SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hapa nitaongea kwa ufupi sana na hii mada inawahusu mafundi wa aina zote hasa wale wanaokuja majumbani au maofisini kufanya matengenezo fulani kuanzia mafundi ujenzi, wapakaji rangi, fundi umeme hadi fundi wa maji.
Kuna mambo mawili ambayo yanakera sana ambayo wanafanya mafundi wa Kitanzania.
Kwanza, ni ishu ya kutofanya usafi baada ya kumaliza kazi. Mafundi wetu hawa hawadhani kuwa ni wajibu wao kuacha pasafi mazingira waliyofanyia kazi. Hili nimeliona hata kwa wale ninaodhani watakuwa wamepitia mafunzo. Nashauri vyuo vya ufundi vifundishe na kusisitiza utaratibu sahihi wa fundi kufanya kazi iliwemo kuacha mazingira safi baada ya kazi.
Pili, ni suala la kuondoka na vifaa vya mteja. Anaweza kuja kubadili au kufix kitu fulani, akimaliza kazi wengi wana tabia ya kuchukua kifaa alichobadilisha. Usipokuwa makini, kama siyo kifaa chote basi kuna kitu alichobadili atabeba bila kuomba au kutoa taarifa.
Kwa leo nitagusia hayo tu.