Huwa unamuuliza bosi sababu ya kuja na fundi hapo dukani kwako? Ukute bosi yuko nae kimkakati kujua bei halisi ya kifaa na ubora unaotakiwa kupitia fundi wakeHii imekaaje, wafanyabiashara wenzangu wa maduka ya vifaa vya ujenzi?
Utakuta fundi amekuja dukani na bosi wake kununua vifaa. Ukimtajia bosi bei ya bidhaa, fundi anaanza kusema, “Mbona bei ni kubwa? Hatujawahi kununua kwa bei hiyo, punguza kidogo,” wakati bosi wake yupo kimya na hana tatizo na bei hiyo.
Hivi hali hii si ushirikina wa biashara?
Jamani mafundi, punguzeni nongwa mnapokuja madukani na mabosi wenu. Kama bosi ameridhia bei, msiingilie kwa kulazimisha bei ishuke.