Mafundi uchwara wanavyotuulia magari yetu

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Nimemeki nimenunua gari nikaendesha wiki moja liko poa kila kitu kipo sawa.

Nikapata wazo kwakuwa nimenunua kwa mtu halafu mi siko deep na magari acha nilipeleke kwa fundi akaicheki ili kama kuna sehemu kuna tatizo tuliweke sawa.

Bwanawee baada ya kumpa fundi akaniambia matatizo lukuki mara stering rak mara bush mara nini. Nikamwambia poa we check nalo tu kinachofaa kubadilishwa badilisha ili litengemae.

Baada ya wiki jioni hii ndio natoka kulifata gari langu halipo tena kama vile. Kwanza ili kuondoka garage ilibidi ni busti betri kifupi betri imekufa. Gari haikai sailensa inazima. Dash bod taa ya eabag na abs haizimi. Stering ngumu kama fiat. Honi haipigi. Nimeambiwa tatizo inaweza kua sababu ya betri.

Walah nimerudi nayo nyumbani stress zimenijaa najuta kuipeleka kwa fundi yule
 
Fundi unakuta hajui kitu,akipelekewa hagomi kuichukua kazi,anadhani anatengeneza,kumbe anaharibu,yawezekana ungemsimamia,ungekua unampa maelekezo,sema uliondoka.
 
Pole mkuu, tafuta mafundi wa insta.

Kuna fundi wangu huyo akifungua engine akirudishia anabakiza nati kibao ukimuuliza anasema hazina kazi. Ukimwambia gari inagonga, yeye yuko tegeta ataondoka na gari yako hadi kiwangwa afu anarudi na mzigo eti ndo anasikiliza ajue tatzo ni nin.

Na hizo taa za abs sijui airbag kwenye dashboard yako ukimpelekea anakata mawasiliano tu zinazima anakupa uendelee kupiga misele.

Naamini ili umpate fundi bora ni lazima uingie gharama.
 
Mie waliniambiq engine ya VVTI huwa haifungiki ,,,lazima tu ikusumbue hata uliweka kila kitu kipya....!!!
 
Kwa ishu ulizotaja umeacha vipi gari Yako gereji wiki mzima?

Ule usemi WA mbuzi kafia Kwa muuza supu ndiyo gari yako walichoifanyia
 
Next time usiachie mtu gari.

Simamia gari yako. It mean alot.
 
Aisee pole.. Ukinunua gari kwa mtu ni bora mwanzoni umtumie fundi wake muuzaji mpaka utakapolizoea gari ndio uende kwa fundi mwingine..!
Gari ikianza kuwa na mafundi wengi nayo ni changamoto..!
 
Hilo la kutorudishia nati zote walizofungua huwa linakera sana. Jamaa kapeleka gari gareji, matokeo yake wamevunja senser ya oil kwenye engine, taa ya airbag inawaka, na sasa linaenda lita 1 kwa kilometa 3. Kaamua kulipaki tu.
 
Usiachie fundi gari, kama huna muda wa kukaa garage weka gari yako home hadi utapopata muda...

Kwanza huwa lazima battery wabadilishe, halafu lazima gari yako itumike kupigia misele...
 
Hapo umeibiwa betri, pia vifaa vingi umebadilishiwa. Pole mkuu. Upo mkoa ngano nikupe namba wa fundi wangu.
 
Masega washakula zamani
 
Wajameni, gari huwa haliachwi garage....hususani kwa hawa mafundi uchwara ambao leo yupo hapa, akiharibu kitu anahama...na hauna guarantee yoyote ya kumkamata..

Garage ambazo utalaza gari liwe salama na uwe na amani ni kwa car dealerships pekee mfano Toyota Tanzania, Nissan Tanzania nk,...

Huko kwingineko ukilaza gari kubaliana na matokeo


Ila, au basi..
 
Aisee nmecheka sana.....
 
Habari wakuu wapi ntapata mafundi wazuri wa Benz c class 180
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…