ya Mafundi Sanifu Maabara yakiwa bora ni rahisi pia hata maslahi yako Mwalimu kutatuliwa maana Mwalimu na Fundi sanifu Maabara wanashirikiana katika ufundishaji.

Ukimsaidia Jirani kupata jua na wewe utapata mana sauti ikiwa moja baina ya Fundi sanifu maabara na Mwalimu basi ubora wa shule na Mafanikio ya shule yanakiwa makubwa.

NB: Walimu ungeni mkono mahitaji ya Mafundi sanifu Maabara nao wakuunge mkono katika mahitaji yako

"Mola ya Seva"
 
Back
Top Bottom