Mafundi Ujenzi punguzeni nongwa mnapokuja madukani na mabosi wenu

Mafundi Ujenzi punguzeni nongwa mnapokuja madukani na mabosi wenu

salama sk

New Member
Joined
Sep 24, 2026
Posts
2
Reaction score
1
Hii imekaaje, wafanyabiashara wenzangu wa maduka ya vifaa vya ujenzi?

Utakuta fundi amekuja dukani na bosi wake kununua vifaa. Ukimtajia bosi bei ya bidhaa, fundi anaanza kusema, “Mbona bei ni kubwa? Hatujawahi kununua kwa bei hiyo, punguza kidogo,” wakati bosi wake yupo kimya na hana tatizo na bei hiyo.

Hivi hali hii si ushirikina wa biashara?

Jamani mafundi, punguzeni nongwa mnapokuja madukani na mabosi wenu. Kama bosi ameridhia bei, msiingilie kwa kulazimisha bei ishuke.
 
Safi sana fundi.Unalazimishwa vipi kushusha bei? Maana yake huwa unajitajia tu bei atakae lainika apigwe.
 
Mafundi wengi wanajua bei za materials kuliko maboss.kwanza elewa kuwa mpaka boss kaja na fundi wake,jua kuwa walipanga ni Duka gani Lina vifaa bora na cheap.

Kwahiyo ukiona boss yupo kimya si kwamba anaweza toa hiyo hela bali anamwachia fundi jukumu zima
 
Mnauza bei kubwa sana vifaa vyenu ndio maana kujenga inaonekana ni anasa..
 
Fundi na boss wake = kitu kimoja
Siku hizi Kila boss ana fundi wake
Moja ya sababu ya mabosi wengi kuwa na mafundi wa kudumu ni
1.Ubora wa kazi
2.Uhaliisia wa bei
3.Uaminifu

Umesema mabosi Huwa wapo kimya ni kweli wanakuwa kimya kwa sababu cyo jukumu lake .jukum lake ni kufanya malipo kwa sababu ana mtu tayar .
 
Hii imekaaje, wafanyabiashara wenzangu wa maduka ya vifaa vya ujenzi?

Utakuta fundi amekuja dukani na bosi wake kununua vifaa. Ukimtajia bosi bei ya bidhaa, fundi anaanza kusema, “Mbona bei ni kubwa? Hatujawahi kununua kwa bei hiyo, punguza kidogo,” wakati bosi wake yupo kimya na hana tatizo na bei hiyo.

Hivi hali hii si ushirikina wa biashara?

Jamani mafundi, punguzeni nongwa mnapokuja madukani na mabosi wenu. Kama bosi ameridhia bei, msiingilie kwa kulazimisha bei ishuke.
Huwa unamuuliza bosi sababu ya kuja na fundi hapo dukani kwako? Ukute bosi yuko nae kimkakati kujua bei halisi ya kifaa na ubora unaotakiwa kupitia fundi wake
 
Maduka mengi ya hadware wamiliki wameruhusu masalange wakae nje ya duka kudaka wateja hawa ndo wezi kama muunzisha mada huyu. Ndo maana binafsi nikitaka kununua ma hadware naenda zangu kwa Maghembe muuzaji maarufu wa mahadware.
 
Ungeandika kichwa kiseme “Fundi supportini wizi wetu sisi wauzaji wa vifaa vya ujenzi”
 
Back
Top Bottom